in , , ,

Yanga wameloweshwa nyumbani, kung’ara ugenini?


Mchezo huo ulichezwa huku jiji la Dar es salaam likiwa limeshuhudia mvua kali

UTELEZI, unyevu, ubaridi, maji na hali ya hewa ya jiji la Dar Es Salaam vilikuwa sehemu ya vitu ambavyo vilitawala katika fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF Confederation Cup) iliyochezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam huku wenyeji wakikubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Union Sportive Medina (USM Alger) ya Algeria. Katika mchezo huo uliochezwa kwa presha kubwa huku uwanja huo ukitapika mashabiki wengi ambao waliruhusiwa kuingia bure kushuhudia fainali hiyo. Hii inakuwa fainali ya pili kwa ngazi ya vilabu kwenye mashindano ya Shirikisho la Soka barani Afrika, ambapo mwaka 1993 mabingwa wa zamani Simba walimenyana na Stella Abdijan ya Ivory Coast kwenye mashindano ya Kombe la CAF. 

Dakika za ‘joto kali’ katikati ya mvua

Kwa muda wa dakika 15 za kwanza timu zote mbili zilikuwa zinatafuta bao la kuongoza. USM Alger walitumia zaidi mashambulizi ya pembeni kuwasumbua walinzi wa Yanga, Kibwana Shomari aliyekuwa akicheza beki wa kushoto na Dickson Job aliyekuwa akicheza beki wa kulia. Hekaheka za mchezo huo ziliwapa nafasi wachezaji wote kucheza kwa uangalifu na kwa ujumla zilikuwa dakika za kuogopana baina ya miamba hiyo. Kwa kawaida hizo ni dakika ambazo kila timu zinakuwa na mkakati maalumu wa kuibuka na bao la kuongoza hali ambayo ilisababisha mchezo huo kuwa na ufundi mwingi. Mchezo huo ulichezwa huku jiji la Dar es salaam likiwa limeshuhudia mvua kali. 

Ukuta mgumu, ufundi mwingi

Kwa kipindi cha dakika 30 timu zote ziliweka walinzi watano katika eneo la ulinzi. Licha ya mashabiki kushuhudia mabao 3 katika fainali hiyo, lakini timu zote zimekuwa makini katika eneo la ulinzi, huku makipa wote Benhot wa USM Alger na Djigui wa Yanga wakiokoa hatari mbalimbali langoni mwao. Ulinzi ulikuwa mkakati wa kwanza ambao timu zote zilikuwa zinaacha wachezaji watano katika eneo la ulinzi. Yanga walikuwa na mabaeki watano (ukiongeza kiungo mkabaji) wakati wa kujilinda, lakini walikuwa wanashambulia. 

Kiufundi Yanga,USM Alger

Kwa upande wa Yanga, mashambulizi yao hupangwa kuanzia kwa mabeki wa kati, ambapo viungo wawili Yannick Bangala na Mudathir Yahya hurudi kuchukua mipira hiyo na kuelekea lango la adui au kutafuta namna ya kumfikishia Stephanie Aziz Ki. Hata hivyo USM Alger walikuwa wamemkabidhi Chita kazi ya kumdhibiti Aziz Ki hali iliyosababisha apoteze mipira mingi. 

Kila alipokuwa anapokea pasi alijikuta amezungukwa na Chita pamoja na Belhaid waliokuwa wanasafisha hatari zote eneo la kiungo wa kati. USM Alger walionekana kuwa wazuri zaidi kwenye mipira mirefu (Long passes) na walitengeza mazingira ya kupata faulo (set pieces) ambazo zilitumiwa vizuri ilikiwemo bao la kuongoza. Mkakati wa USM Alger ulikuwa kudhibiti wapishi wa Fiston Mayele ambao ni Aziz Ki, Mushonda na Mudathir. Upande wa winga wa kulia, Kisinda Tuisila hakuwa na siku nzuri kazini, lakini hakuwa mbaya katika mchezo. 

Kipindi cha pili USM Alger walibadili mbinu kwa kuzuia kuanzia eneo la hatari la Yanga ili kuwanyima nafasi mabeki wa kati kuandaa mashambulizi. Kocha Nabi alililiona hilo, ndipo akafanya mabadiliko ya kuwatoa Dickson Job na Kibwana Shomari ambao ni walinzi wa pembeni katika mkakati w akujilinda na kuwaingia mabeki Djuma Shaban na Lomalisa Mukandala ambao ni mabeki wanaopendelea kushambulia zaidi. kiufundi Nabi alitaka kuwarudisha nyuma USM Alger, ambao nao walibadilika kwa kupiga mipira mirefu zaidi.

