in , ,

Wambura, wengine wasimamishwa uanachama Simba..

*WACHEZAJI KULIPWA LEO

UONGOZI wa Klabu ya Soka ya Simba umetangaza rasmi kumsimamisha uanachama aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Urais katika uchaguzi uliofanyika Jumapili, Michael Wambura, pamoja na wengine 70 kutokana na hatua za kwenda kufungua kesi kwenye mahakama za kawaida za nchi imeelezwa jana jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye makao makuu ya klabu hiyo yaliyoko mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini jana, Rais wa Simba, Evans Aveva, alisema kuwa maamuzi ya kumsimamisha Wambura na wenzake yametolewa na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ambao walikutana kwa mara ya kwanza hapo juzi.

Aveva alisema kuwa kamati hiyo imechukua maamuzi ya kuwasimamisha kwa kufuata ibara ya 11 (1) (b) ya katiba ya Simba na kuongeza kuwa hatma yao itajulikana katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa klabu unaotarajiwa kufanyika Agosti 3.
Rais huyo alisema kuwa wameamua kuchukua hatua hiyo ili kuilinda katiba ya Simba na uanachama wa klabu hiyo katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

“Saula la Wambura lilijadiliwa lakini hatukufikia muafaka na kuamua lipelekwe katika mkutano mkuu ili wanachama waamue, tumewasimamisha wale 69 na katika kesi ya mwaka 2010 aliyofungua alishirikiana na Juma Mtemi, naye tumemsimamisha,” alieleza Aveva.
Alisema kuwa katika mkutano mkuu unaokuna wanachama watajadili pia ripoti ya fedha na mabadiliko ya katiba ambayo yameonekana kuwa na mapungufu.

Kiongozi huyo pia aliwashukuru wanachama wote wa Simba waliompigia na wasiompigia kura kwa sababu kila mmoja ametekeleza haki yake ya kidemokrasia.

Alisema uchaguzi umekwisha sasa wanachama wote ni kitu kimoja waungane kuijenga klabu yao.
“Sasa tuungane kutekeleza ahadi zetu ambazo ni pointi tatu uwanjani, umoja na maendeleo, tusahau tofauti zetu, Simba ni mhumi kuliko sisi sote,” alisema kiongozi huyo.

WACHEZAJI KULIPWA LEO

Aveva alisema kuwa uongozi wake unatarajia leo kuwalipa mishahara wachezaji wake ili kuwaweka tayari kwa ajili ya kuanza maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Alisema kuwa kikosi cha timu hiyo kitaanza mazoezi yake ifikapo Jumatano Julai 9 huku pia wakianza maandalizi ya tamasha la Simba Day litakalofanyika Agosti 8 mwaka huu.

Alisema kwamba kocha mkuu wa timu hiyo, Mcroatia, Zdravko Logarusic, atarejea nchini Jumatatu na taratibu za kumtumia tiketi ya ndege zimeshaanza.

WAJUME WAPYA, KAMATI MPYA

Aveva aliwataja wajumbe watatu wapya wa kuteuliwa watakaoingia katika Kamati ya Utendaji ni pamoja na Mohammed Nassor, Musley Al Ruwey na Salim Abdallah huku wengine wawili waliobakia kwa mujibu wa matakwa ya katiba atawatangaza baadaye.

Uongozi huo mpya pia jana ulitangaza kamati tatu zitakazosimamia shughuli mbalimbali za kila siku lakini akiitaja Kamati ya Usajili itakuwa ni ya muda na itaongozwa na Hanspoppe Zacharia, Kassim Dewji, Saidi Tulliy, Musley Al Ruweh, Crescentius Magori na Rodney Chiduo.
Aliwataja wajumbe wanaounda kamati ya mashindano itakayokuwa chini ya mwenyekiti, Mohammed Nassor, ni Iddi Kajuna, Jerry Yambi, Hussein Simba na Mohammed Omary.

Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana ni Tulliy, Ally Suru, ambao wote ni wajumbe wa Kamati ya Utendaji, Patrick Rweyemamu, Mulamu Nghambi, Madaraka Suleiman na Amina Poyo

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Robo fainali yapikwa

Barca wakaribia dili la Suarez