in , ,

Ambacho tunakikosa kipo Zanzibar

Mwisho wa kila safari huwa kuna funzo kubwa ndani yake, na binadamu
siku zote huimarika na kuwa bora kupitia mafunzo tunayoyapata katika
safari zetu kwenye maisha.

Safari ya michuano ya kombe la nchi wanachama wa Afrika Mashariki (
CECAFA) iliisha jana kwa kushuhudia Kenya ikichukua kombe lile.

Kenya kuchukua kombe lile haikuwa habari kubwa na ya kushangaza sana,
lakini Zanzibar kufika fainali ya michuano hiyo ilikuwa habari kubwa
na ya kushangaza.

Timu ambayo ilikuwa imesubiri miaka 22 kufika fainali ya michuano hii,
ambapo mara ya mwisho kufika ilikuwa mwaka 1995.

Muda mrefu ulikuwa umepita huku Zanzibar akisubiri kwa hamu siku hii,
kukaa kwake muda mrefu bila kufika fainali ya kombe hili ndiko
kuliwapa watu moja ya sababu ya Zanzibar kutokufanya vizuri.

Kikosi cha Zanzibar hakikuwa kimesheheni nyota wengi wa majina ya
kutisha ambayo yangetumika kuogofya timu zingine.

Lakini walikuja na wachezaji wenye majina ya kawaida, hali ambayo
iliwafanya wapinzani wao kuiona Zanzibar kama timu ya kawaida.

Wakaiweka kwenye ukawaida, hawakuipa nafasi kubwa ,wakaipa nafasi ya kawaida.

Zanzibar ikakubali kuwa timu ya kawaida ikaingia na faida ya kuitwa
timu ya kawaida.

Faida hii iliwanufaisha sana wao kwani timu nyingi ziliingia zikiamini
Zanzibar ni underdog, hivo timu zikiingia zikiwa zimejiamini sana
mbele ya Zanzibar.

Zanzibar iliingia kawaida, ikiwa haijiamini sana kama timu zingine,
hali ambayo iliifanya icheze mpira ikiwa katika hali ya utulivu, hali
ambayo iliifanya wafanye maamuzi mazuri ambayo yalikuwa na manufaa
kwao.

Utulivu wao uliwafanya wacheze bila presha na kutumia vizuri nafasi
ambazo walikuwa wamezitengeneza.

Mfano katika mechi ya fainali, walitanguliwa na wenyeji Kenya mara
mbili, lakini hawakuonekana kuwa na presha, ila walitulia na
kutengeneza nafasi ambazo ziliwasaidia kusawazisha magoli yale.

Moja ya timu ambazo zilikuwa zinapewa posho ndogo, Zanzibar ilikuwa moja wapo.

Lakini kwao posho kubwa lilikuwa siyo jambo la mbele, kitu ambacho
ƙkilikuwa mbele zaidi kwao ni maslahi ya Taifa lao.

Nchi yao ilikuwa kila kitu kwao kuliko kitu kingine, waliamua
kuipigania nchi yao katika ardhi ya ugenini.

Manung’uniko ya posho ndogo kwao hayakuwepo, kitu pekee kilichokuwepo
katika kichwa chao ni wao kujitengeneza wawe mashujaa wa nchi yao.

Mashujaa ambao wataimbwa, watasomwa kwenye vitabu vya mashujaa, ndiyo
maana walipigana kwa nguvu na kwa pamoja bila kuchoka kuhakikisha nchi
yao ikipata ushindi.

Walipigana katika mazingira magumu kuhakikisha wanaipata furaha, jasho
lao lilikuwa muhimu kwa nchi yao kuliko kitu chochote.

Waliamua kuitumikia nchi yao na kuachana na dhana ya kuitumikia pesa,
uzalendo ulikuwepo ndani yao.

Hii imekuwa tofauti sana katika kikosi cha timu yetu ya Taifa, timu ya
taifa wachezaji wake hawachezi kwa uzalendo licha ya kupewa posho
vizuri kama motisha lakini uzalendo ndani yao wanakosa.

Hata kipindi ambapo huwa wanakuwa “underdogs” huwa wanatoka mchezoni
kwa kukubali kufungwa kabla hata mechi haijaanza.

Lakini Zanzibar imetupa somo ambalo tunatakiwa kulichukua na kutembea
nalo kwa ajili ya manufaa ya mpira wetu .

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

MBIO ZA UBINGWA ZIMEFIKIA UKINGONI ?

Tanzania Sports

ARSENE WENGER ATAENDELEA KUWA MNYONGE KWA JURGEN KLOPP?