in

Yanga wampe muda Michael Sarpong

michael sarpong

Kuna baadhi ya wachezaji ambao wamewahi kucheza kwenye ligi kuu ya Tanzania bara lakini hawakufikia mafanikio makubwa kutokana na presha kubwa nje ya uwanja.

Mara nyingi waliacha kufikia hatua ya mafanikio siyo kwa sababu hawakuwa na viwango vikubwa. La hasha! Presha kubwa ya mashabiki nje ya uwanja iliwalazimu kuondoka kwenye ligi yetu bila kufikia mafanikio makubwa.

Mashabiki hutamani kitu kikubwa kutoka kwa wachezaji hao bila hata kuwapa muda wachezaji husika. Simba iliwahi kuwa na mshambuliaji mzuri kutoka Burundi, Laurent Mavugo.

Kabla ya kuja Simba alikuwa mfungaji bora katika ligi kuu ya Burundi mara tatu mfululizo. Hili halikuwa jambo la kawaida kabisa, mshambuliaji kuwa mfungaji bora kwenye ligi kuu tena mara tatu mfululizo.

Baada ya kufika Tanzania alikutana na mazingira tofauti na mazingira ya Burundi. Aina ya mpira wa Tanzania ni tofauti na wa Burundi. Ushindani wa ligi ya Tanzania ulikuwa mkubwa ukilinganisha na ushindani wa ligi ya Burundi.

Laurent Mavugo alikutana na kikosi kipya, kikosi ambacho alitakiwa kuzoeana nacho vizuri ili kuonesha uwezo wake mkubwa wa kufumania nyavu. Alikutana na falsafa mpya kabisa ambayo alitakiwa kuizoea ili kuonesha kiwango chake kikubwa.

Laurent Mavugo alihitaji muda ili kuwapa furaha mashabiki wa Simba lakini cha kusikitisha mashabiki wa Simba hawakutaka kumpa muda Laurent Mavugo.

Kitu pekee ambacho mashabiki wa Simba walichokuwa wanakitaka ni magoli tu. Presha ilikuwa kubwa kwa Laurent Mavugo. Muda ambao anatakiwa kujitafuta yeye binafsi ndiyo muda ambao mashabiki wa walitaka magoli.

Presha kubwa ilimuondoa Laurent Mavugo Simba. Hakupewa utulivu kabisa ndani ya Simba mwisho wa siku akaondoka Simba na Simba wakawa wamepoteza mchezaji mzuri kwa sababu ya kumpa presha kubwa.

Unamkumbuka kiungo wa Simba kutoka Sudan, Ally Shiboub? Moja ya viungo bora kabisa kuwahi kucheza kwenye ligi yetu. Huyu naye aliondoka Simba kwa sababu ya presha kubwa ya nje ya uwanja.

Nje ya uwanja kulikuwa na mahitaji makubwa ambayo walikuwa wanayataka kutoka kwa Shiboub . Walitaka magoli , wakataka pasi za mwisho za magoli, wakata unabaki mzuri lakini wakasahau kumpa muda Shiboub.

Shiboub aliondoka Simba kwa sababu ya presha kubwa kutoka kwa mashabiki wa Simba, kwa mara nyingine Simba walipoteza kiungo bora kwa sababu ya kumpa presha kubwa.

Presha hii imerudi tena kwa Yanga. Yanga wana mshambuliaji ambaye anapewa presha kubwa sana. Yanga kwa sasa wanahitaji kuona washambuliaji wao wafunge magoli mengi.

Wameweka presha kubwa kwa washambuliaji wao. Presha ambayo inaondoa utulivu kwa wachezaji wa Yanga hasa washambuliaji wa Yanga.

Michael Sarpong ni moja ya washambuliaji wazuri lakini kwa sasa anakosa utulivu na anaondokewa na kutokujiamini kwa sababu ya presha kubwa anayopata kutoka kwa mashabiki wa Yanga.

Kilichowatokea Simba kwa kupoteza wachezaji wazuri kwa sababu ya kuwapa presha kubwa baadhi ya wachezaji bora. Michael Sarpong anatakiwa kupewa muda na siyo kupewa presha kubwa.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Yanga na Simba Uwanjani

Yanga wanatakiwa kuionea wivu Simba!

Taifa Stars

Taifa Stars, bila Jonas Mkude..