in

Yanga Walimnyatia Senzo Kitambo

Senzo

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga SC Simon Patrick  ameweka wazi juu ya mfumo wa timu ya Yanga kuelekea katika mabadiliko ya timu yao.

Kwa mipango ambayo ameieleza Simon Patrick ambapo nimeweka chini ya makala hii utajua kabisa kuwa Senzo alikuwa katika mipango ya Yanga.

Hii inamaanisha kuwa Yanga katika mipango yao walimtaka mtu kama Senzo ili kuelekea katika mabadiliko yaliyo mema na bahati nzuri wamempata.

Patrick amesema kuwa katika sehemu ya kwanza wataimarisha sehemu ya uongozi ili ikae sawa na ndio maana tunaona mabadiliko ya viongozi mfano Senzo Mazingiza amejiunga na timu yao akitokea Simba.

Bado kama haitoshi wamewaongeza watu wenye weledi pia kutoka ligi kuu ya Hispaniakatika timu ya Sevilla.

Ili kuendelea kuijenga timu ya Yanga wanatakiwa wawe wapole na wasiende kwa pupa itawasaidia sana kuelekea katika mabadiliko ya kweli.

Maelezo ya Kaimu katibu mkuu ya Yanga Simon Patrick  mbayo ameyatoa ni kama ifuatavyo hapo chini.

‘’Katika mabadiliko ya kweli tunayoyataka wana Yanga, kama tulivosema hapo awali, tutaanza na mambo makuu matatu;

‘Proper Management’:-  Kwenye ‘phase’ ya kwanza ya mabadiliko ya kimfumo, Klabu yetu itapendekeza kwa wanachama mfumo wa kisasa wa Uongozi kwenye vilabu (Modern Organizational Structure) na kuruhusu uwekezaji huku Klabu ikibaki ni mali ya wanachama kwa asilimia zaidi ya hamsini.

Katika mfumo huu, muwekezaji atanunua hisa kwanza ndipo atapata uhalali wa kua mwanahisa “shareholder” na sio kwa ahadi.

‘Proper Technical Department’-  Tutatengeneza bench la ufundi lililo bora kuweza kuzisaidia timu zetu nje na ndani ya uwanja kwa weredi mkubwa sana na wa kisasa.

‘Top Class Players’-  Tutajenga timu yenye ushindani mkubwa sana na nidhamu ya hali ya juu, na usajili utafanywa kwa weledi mkubwa sana bila ujanja ujanja, mihemko huku tukizingatia kanuni za usajili.

Utekelezaji wa haya yote ndio kiashiria halisi cha mabadiliko “Transformation”. Wananchi wenzangu naomba mnielewe ninavyowaambia msikubali kuyumbishwa, kuna watu hawafurahii mabadiliko haya, yanawaogopesha sana watu ndio maana wanajaribu kutuvuruga lakini hawataweza.

Klabu ya Yanga inaenda kuweka historia ya kuwa Klabu ya kwanza kufanya ‘real transformation’ Tanzania katika vile vilabu vinavyomilikiwa na wananchi, hili ni la kujivunia, na tulilinde kwa nguvu zetu zote.

Hayo juu ndio maelezo mahususi ya Patrick Simon  Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga.

Tanzania Sports
usajili ukiendelea

Yanga ambayo inaendelea na michakato hiyo ili kuanza kuonesha mfano siku ya jumatatu wamemuongezea mkataba wa miaka minne kiungo nyota Feisal Salum ‘Fei Toto’ huku katika kipengele kimoja wapo kitampelekea La Liga kwenda kupata ujuzi zaidi.

Huu ni mfano mzuri kabisa na ni Yanga hao walioanzia mambo haya kwa soka la Tanzania.

Tukumbuke kuwa waliwahi kumsaini Ramadhani Kabwili kwa mkataba mrefu na sasa Feisal.

Lakini pia hayo mengine yote wanayoyasema basi inatakiwa yaonekane na yatendeke.

Kuelekea katika mafanikio Yanga wanatakiwa wafahamu kuwa kuna vikwazo vingi sana ndani yake hivyo watulie na watengeneze mfumo uliokuwa makini.

Michael Wambura aliwahi kusema kuwa sio haki itendeke ila ionekane kutendeka. Nami nawaambia kuwa sio maneno tu bali vitendo vionekane kutendeka.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Usajili wa Yanga

Yanga yanasa mmoja, Morrison bado..

Tanzania Sports

Yanga na Ajib wanahitajiana..