in , ,

*WATATU KUSHIRIKI KOZI YA FUTURO ADDIS ABABA*

Watanzania watatu ni miongoni mwa washiriki 30 walioteuliwa kuhudhuria kozi
ya wakufunzi ya waamuzi ya FUTURO III itakayofanyika Addis Ababa, Ethiopia
kuanzia Oktoba 5 hadi 10 mwaka huu.

Leslie Leonard Liunda, Abdi Soud Mohamed na Israel Nkongo Mujuni ndiyo
watakaoshiriki katika kozi hiyo itakayoendeshwa na wakufunzi kutoka
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Kozi hiyo pia itakuwa na washiriki kutoka nchi nyingine tisa za Afrika.
Nchi hizo ni Gambia, Ghana, Kenya, Liberia, Nigeria, Seychelles, Sierra
Leone, Somalia na Uganda.

*WARUNDI KUCHEZESHA WANAWAKE U20 KOMBE LA DUNIA*

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Burundi
kuchezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa wanawake chini ya miaka 20
Kanda ya Afrika kati ya Tanzania na Msumbiji.

Waamuzi hao watakaochezesha mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza
itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Oktoba 26 na 27 mwaka
huu wataongozwa na Ines Niyonsara. Atasaidiwa na Jacqueline Ndimurukundo na
Axelle Shikana.

Irene Namiburu kutoka Uganda ndiye atakayekuwa mwamuzi wa mezani wakati
Kamishna wa mechi hiyo ni Evelyn Awuor wa Kenya. Mechi ya marudiano
itachezwa jijini Maputo kati ya Novemba 9 na 10 mwaka huu, na itachezeshwa
na waamuzi kutoka Madagascar.

Fainali hizo za Kombe la Dunia zitafanyika mwakani nchini Canada, ambapo
Tanzania inashiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo ya Kombe la Dunia kwa
wasichana.

Timu ya Tanzania tayari imepiga kambi mkoani Pwani ikiwa chini ya Kocha
wake Rogasian Kaijage.

Wachezaji walioko kambini ni Amina Ally, Amina Ramadhan, Amisa Athuman,
Anastazia Anthony, Anna Hebron, Belina Julius, Donisia Daniel, Esther
Mayala, Fatuma Issa, Gerwa Lugomba, Happiness Lazoni, Harriet Edward,
Hellen Maduka, Irene Ndibalema, Jane Cloud, Khadija Hiza na Latifa Salum.

Wengine ni Maimuna Hamis, Mwanaidi Khamis, Najiati Abbas, Neema Paul,
Niwael Khalfan, Rehema Abdul, Sabahi Hashim, Sada Ramadhan, Shamimo Hamis,
Shelder Boniface, Stumai Abdallah, Tatu Idd, Therese Yona, Violet Nicholas,
Vumilia Maarifa, Yulitha Kimbuya na Zena Said.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Arsenal wawanyamazisha Napoli

Man United wachanganywa Ukraine