in

Yanga Inafaidika Na Wachezaji Wa Simba

Yanga na Simba wamekuwa wakichukuliana wachezaji kwa mbinde sana, baada ya hapo wengi wakitarajia kuona vitu vizuri kutoka kwa wachezahi hao.

Wakati wanatoka katika timu zao husika wanakuwa wa moto sana lakini wakifika eneo lao jipya la kufanyia kazi matokeo yanakuwa hafifu sana yaani ‘Work done is equal to zero’.

Yanga imekuwa inafaidika zaidi na wachezaji wanaotoka  Simba kuliko wale wanaotoka Yanga kwenda Simba, na ushahidi upo tangu zamani hadi miaka ya hivi karibuni.

Mfano mzuri tuangalie hawa wanaocheza hivi sasa kisha tutawataja wengine japo kwa ufupi ili tupate mantiki kamili ya tunayoyasema.

Hapa tuaanza waliotoka mabingwa wa nchi Simba kuelekea kwa mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga.

Gadiel Michael

Huyu mtu amecheza timu tatu kubwa hapa Tanzania ameanzia Azam FC, Yanga na sasa Simba safari yake imekuwa ngumu alipotua Simba kutokana na kukosa nafasi ya kudumu katika timu hiyo.

Alikuwa mchezaji tegemeo wakati yupo Yanga aliitwa timu ya taifa na alikuwa katika orodha ya wachezaji 11 wa kikosi cha kwanza, hii ilitokana na kiwango chake kuwa bora mashavu yalijaa na kuwekwa katika vitabu vya historia.

Hebu angalia kwa sasa mashavu aliyokuwa nayo Yanga hadi timu ya taifa yapo tena ?  Lakini angalia kile kiwango kikubwa alichokionesha Yanga bado kipo.

Huu ni mfano wa kwanza baadhi ya wachezaji wa Yanga kwenda Simba na inaoneka imefeli wengine wanamshauri atafute chaka la kufanya kazi yake kwa ufasaha ili arudi kileleni kama zamani.

Inaonekana hawezi kuichukua namba kwa Mohamed Hussein labda awe majeruhi au wanatiana mismumari hawa( Jokes).

Beno Kakolanya

Goli kipa mahiri kabisa Tanzania, umaarufu ameupata katika mechi ya Simba dhidi ya Yanga, naye aliwahi kucheza timu ya taifa.

Anayemnyima usingizi Aishi Manula ambaye amejiimarisha kupita maelezo sasa ufanisi wake umekuwa butu, akigombana na Yanga kutokana na kukosa fedha ila sasa anapata kila kitu ila uwanjani ndio basi tena.

Mrisho Ngassa 

Huyu kada namba moja wa Yanga, anaipenda sana timu hiyo lakini alibadili upepo akajiunga na Azam ila alienda Simba kwa mkopo hakuonesha yale yaliyokuwa Yanga.

Baadae akarudi na akafanya vizuri katika timu yake pendwa hadi walipoamua kuachana naye msimu huu.

Ibrahim Ajibu

Ajibu tutamuelezea mara mbili kutokana na kile alichokifanya kizuri akiwa Yanga.

Ajibu alikuwa katika timu ya Simba baadae Yanga wakamchukua alikiwasha sana.

Msimu wa mwisho kucheza Yanga alifunga magoli 8 na kutoa nafasi 8 za magoli wakati huo alikuwepo mshambuliaji Heritier Makambo.

Tanzania Sports
mahasimu..

Ajibu hadi jina wakambatiza na kumuita ‘Ibrakadabra’ wakimfananisha na Ibrahimovic kwa jina ila uwezo wake pia.

Nyota yake ilififia na sasa anapata nafasi katika kikosi cha pili tena michezo ya kirafiki, sio kwamba hawezi mpira ila waliopo huenda mafundi zaidi yake, inawezekana pia uchaguzi wake wa kurudi katika timu yake anayoipenda ya Simba.

Naye afanye uchaguzi mzuri atafute sehemu aoneshe kiwango chake ili kila mmoja afurahie kipaji chake kikubwa alichonacho maana uwezo wake mkubwa unafahamika.

Waliotoka Simba kwenda Yanga tuwaaangalie namna walivyofanya kisha tutapata uhalisia wa hili.

Kelvin Yondani

Alitua mwaka 2011 alichokosa Yanga kombe la Afrika pekee ila kila kitu amepata hela, makombe ya ndani na mafanikio uwanjani.

Matokeo mazuri ya Yanga katika ukuta aliyabeba mgongoni mwake alicheza kwa uwezo mkubwa na alikuwa ndani ya timu ya taifa kwa muda mrefu sana.

Nurdin Bakari

Huenda waliowengi wasimfahamu  kiungo huyu aliondoka Simba baada ya michuano ya vijana waliochini ya miaka 20 ya timu ya taifa ya Tanzania pia lile sakata la kughushi umri , baada ya hapo mwaka 2007 aliondoka  Mnyama  akiwadanganya Simba kuwa anaumwa moyo alicheza Yanga kwa kiwango safi kabisa.

Ibrahimu Ajibu

Tanzania Sports
Ajibu

Alipotua Yanga hakuwa na ukubwa huo japo kila mtu alijua kijana huyo alikuwa na kipaji kikubwa sana.

Alipotua Jangwani alipewa nafasi kubwa ya kuwa huru alicheza kwa mafanikio makubwa japo alikuja kipindi ambacho utawala wa Yanga ulipotea hakuchukua ubingwa.

Tulishasema juu alifunga magoli 8 na kutoa pasi za mwisho 15 hii imekuwa historia kwa ligi kuu Tanzania Bara.

Mchezaji pekee ambaye alitoka Simba na akafeli Yanga ni Ramadhani Waso beki wa kushoto huyu ukweli hakuwa na kiwango safu kama alivyokuwa Simba ila waliobaki walifanya vizuri sana.

Vipi wadau mnasubiri tummjadili Benard Morrison juu ya mwenendo wake Simba? Huyu bado hatuwezi kumjadili kwakuwa bado ila hadi sasa bado hajaonesha cheche kama alizokuwa nazo Yanga.

Wachezaji wengine waliocheza vilabu hivyo viwili ni pamoja na Haruna Moshi, Bakari Malima, Said Maulid na Edibiliy Jonas Lunyamila.

Wapo wengi sana ila tosheka na baadhi tu ya nyota hao ambao walikipiga katika timu hizo, kwa wenye kumbukumbu hao ambao sijawachambua mtaweza kusema walivyoingia Simba ilikuwa na walivyokuwa Yanga ilikuwaje.

Nawe unaweza kushiriki katika ukurasa wetu wa Facebook utuambie ni nani alitoka huko kaenda kuhu.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

69 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Visa vya Camp Nou

LA LIGA; EL Clasico bado ni mechi kubwa duniani?

LH MS

Lewis Hamilton kuvunja rekodi ya Michael Schumacher