in , ,

Yanga: Tunakata rufaa FIFA

*OKWI,OKWI,OKWI….

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema utapinga maamuzi ya kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji kuhusiana na maamuzi yake ya kumtangaza mchezaji wake, Emmanuel Okwi kuwa huru.

Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ya Yanga, Sam Mapande amesema kuwa hawajaridhishwa na maamuzi hayo ambayo yanakinzana na sataka zima la mchezaji huyo.

Mapande alisema kuwa kamati ya TFF imeamua sakata la Okwi kinyume na malalamiko yao kwani hakukuwa na lalamiko la mchezaji huyo wa Uganda kuhusiana na malipo ya fedha zake za usajili.

Alisema kuwa cha kushangaza, kamati hiyo ya TFF iliamua kusikiliza kesi ambayo haikuwa mbele yao na kutoa maamuzi ambayo hata wao wameshangazwa nayo.
okwiiiii

“Kwanza kesi yenyewe ilikuwa haijamalizika, walituambia tuwasilishe vielelezo kuhusiana na kitendo cha mchezaji huyo kufanya mazungumzo na klabu ya Misri, lakini cha kushangaza maamuzi yametolewa, hili limetushangaza sana,” alisema Mapande.

Alisema kuwa mazingira yalikuwa yameandaliwa kuibeba Simba na Okwi kwani hata malalamiko yao kwa Simba hayakusikilizwa. “Malalamiko yetu yalikuwa wazi kabisa, yapo kimaandishi, hatukuwai kulalamikiwa, suala la fedha za usajili la Okwi limetoka wapi, kama lilikuwepo, mbona hatujajulishwa kimaandishi kama utaratibu ulivyo,” alisema.

Alisema kuwa Kamati hiyo kumruhusu mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Zacharia Hans Pope ambaye pia ni mwenyekiti wakamati ya usajili ya Simba kuwemo katika kikao hicho kinyume na taratibu za Fifa kupitia kifungu namba 19 kinachoeleza mgongano wa kimaslahi.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Ujerumani wawazidi Scotland

Welbeck awabeba England