in , ,

WAAMUZI WA ANGOLA KUCHEZESHA MECHI YA STARS DAR!

Kocha mkuu wa Taifa Stars

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeteua waamuzi kutoka
Angola kuchezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa
Stars) na Morocco (Lions of the Atlas).

Mechi hiyo ya kundi C itachezwa Machi 24 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam. Ivory Coast ndiyo inayoongoza kundi hilo ikiwa na pointi nne
na kufuatiwa na Taifa Stars yenye pointi tatu.

Mwamuzi wa mechi hiyo ni Helder Martins de Carvalho wakati mwamuzi msaidizi
namba moja ni Inacio Manuel Candido huku Ricardo Daniel Cachicumi akiwa
mwamuzi msaidizi namba mbili. Mwamuzi wa mezani (fourth official) ni
Antonio Muachihuissa Caxala.

Waamuzi hao watawasili nchini saa 1.20 usiku Machi 22 mwaka huu kwa ndege
ya Kenya Airways wakitokea Luanda, Angola kupitia Nairobi, Kenya.

Kamishna wa mechi hiyo atakuwa David Fani kutoka Botswana anatarajiwa
kuwasili Machi 22 mwaka huu saa 1.45 usiku kwa ndege ya South African
Airways.

Naye mtathmini wa waamuzi (referee assessor) Neermal Boodhoo kutoka Afrika
Kusini atawasili nchini Machi 22 mwaka huu 1.45 usiku kwa ndege ya South
African Airways.

*MECHI YA RUVU SHOOTING, YANGA YAINGIZA MIL 62/-*

Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Ruvu Shooting na Yanga iliyochezwa
jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 62,228,000 kutokana na
watazamaji 10,929.**

Viingilio katika mechi hiyo namba 146 iliyomalizika kwa Yanga kuibuka na
ushindi wa bao 1-0 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000
huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 14,336,764.95 wakati Kodi ya Ongezeko
la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 9,492,406.78.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,289,880.48,
tiketi sh. 4,136,390, gharama za mechi sh. 4,373,928.29, Kamati ya Ligi sh.
4,373,928.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,186,964.14,
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 850,486.06 na Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 850,486.06.

* *

*TAIFA STARS YAINGIA KAMBINI KUIWINDA MOROCCO*

Taifa Stars imeanza kambi jana jioni (Machi 16 mwaka huu) ambapo wachezaji
14 kati ya 23 walioitwa wameripoti na kufanya mazoezi leo asubuhi chini ya
Kocha Kim Poulsen.

Wachezaji walioripoti ni nahodha Juma Kaseja kutoka Simba na msaidizi wake
Aggrey Morris wa Azam, Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir
Haroub (Yanga), Nassoro Masoud Cholo (Simba), Shomari Kapombe (Simba) na
Salum Abubakar (Azam).

Wengine ni Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Frank Domayo (Yanga),
Mwinyi Kazimoto (Simba), Mrisho Ngasa (Simba) na Simon Msuva (Yanga).

Wachezaji Hussein Shariff, Issa Rashid na Shabani Nditi ambao timu yao ya
Mtibwa Sugar jana ilicheza mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) mjini Turiani
wataripoti kambini leo jioni.

Kikosi hicho kitakamilika Jumanne asubuhi baada ya wachezaji walio katika
kikosi cha Azam nchini Liberia kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho kurejea
nchini. Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea TP Mazembe ya Jamhuri
ya Kidemorasi ya Congo (DRC) wanatarajiwa kutua nchini kesho usiku.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Manchester United kwa raha zao

Chelsea tatu bora