in , ,

YANGA WAMETUPA TULICHOKUWA TUNAKITAKA

Sehemu ya wachezaji wa Yanga

Yanga waliingia na mfumo wa 4-4-2 Diamond wakati Wallayta Dicha
walikuwa wanacheza mfumo wa 4-4-2

Lakini pamoja na kwamba Yanga kwenye karatasi ilionekana wanacheza
4-4-2 Diamond, uwanjani walionekana kucheza bila mshambuliaji halisi
wa katikati, ambapo Raphael Daud alikuwa anacheza kama false 9

Kitu ambacho kilikuwa kinamsaidia kushuka chini katikati kuchukua
mipira hali ambayo ilikuwa inawalazimu mabeki wa Wallayta Dicha
kupanda juu yao na kuacha uwazi kule nyuma, uwazi ambao ulikuwa
unatumiwa na kina Yusuph Mhilu pamoja na Emmanuel Martin , wakati
mwingine Ibrahim Ajib.

Hiki ndicho kilikuwa msaada mkubwa wa Yanga katika eneo la Mbele,
ambapo iliruhusu wachezaji wengi wa Yanga kuwa katika eneo la box
kipindi walipokuwa wanashambulia.

Walipokuwa wanashambuliwa Yanga, wachezaji wawili walikuwa wanakuja
katikati kuungana na Kamusoko na Pius Buswita katika eneo la katikati,
ambapo Emmanuel Martin na Ibrahim Ajib ndiyo walikuwa wanaongeza idadi
ya watu eneo la katikati , hivo Yanga ikawa inakuwa na watu wanne
dhidi ya wawili wa Wallayta Dicha.

Hali hii ilikuwa ngumu sana kwa Wallyta Dicha kwa sababu walipokuwa
wanajaribu kwenda mbele kuanzia katika eneo la katikati Yanga
waliwapokonya mipira na kuanza kushambulia kwa kasi kuanzia eneo la
katikati.

Kitu ambacho kilikuwa kinawagharimu Yanga walipokuwa wanaanza
kushambulia ni Ibrahim Ajib kupoteza mipira mingi sana.

Upi ulikuwa ubora wa Wallyta Dicha katika mechi ya leo?

Kumiliki kwao mpira kulikuwa na msaada kwao kwa sababu waliwezesha
kupunguza kasi ya Yanga

Lakini walipokuwa wanamiliki mpira walikuwa wanamiliki mpira bila
tahadhari na wao kutengeneza uwazi sehemu mbalimbali ndani ya uwanja.

Uwazi huu ulikuwa unatumiwa na wachezaji wa Yanga, mfano magoli yote
mawili ya Yanga yamefungwa wakati ambao wafungaji wa Yanga walipokuwa
katika eneo ambalo kulikuwa na uwazi hivo kuwa na uhuru zaidi wa
kupiga kichwa.

Pili, magoli yote ya Yanga yamefungwa kutokana na mipira ya krosi
(mipira ya juu) hii inaonesha kabisa udhaifu mkubwa wa Wallayta Dicha
wakati wanajizuia ni mipira ya juu

Upi ulikuwa ubora wa Yanga?

Nidhamu yao ya kujilinda ilikuwa silaha kubwa kwao, utulivu ilikuwa
mkubwa kuanzia kwa golikipa mpaka kwa viungo wa kati.

Kuanzia katikati mpaka nyuma Yanga walikuwa wanajilinda vizuri
hawakuruhusu presha kubwa ndani yao hali ambayo iliifanya timu iwepo
ndani ya mchezo kwa muda mrefu.

Tatizo kubwa ambalo walikuwa nao Yanga ni nidhamu ya matumizi ya
nafasi walizokuwa wanazipata ambapo Yusuph Mhilu pamoja na kucheza
vizuri leo lakini yeye pamoja na Ibrahim Ajib walikosa nafasi nyingi
ambazo zingeiwezesha Yanga kuwa na mtaji mkubwa kwao.

Hitimisho: Tangu msimu huu uanze Yanga haijawahi kufungwa magoli
kuanzia 3-0 katika mechi moja, ushindi wao wa magoli 2-0 utawalazimu
Wallayta Dicha kushinda magoli 3-0 dhidi ya Yanga ili wapite katika
hatua ya makundi kitu ambacho Yanga hawajawahi kuruhusu msimu huu,
hivo kwa 75% Yanga watakuwa wana nafasi kubwa ya kufuzu kwenda katika
hatua ya makundi.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

TUNA DUNIA YA RONALDO NA DUNIA YA MESSI

Tanzania Sports

YANGA INAWAZA VIZURI , INATEKELEZA KAWAIDA