Tanzania Sports

Siri ya USM Alger

Bao la kwanza lililofungwa na mshambuliaji wa USM Alger AAimen Mahious katika dakika ya 32 lilitokana na mpira wa faulo. Timu hii inaonekana kujipanga kutumia vizuri faulo na imefanyia kazi kubwa dhidi ya Yanga. Lakini pia siri yao ni kuwa watulivu sana, wachezaji wao hawana papara, wameisoma Yanga na kuwadhibiti watu muhimu kama Fiston Mayele. Bao la pili lilifungwa na Islam Merili katika dakika 84 lilionesha namna timu yao ilivyojipanga kwa utulivu. Ni dhahiri kocha Nabi na Cedric Kaze wanatakiwa kukiangalia mara nyingi zaidi na kuwasisitizia mabeki na viungo wake kuwa watulivu. USM Alger ni wazuri katika umaliziaji (final third) ambapo walifunga bao la pili kwa mkakati wa utulivu ambao ulionesha kutokuwa na papara na wazi walijipanga kwa kuisoma safu ya ulizi ya Yanga.

Presha kubwa makocha

Wao ndiyo walikuwa wenyeji wa mchezo huu wa kwanza. Makocha walikuwa na kila sababu ya kuwa na presha kubwa ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hiyo kufika fainali ya mashindano yanayosimamiwa na CAF. Kocha wa Yanga Nasredine Nabi hakutulia, alisimama mara kwa mara kuwaelekeza wachezaji wake. Kuna wakati alialaizmika kushikilia bega la msaidizi wake Cedric Kaze kudhihirisha fainali hiyo kuwa kubwa na yenye presha.

Miguu yao Afrika kusini

Yanga na USM Alger zote kwa pamoja zimefika fainali huku zikiwa zimekutana na timu za Afrika kusini. Yanga walipepetana na Marumo Gallants wakati USM Alger wao walichuana na Cape Tpown City FC. Timu hizo zimefika fainali kupitia Afrika kusini, ikiwa ni sehemu mojawapo waliyovuja jasho katika safari ya kulitafuta kombe la Shirikisho. Yanga waliwafunga Marumo Gallants katika mechi zote mbili (2-0 na 1-2), wakati USM Alger walilazimisha suluhu (0-0) na kuibuka na ushindi 1-0 katika uwanja wao wa nyumbani.

Mfugaji bora wa mashindano

Hadi mchezo wa kwanza fainali hiyo ulipomalizika, mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele ameongeza idadi ya mabao kwa kupachika bao lake la 7. Hilo lina maana kuwa Yanga watakuwa na uhakika wa kunyakua kiatu cha dhahabu kupitia nyota wao huyo.

Yanga kushinda ugenini?

Hili ndilo swali ambalo wanajiuliza mashabiki wengi. Kucheza ugenini na kuibuka washindi katika fainali ya pili ni jambo ambalo makocha wanatakiwa kulipangia mkakati. Takwimu zinaonesha hakuna timu iliyocheza na USM Alger ikashinda kwenye uwanja wao. Timu zote zilizokaribishwa kwenye uwanja wa USM Alger zilifungwa. Hata hivyo ukitazama namna Cape Town City walivyofungwa kwa tabu yaani 1-0 ni dhahiri Yanga wanaweza kuikabili timu hiyo. Yanga wameshinda mechi kadhaa za ugenini katika mashindano haya. 

Waliwashinda Marumo Gallants (Afrika kusini), Rivers United(Nigeria), TP Mazembe(DRC), Club Afrain (Tunisia). Hata hivyo benchi la ufundi litakuwa na kibarua kuamua ni kikosi gani kianze Juni 3 mwaka huu katika mchezo wa pili wa fainali. Mkakati wa kwanza waweza kuwatumia Jesus Moloko na Tuisila Kisinda au Bernard Morrison na Farid katika safu ya mawinga. Mkakati wa pili ni kuwatumia mabeki Dickson Job na Shomari 

Kibwana tena au kuanza na Djuma Shaban na Lomalisa Mukandala katika safu ya ulinzi. Mkakati wa tatu ni kuwatumia Fiston Mayele Musonda kikosi cha kwanza au kuipangua na kuwaongeza Clement Mzize na Aziz Ki. Shughuli nyingine itakuwa safu ya kiungo kati ya Mudathir Yahya, Yannick Bangala na Zawadi Mauya. Kwa vyovyote ulinzi ni muhimu, lakini USM Alger wanafahamu mkakati wa Yanga utakuwa ni kushambulia kuanzia mwanzo. Ni uamuzi wa benchi la ufundi kuchagua mfumo sahihi wa kuwakabili wapinzani wao.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Mikel Arteta, na Arsenal watembee kifua mbele

Tanzania Sports

Unai Emery wa Aston Villa apewe maua yake