in , , ,

Wachezaji EPL na uchovu wa Kombe la Dunia

FAINALI za Kombe la Dunia zimemalizika nchini Urusi na wachezaji
waliokuwa huko sasa wapo mapumzikoni.

Klabu mbalimbali zimeanza maandalizi ya msimu ujao wa soka 2018/19
zikiwamo za Ligi Kuu ya England (EPL) bila wanasoka wake nyota
waliokuwa huko.

Klabu saba za ligi hiyo kubwa na maarufu zaidi duniani zilikuwa na
walau wachezaji 10 kwenye kazi ya kimataifa kwa nchi mbalimbali huko
Urusi na sasa wapo mapumzikoni.

Ni klabu za Bournemouth na Fulham tu zinazoendelea na mazoezi ya
maandalizi ya EPL ijayo wakiwa na vikosi timilifu.

Iwapo kuna uwezo wa kuwa na soka sana au la ni maswali ambayo huulizwa
wakati wa kiangazi cha fainali za Kombe la Dunia na kunyanyua vichwa
juu kuhusu mipango ya ligi za ndani.

EPL klabu wapo katika mambo tofauti ikiwa ni pamoja na nyingine kuanza
kuzoeana miongoni mwa wachezaji na makocha lakini pia kuendelea kwa
usajili.

Msimu mpya wa ligi unaanza kama kawaida licha ya uchovu wa wachezaji
waliokuwa kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia, hasa wale waliosonga
mbele hadi walau haua za robo, nusu au fainali yenyewe.

Mashindano hayo huwachosha wachezaji kimwili na kiakili kutokana na
ugumu wake na utofauti pamoja na ushindani mkubwa uliopo kwenye kazi
hiyo. Baadhi ya wachezaji pia huingia humo wakiwa katika mawazo juu ya
kujiunga na klabu mpya au wakiwa na utata wa uhakika wa kubaki kwenye
klabu zao.

Idadi ya wachezaji na vilabu vyao (EPL) na hatua waliyofikia katika mashindano ya kombe la Dunia Urusi.

Makocha wameanza kulia juu ya kukosekana kwa baadhi ya wachezaji
muhimu, mmoja wao akiwa ni yule wa Manchester United, Jose Mourinho,
maana nyota wake kadhaa wapo kwenye mapumziko bado ili kuhakikisha
wanakuja kuwa timamu kwa mechi msimu ujao.

Kwa kawaida watakuwa na mapumziko ya walau wiki tatu ambazo ni sawa
kwa wachezaji waliokaa hadi Juni lakini ngumu kidogo kwa waliosonga
mbele hadi katikati ya Julai hii.

Kwa kawaida kuna pengo la wiki nne tu kati ya mwisho wa fainali hizo
na kuanza kwa EPL, hata kama Bodi ya EPL imesogeza mbele zaidi muda wa
kuanza kwa EPL hadi Ijumaa usiku.

Manchester United na Leicester ndio watakaokuwa wa kwanza kwenye
mtanange na ilivyo ni kwamba waliwakilishwa vilivyo huko Urusi na
wachezaji wake.

United walikuwa na wachezaji 11 Urusi, ikiwa ni pamoja na Paul Pogba
aliyekwenda mbali hadi kucheza mechi ya fainali na kunyakua kombe,
akishiriki dakika 4,230 za nchi yake uwanjani. Leicester walikuwa na
wachezaji 10 kwenye michuano hiyo, aliyeng’ara zaidi akiwa Mwingereza
Harry Maguire aliyepata dakika zake 700.

Hawatarajiwi kucheza kwenye mechi ya kwanza Old Trafford usiku huo wa
Ijumaa ya kwanza kwenye ligi kuu na wapo wengine kadhaa.

Bournemouth na Fulham hawakuwa na mchezaji hata mmoja kwenye fainali
hizo kwa hiyo wachezaji wao wote walipata muda wa kutosha wa kupumzika
wakati Cardiff, Crystal Palace, Burnley na Newcastle waliathiriwa
kidogo zaidi kwa wachezaji wawili wawili kwenda Urusi.

Everton walishuhudia zaidi ya nusu ya dakika 1,324 za fainali hizo
zikiwa na kipa wake Jordan Pickford kwneye jezi za England wakati
Dejan Lovren wa Liverpool alifika fainali akicheza na dakika za ziada,
jumla akifikisha dakika 706.

Washabiki wengi wangependa kuwatazama wachezaji waliokuwa kwenye
fainali hizo waliochoka kuliko walio ‘freshi’ ambao hawakwenda Urusi
na labda wapo sawa, kutokana na umaarufu ule.

Spurs, Chelsea na wengine wanao waliowika Urusi kama Harry Kane na
Kieran Trippier na kwa hakika kocha Mauricio Pochettino atakuwa na
wasiwasi juu ya lini wachezaji hao watakuwa wametulia vyema kuingia
uwanjani, akiwamo kipa wa Ufaransa, Hugo Lloris.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Hivi bado hatujaona pesa kupitia neno “Ali Kiba”?

Tanzania Sports

UITALIANO UTAKUWA NGUZO YA MAURIZIO SARRI PALE CHELSEA?