Klabu ya Zamalek wametangazwa kuwa mabingwa wapya wa Misri na wameshangilia kwa nguvu taji hilo walilolisaka kwa zaidi ya muongo mmoja.

Zamalek walishinda 3-2 walipocheza na Al Geish katika mechi ambayo washabiki hawakuruhusiwa. Ilikuwa msisimko wa aina yake kwani mahasimu wao wakubwa, Al Ahly walikuwa wakitarajia kutwaa tena ubingwa huo.

Al Ahly ambao wametawala sana kutwaa ubingwa wa Misri walibanwa na Smouha kwa kwenda sare ya 1-1, hivyo kuwakosesha sifa ya kuweza kuwafikia Zamalek waliocheza kwenye Uwanja wa Jeshi jijini Cairo.

Wakiwa wamebakiza mechi moja, Zamalek wamefikisha pointi 86, nane zaidi ya Ahly. Zamalek wamepata kuwa mabingwa wa Afrika mara tano na dhihirisho la ubingwa wao lilitokana bao la Mohamed Hashem la kujifunga mwenyewe kisha lile la mkongwe Ahmed Eid.

Hashem alisahihisha makosa yake ya awali kwa kufunga bao kabla ya Bassem Morsy kuongeza jingine kwa Zamalek, likiwa ni bao lake la 18 msimu huu.

Islam Kamal alichomoa moja dakika za mwisho lakini halikuwazuia Zamalek kutwaa ubingwa wa Misri. Ni miaka 11 imepita tangu Zamalek wapate ubingwa, na katika wakati huo Ahly wameutwaa mara nane na misimu mingine miwili hapakuwapo ligi kutokana na machafuko.

Msimu huu pia ulitawaliwa na vurugu kiasi. Misri ilikuwa katika wakati mgumu hasa kipindi cha mpito baada ya vuguvugu la mapinduzi lililomwondosha madarakani Rais Hosni Mubarak, uchaguzi ukafanyika akachukua Mohamed Morsi kisha akaondoshwa na sasa anao Jenerali Abdel Fatah el-Sisi.

Washabiki wa Zamalek walikanyagana wakilazimisha kuingia uwanjani wakati walikuwa wamezuiwa Februari mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 22. Ligi hiyo ilisitishwa kwa mwezi mmoja kabla ya serikali kuruhusu kuanza tena, lakini bila washabiki kuingia uwanjani.

Kocha wa zamani wa Porto, Jesualdo Ferreira ndiye aliyewaongoza Zamalek kwenye ubingwa, akiwa ni wa nne kwa msimu huu. Hata hivyo, wiki iliyopita walifungwa na Ahly 2-0 na hadi sasa wana rekodi ya kutoshinda kwenye ‘derby’ ya Cairo kwa mechi 20.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Stopilla Sunzu aenda Lille

FAINALI KAGAME: HISTORIA ITAJENGWA