in

LoveLove SurprisedSurprised

Yanga, Azam FC utamu wake uko hapa

Mchezaji wa Azam FC

Kuelekea katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga dhidi ya Azam FC mchezo utakaopigwa pale kwa Mkapa siku ya jumapili saa kumi jioni.

Mchezo huo unaweza ukawa wa kuamua nani ataibuka kuwa mshindi wa pili ambapo Simba ndio kinara  akiwa na alama 72.

Tuanzie hapa sasa Yanga wana alama 55 wakati Azam FC wakikusanya alama 57 wakiwa sawa michezo waliyocheza.

Kitu pekee ambacho kinavutia katika mchezo huo ni ufanano wao katika rekodi zao tangu Azam FC ilipoingia ligi kuu Tanzania Bara mwaka 2007.

Timu hizo zimecheza michezo 23 kila mmoja, katika nyakati zote hizo zinafanana kila kitu kasoro magoli tu.

Timu hizo zimetoka sare mara 7 kila mmoja na kila timu imekubali vipigo mara nane.

Hebu angalia rekodi hii, Yanga imeshinda mara 8 wakati Azam FC nayo ikishinda mara nane.

Tufanye hesabu hapa ili usivurugwe angalia hapa kila timu imecheza michezo 23, sare 7, zimeshinda mara 8 na kufungwa mara 8, hapo ukifanya mahesabu utapata mechi 23 kila timu.

Tanzania Sports
Wachezaji wa Yanga, wakiwa mazoezini

Utofauti uliopo ni wa magoli tu ambapo Wanarambaramba kutoka nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam Azam FC imefunga magoli 31 wakati Yanga wameambulia magoli 30.

Hapa kila mmoja atakuwa na hamu ya kuona nani ataibuka mshindi ili awe na ushindi wa moja kwa moja kwa msimu huu kabla haujaisha.

Kabla ya mengine hebu tuangalie rekodi zao kunako msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara msimu huu hizo hapo chini.

Wakiwa na utofauti wa goli za kufunga na kufungwa ambapo wenyeji Yanga wakitundika nyavuni magoli 33 na kufungwa magoli 21 wakati Azam FC wakifunga magoli 39 na kufungwa 20.

Yanga imetoa sare mara 10 na kupoteza minne wakati Azam FC imepoteza michezo 6 na sare 6.

Wanajangwani wamekusanya alama 55 huku Azam FC wakiwa na alama 57 ambapo tayari nishakueleza hapo juu.

Wakati wote ambapo Yanga na Azam zinakutana kumekuwa na burudani ya aina yake, imefika hatua hadi wapenzi na mashabiki wa bongo wakisema kuwa Azam ikicheza na Simba mchezo hauwi mzuri kwakuwa mshindi anajulikana.

Zamani kidogo iliwahi kutokea  Yanga na Azam wachezaji wake kupigana ngumi uwanja wa taifa nakumbuka Stephano  Mwasika ndio alikuwa kinara wa upigaji ngumi muamuzi alikuwa Israel Nkongo.

Tuangalie vikosi vya timu zote mbili ili tuje tubeti mwisho wa stori yetu hii.

Kikosi cha Yanga, Metecha Mnata, Jaffari Mohamed, Juma Abdul, Said Makapu, Kelvin Yondani, Pappy Tshishimbi, Balama Mapinduzi, Feisal Salum, Ditram Nchimbi, Haruna Niyonzima na Patrick Sibomana.

Kikosi cha Azam FC, Benedict Haule, Abdul Shomary, Bruce Kangwa, Agrrey Morris, Yakubu Mohamed, Aboubakari Salum, Andrey Simchimba, Frank Domayo,Shaban Iddi, Richard Djodi na Iddi Kipagwile.

Vikosi vyote viwili  vinanyota wa kutosha kutoa burudani lakini wengi wakikumbuka mchezo wa kwanza Yanga ilikufa kwa goli 1-0.

Ugumu wa mchezo kwa kila utakuwa eneo la katikati kwakuwa kila timu ina wachezaji wanaoweza kucheza vizuri eneo hilo lakini pia kutafuta nafasi ya pili ambayo ina umhimu huenda siku za baadae.

Yanga watatumia winga pia kwakuwa nyota wao Benard Morrison amerejea hivyo upande huo utakuwa na ugumu wa aina yake.

Huku Andrew Simchimba wa Azam akiwa katika kiwango bora kabisa umbo lake lakini uwezo wake wa kupiga mipira ya mbali inaweza ikawa tatizo kwa Yanga.

Bado nina wasi sana na mchezo huu, kwani inawezekana ikawa ‘patulo’ yaani sare ya kufungana magoli au ya bila kufungana.

Kocha wa Yanga amesema kuwa mchezo huo wanauchukulia kwa umuhimu mkubwa kutokana na umuhimu wa kuhitaji nafasi ya pili.

“Tunahitaji kushinda mchezo huu ili tuwe katika nafasi ya pili huenda tukacheza mashindano ya kimataifa,”alisema.

Aymael anahistoria ya kushinda mechi kubwa huku Aristica Ciaoba kocha wa Azam naye akiwa na sifa hiyo.

Naomba ieleweke kuwa msimu huu Tanzania itapeleka timu mbili , moja ligi ya Mabingwa, nyingine kombe la Shirikisho.

Ila kuna tetesi zinasema kuna nchi itafutiwa ushiriki na huenda nafasi ikaja Tanzania hiyo nayo haijawa habari kamili.

Je wewe unahisi timu ipi inaweza kushinda na hatimaye kuondoka na alama tatu muhimu, unaweza kutoa maoni yako hapo chini.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

74 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Kikosi cha Simba Sports Club

Ibrahim Ajib, Jangwani inakuhitaji

Manchester United’s Paul Pogba

Dakika 33 za dhahabu za Paul Pogba