in , ,

ALEX IWOBI , NIGERIA ITAKUKUMBUKA KWENYE VITABU VYAKE

Dunia ni kwa ajili ya mashujaa, na mashujaa huzaliwa kila siku . Kila
mtu ni shujaa kwenye nafasi yake.

Hakuna asiye shujaa kwa sababu dunia huzalisha mashujaa kila jua linapochomoza.

Kitu kinachotokea ni kidogo tu, juhudi za kupigania ushujaa wako
uonekane ndani ya jamii

Ushujaa hauji tu kwa wewe kukaa ndani bali ushujaa unakuja kwa wewe
kwenda kwenye uwanja wa vita na kuonesha nguvu ya ushujaa wako
hadharani

Mara nyingi mashujaa hukumbukwa sana, historia yao ni vigumu sana
kuifuta hata siku moja.

Maana hufanya vitu ambavyo huleta heshima kwa taifa. Hakuna heshima
kubwa katika soka kama kushiriki michuano mikubwa kama ya kombe la
dunia.

Michuano ambayo kila jicho hutazama tena kwa hisia za ndani kwa sababu
nyota wengi wa mpira wa miguu hukusanyika kwa pamoja .

Ni fahari kubwa sana kuiona timu yako ya taifa ikiwa uwanjani
inapambana na kuwawakilisha wananchi wa Taifa husika.

Ni fahari kuona bendera ya taifa ya nchi yako, wimbo wa taifa wa nchi
yako ukipigwa mbele ya dunia nzima.

Hii ndiyo huwa ni vita ya dunia, vita ya mpira ya dunia. Vita ya amani
ambayo kila mpendasoka hutamani kuiona nchi yake ikiwa kwenye uwanja
huo wa vita ya kisoka ikipambana kwa hali na mali.

Mataifa mengi hukumbuka sana hizi kumbukumbu kwa furaha, ndiyo maaa
huwa wanawakumbuka kwa kiasi kikubwa watu ambao huwafanya waweze
kuwapeleka huko.

Jana Alex Iwobi alifunga goli pekee ambalo liliifanya nchi ya Nigeria
kuwa nchi ya kwanza ya Afrika kufuzu kombe la dunia nchini Russia.

Ni furaha kubwa kwa wa Naigeria , furaha hii imechagizwa kwa kiasi
kikubwa na ubora wa kikosi chao lakini aliyekuja kuhitimisha furaha
yao ni Alex Iwobi kwa kufunga goli lililowapeleka Naigeria nchini
Russia.

Goli ambalo halitofutika kwenye kumbukumbu za soka la nchi ya Nigeria.
Kila kizazi kitakachokuja kitakuta maandishi yanayoelezea kuwa mwaka
2017 mwezi wa 10 tarehe 7 Alex Iwobi alifunga goli lililopelekea timu
ya taifa kufuzu kombe la dunia nchini Russia zitakazofanyika 2018.

Heshima kama hii kila mchezaji hutamani kuipata, na haiwezi ikaja kwa
kila mchezaji ila juhudi ya mchezaji husika ndiyo humfanya aweze
kupata heshima hii kubwa.

Na hapa ndipo kuna somo kubwa sana kwa wachezaji wetu hapa nchini.
Wanatakiwa wapigane ili wajenge historia yao ndani ya mpira wa
Tanzania na dunia kwa ujumla.

Wanatakiwa watafute sababu ya kwanini dunia iwakumbuke? Mpira
utawakumbuka kwa lipi?

Kipi ni wanatakiwa kukifanya ili wakumbukwe na ramani ya mpira.

Jitihada zao binafsi ndicho kitu ambacho kinaweza kuwafanya kukumbukwa.

Bila kuweka juhudi ndani yao ni ngumu kwao kukumbukwa kwa lolote lile.
————————————————————————–
NCHI ZILIZOFUZU KOMBE LA DUNIA NCHINI RUSSIA MPAKA SASA

UEFA (EUROPE)

Russia (MWENYEJI), Belgium, Germany, England, Spain.

CAF (AFRICA)

Nigeria

AFC (ASIA)

Iran, South Korea, Japan, Saudi Arabia

CONCACAF (NORTH AMERICA)

Mexico

CONMEBOL (SOUTH AMERICA)

Brazil

OFC (OCEANIA)

Hakuna iliyofuzu bado

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Issues with Tanzanian football: Interview with Paul Mitchell, Siyavuma Sports Group

Tanzania Sports

HISTORIA ITAMKUZA SALAH JUU YA KINA ABOUTRIKA