in , ,

Argentina

Lionel Messi

Shujaa wa Kombe la Dunia? Hata ushindi kwa Messi hautaokoa hali hii

LIONEL Messi atakuwa kwenye fainali zake za tano za Kombe la Dunia, baada ya kufika fainali 2014, lakini hajapata kutwaa ubingwa huo wa dunia.

Buenos Aires wanaye Diego Maradona mpya kwa ajili ya Kombe la Dunia. Yanaonekana ni mambo makubwa, japokuwa ni dhahiri si yule wa 1986 wakati Maradona akifanya mambo yake kwa kiwango cha hali ya juu na mwanga safi ukiangazia.

Badala yake, Buenos Aires imeenda kwa mfumo wa toleo la Italia 90, wakijidai kwa jezi za buluu iliyoiva, nywele zikiwa zimenyolewa katika mtindo wa kisasa. Ni wakati huu Maradona alifanikiwa kuwaongoza Argentina kwenye fainali nchini Italia, akifanya makubwa kama vile kutoa pasi ya aina yake kwa Claudio Caniggia dhidi ya Brazil.

Hata hivyo, alikuwa tayari ameonekana mwenye vituko, akitumia muda mwingi wa fainali hizo si katika kucheza soka, akizunguka zunguka na kusababisha matukio, akibishana, kudanganya , huku kila mpira ukisimama akionekana kutoa madai kwa hasira.

Binafsi nilipenda zaidi ilivyokuwa Marekani 94, wakati Maradona, walau alionekana kuwa mwenyewe, alipofunga bao zuri dhidi ya Ugiriki, Argentina wakianza kwa pasi kali kasha akamalizia kwa kutia mpira langoni kwenye kona ya juu. Si wengi wanapenda kuzungumzia hilo, lakini kulikuwa na chembechembe za madawa.

Picha yote hii maana yake ni kwamba Kombe la Dunia la mwaka huu nchini Qatar ni la kwanza katika miaka 44 bila Maradona ama kucheza au kutazama majukwaani kama alivyofanya mara ya kwanza, akiruka kwenye eneo la waandishi wakati Argentina wakipata tabu kupambana na Iceland.

Mwishoni mwa mechi hiyo, Maradona, inaaminika alikuwa ametumia nguvu kubwa kuliko Lionel Messi, aliyeonekana kuchoka huko Urusi; na anatarajiwa kushiriki kwenye mashindano haya na huenda yakawa ya mwisho kwake.

Hakika, hii inaweza kuwa kwa namna moja au nyingine. Ama Messi atakuwa mwokozi huko Qatar, ikiwa atasakata soka lake tamu na kufanya mashindano yawe mazuri au anaweza kuwa kana kwamba haonekani uwanjani kwa kukosa ufanisi.

Katikati ya kelele zote hizi, kuna suala moja la heshima, kwamba huenda hakika ukawa mwaka wa Messi. Ni kwa mara ya kwanza wakati wa fainali za Kombe la Dunia anakuwa timamu kimwili, akitoka kwenye nusu ya msimu akiwa na mabao ya kufunga pamoja nay a usaidizi. Anaelekea kuwa amepata tena uwezo wa kufanya mambo yake makubwa aliyozoea nyakati zilizopita.

Kuna mtazamo potofu kwamba hili limepatikana klatika hali ya ushindani miongoni mwa wafanyakazi wa kilimo, kwamba Ligi Kuu ya Ufaransa nib utu, iliyo kana kwamba kwenye suala la wafugaji. Ukweli ni kwamba Ligue 1 ni kali na yenye wachezaji wenye tamaa ya kufanya makubwa

Messi ana umri wa miaka 35, nab ado anaonekana kuwa mchezaji bora duniani. Na Argentina ni timu wenye ushawishi, wakiwa hawajafungwa katika mechi 35, wakiwa na kombora dhidi ya Denmark kwenye 16 bora, kasha England au Uholanzi. Nani anajua, huenda kipaji hiki kikatoa uamuzi wa mwisho.

Labda Messi kushinda Kombe la Dunia kunaweza kubadili kabisa suala hili, likitupa aina bora kabisa ya mchezo, hali bora ya kibinadamu, uzuri uonekanao hata kupitia kwenye kioo cheusi zaidi.

Messi anakaribia kuanza ushindani kwenye maonesho ya propaganda kubwa za Qatar. PSG wapo mbali nchini Ufaransa. Atafanya nini kule Qatar? Je, itakuwa uhatarishi dhidi ya Auxerre?

Pengine atacheza kidogo Jumapili. Na hakuna shaka kwaba hili ni jambo la moja kwa moja. Lakini, kwa sasa Messi yupo tayari kwa ajili ya kuingia kwenye fainali za Kombe la Dunia, bnaada ya kuwa hajacheza kwa siku 20, akiwa amecheza mechi saba tu tangu Desemba 1.

Harry Kane atakuwa amecheza 13 katika muda huo. Kila mmoja anamtaka Messi pale. Lakini, huu ni uhalisia? Ni kweli kwamba mchezo wa ushindani imara utafanyika pale?

Ikiwa ndivyo, basi upo uwezekano wa Messi kushinda kombe hilo, hebu chukua picha yake, kwa muda, akiwa pale jukwaani. Au fikiria picha ya mchezaji nyota wa timu yoyote inayopewa nafasi ya kushinda. Fikiria juu ya Neymar wa Brazil au Kylian Mbappé wa Ufaransa wakichukua kombe lile.

Huu ndio ule uzuri wa mipango na utekelezaji wa jambo la Qatar, na kiwango cha kujitolea. Qatar haina mtu mmoja tu ndani, bali watatu. Kwa namna moja au nyingine si ajabu kombe likanyanyuliwa na mwajiriwa wa nchi mwenyeji.

Ndiyo, unaweza pia kutumaini labda Denmark au England watashinda taji hilo. Ni ushindi wa Qatar, ulioandaliwa kwa miaka 12: Kombe la Dunia, ambalo sasa ni vigumu pia kudhani kwamba Messi anaweza kulishinda, au kuhisi kwamba maonesho haya yaliyoandaliwa mgongoni mwa rushwa ya Fifa kama kweli inastahili utimamu wa kimchezo.

Messi ni balozi wa utalii wa Saudi Arabia (je, kuna yeyote aliyemwambia Emir?). Kipaji chake ni cha thamani, aina ya uthibitisho. Kule Qatar Messi anaweza kujihisi

Messi huko Qatar bado anaweza kujihisi kama pumzi ya maisha ndani ya mashine. Inaweza pia kuhisiwa kama mapinduzi ya propaganda ya Kombe la Dunia yaliyojengwa vyema zaidi inayoweza kufikirika, mshirika wa kusafisha mchezo. Kilicho bora zaidi tunachoweza kutarajia ni fursa ya kujua kipi ni kipi.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

70 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

England

England 1990

Fainali za 1990 Italia