in

Wanamichezo wa Tanzania waaga michezo ya Madola

WACHEZAJI  20  wa Tanzania tayari wamekwishaaga mashindano ya Jumuiya ya Madola yanayofikia tamati Alhamisi  mjini New Delhi, India baada ya kupoteza katika michezo yao yote.

Leo ni siku ya tisa tangu kufunguliwa kwa mashindano hayo ambapo Tanzania iliwakilishwa na wachezaji 28, lakini wachezaji waliobaki ambao wanaweza kutufuta machozi ni nane tu ambao kati yao hakuna aliyecheza hata mmoja hivyo bado hawajaonja tamu na chungu ya mashindano hayo.

Akizungumza na Mwanachi kwa njia ya simu kutoka New Delhi, Mkuu wa msafara wa Tanzania, Juliana Yasoda alisema kuwa tayari mabondia nane wa Tanzania na waogeleaji wanne wamekwishatolewa.

“Wachezaji sita wa Mpira wa Meza wanamalizia tu mechi zao, lakini tayari wamekwishatolewa pia Paraolimpiki mmoja ametolewa na mmoja atacheza leo, lakini tegemeo limebaki kwenye Riadha na mchezaji huyo wa Paraolimpiki.

“Wachezaji wetu walijitahidi, lakini bahati haikuwa yao hivyo nguvu zetu zote tumezielekeza kwa wachezaji wetu ambao bado hawajacheza ili angalau waweze kufanya vizuri na kurejea na medali hizo chache za wachezaji waliosalia,” alisema Yasoda.

Tegemeo la Tanzania limebaki kwa wanariadha  Marco Joseph katika mbio za mita  10,000 na 5,000,  Frank Martin  anayekimbia mita 800 na Barae Hera  anayekimbia Mita 1,500 na 800.

Wanariadha wengine ni Shamba Kitin, Samson Ramadhan na Patrick Nyangero watakao kimbia mbio za Marathon (km 42) upande wa wanaume na kwa Wanawake Restituta Joseph atakimbia Marathon (KM 42), pamoja na mchezaji mmoja wa michezo ya walemavu, ambao bado hawajacheza tangu kuanza kwa mashindano hayo.

Katika mashindano hayo yaliyofunguliwa rasmi Oktoba 3, Tanzania ilitupa karata yake ya kwanza katika mchezo wa kuogelea Oktoba 4 kwa muogeleaji wake Mariam Foum kuanza vibaya hivyo kufungua dimba bila matumaini huku wachezaji sita wa Mpira wa Meza wakishindwa kutamba siku hiyo hiyo mbele ya Ghana na kuishia kutolewa pia katika hatua za awali.

Oktoba 5 wachezaji watatu wa Tanzania pia waliendelea kuwapa simanzi mashabiki wao hapa nchini pamoja na kupoteza matumaini ya kuibuka na Medali nyingi katika mashindano hayo kwa kufanya vibaya.

Wachezaji hao ni Sunday Elias na Hashim Saimon (Ngumi), Khalid Rushaka (Kuogelea).

Nasser Mafuru na Seleman Kidunda (Ngumi) wiki iliyopita  walianza kurejesha matumaini ya Watanzania yaliyokuwa yamepotea baada ya kuibuka na ushindi katika mapambano yao ya awali, lakini walishindwa kung’ara katika hatua ya mtoano juzi na kujikuta wakiaga mashindano hayo.

Mbali na wachezaji hao pia mwanariadha Damian Chopa,  mchezaji wa michezo ya walemavu Ignas Mtemve, muogeleaji Magdalena Mosha, mabondia Haruna Swaga, Leonard Machichi na Revocatus Shomari wameaga mashindano hayo.

Enhanced by Zemanta

Report

Tottenham Hotspur

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Loading…

0

FIFA

Mazungumzo baada kazi