in

Vita kubaki EPL ngumu

Vita ya kubaki EPL

Ligi Kuu ya England (EPL) inatarajiwa kurejea Juni 17 kwa ajili ya kumaliza mechi 92 zilizositishwa kutokana na kuenea kwa virusi vya Corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu na kuua maelfu ya watu.

Inaporejea ligi hiyo katika mazingira mapya ambapo washangiliaji hawataruhusiwa uwanjani isipokuwa wachezaji, makocha na maofisa wasiozidi 300, kuna mengi yanaangaliwa, hasa kwenye vita ya nani atashuka daraja na nani watabaki kwenye ligi hiyo maarufu zaidi duniani.

Mechi ya kwanza inasubiriwa kwa hamu na wadau wanataka kuona kipi kitatokea kwa sababu mmoja wao yuko kwenye eneo la kushuka daraja. Huyo ni Aston Villa mwenye mchezaji wa kwanza Mtanzania kucheza EPL – Mbwana Samatta.

Watakuwa wanacheza na  dhidi ya Sheffield United Jumatano ya Juni 17 saa 12 jioni, kabla ya Arsenal kukaribishwa Etihad na Manchester City usiku was aa 2.15 siku hiyo hiyo.

Kila mmoja anajua kwamba suala ni la lini na wapi na si iwapo, Liverpool watachukua ubingwa. Wana alama 25 zaidi ya wale wanaowafuata na ni dhahiri watawavua ubingwa Manchester City. 

Chenye utata mkubwa zaidi kwa sasa ni swali kwamba ni klabu zipi tatu ambazo msimu ujao hazitapata fursa ya kusafiri kucheza Anfield kukabiliana na vijana wa Jurgen Klopp katika mechi za EPL kwani zitakuwa zimeshuka daraja.

Vita ya kuepuka kushuka daraja kwa klabu zilizo huko chini ni kubwa sana kama ambavyo haijapata kutokea, kutokana na ukweli kwamba zimebanana sana. Kuna tofauti ya alama nne tu kati ya Villa walio nafasi ya pili kutoka chini na Brighton & Hove Albion wanaoshika nafasi ya 15.

Alama moja tu itatenganisha klabu nne, juu na chini ya ukingo wa kushuka daraja ikiwa Villa watapata alama yoyote kutoka kwa Sheffield United na kuwatingisha wenzake. Kila matokeo yatakuwa na maana kubwa – iwe chanya au hasi kwa klabu husika na hili sasa ni suala la kufa au kupona kwa sababu kuna athari mbaya kifedha kwa klabu inayoshuka daraja.

Kadiri ligi itakavyokuwa ikisogea, huku mechi zikiwa karibu karibu – katikati ya wiki na wikiendi, ndivyo klabu zitakavyokuwa katika harakati na shinikizo la kujizuia kushuka daraja.

Kwa sasa klabu zilizo kwenye eneo la kushuka daraja ni Norwich wanaoshika mkia wakifuatiwa na Villa na Bournemouth. Wengine hatarini japo wako juu ya mstari ni Watford, West Ham na Brighton. Wa chini kabisa ana alama 21 tu wakati wa juu miongoni mwao anazo 29 na anayefuata ambao niSouthampton wanazo 34 huku Newcastle wakiwa na alama 35.

Mechi zote zitaoneshwa na vituo mbalimbali vya televisheni, ikiwa ni pamoja na vilivyoongezwa na Baadhi ya mechi zitakuwa bure baada ya janga la Covid-19 kutikisa vilivyo dunia na kupelekea baadhi ya nchi kulazimisha wananchi wao kujifungia ndani isipokuwa ikilazimu kwenda kwenye mahitaji muhimu na matibabu.

Villa wana bahati kwa sababu mechi zao nne za awali zitakuwa nyumbani, hivyo bila shaka watatumia fursa hiyo kujikusanyia alama zaidi na kukwepa kushuka daraja, japokuwa hawatakuwa na ile nguvu ya washabiki wao kadiri ya 40,000.

Miongoni mwa kklabu zilizo kwenye hatari ya kushuka daraja, ni Brighton tu waliofanikiwa kufanya vyema zaidi nyumbani kwa Villa. Kucheeza kwao nyumbani ni bonasi kwa sababu hakuna uchovu wa kusafiri, baada ya wiki 14 za kujifungia ndani bila mechi.

Aina ya vita itakayopigwa kwenye kuepuka kushuka daraja si ya kawaida na kwa hali ilivyo na ushindani mkubwa, hapana shaka kwamba watakaoshuka si ajabu wakajulikana siku za mwisho kabisa.

Ratiba ya timu sita za mwisho kwenye msimamo wa EPL:-

Jumatano, June 17
18:00 Aston Villa v Sheffield United (Sky Sports)

Ijumaa, June 19
18:00 Norwich v Southampton (Sky Sports)

Jumamosi, June 20
12:30 Watford v Leicester (BT Sport)
15:00 Brighton v Arsenal (BT Sport)
17:30 West Ham v Wolves  (Sky Sports)
19:45 Bournemouth v Crystal Palace (BBC)

Jumapili, June 21
16:15 Aston Villa v Chelsea (Sky Sports)

Jumanne, June 23
18:00 Leicester  v Brighton (Sky Sports)
20:15 Tottenham v West Ham (Sky Sports)

Jumatano, June 24
18:00 Newcastle v Aston Villa (BT Sport)
18:00 Norwich v Everton (BBC)
18:00 Wolves v Bournemouth (BT Sport)

Alhamisi, June 25
18:00 Burnley v Watford (Sky Sports)

Jumamosi, June 27
12:30 Aston Villa v Wolves (BT Sport)

Jumapili, June 28
16:30 Watford v Southampton (Sky Sports)

Jumanne, June 30
20:15 Brighton v Manchester United (Sky Sports)

Jumatano, July 1
18:00 Arsenal v Norwich (BT Sport)
18:00 Bournemouth v Newcastle (Sky Sports)
20:15 West Ham v Chelsea (Sky Sports)

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Dar Young Aricans

Molinga,Yikpe, Zahera na Yanga

Tofauti kati ya Uingereza na England

Ligi Kuu England ni ipi hasa?