in , ,

VIPI WAGOMBEA UCHAGUZI HAWATAJI MICHEZO NDANI YA KAMPENI ZAO ?

*Uchaguzi 25-Oktoba-2015-Tanzania*

 

*Suala la michezo bado liko hewani na halieleweki*

 

Wakati kampeni za uchaguzi utakaofanyika Jumapili Oktoba 25 zikiendelea ni vyema tukiangalia kauli zao kuhusu michezo. Hivi kwanini hatujamsikia mgombania yeyote akitaja atakalolifanya kuendeleza michezo akishinda?

Mara ya kwanza kusikia michezo ikizungumziwa kwa kina ni siku chache zilizopita ambapo Rais Jakaya Kikwete alipewa tuzo kwa kuisaidia tasnia ya michezo nchini. Alikabidhiwa zawadi  na Chama cha Wanahabari wa Michezo Tanzania ( TASWA).  Siku hiyo hiyo Rais Kikwete alieleza pia namna anavyomtegemea mgombania Rais wa CCM, John Pombe Magufuli kuendeleza dimba. Atamshauri aendelee kupigania  michezo Tanzania.

Rais Kikwete alisema anatuachia kituo cha kujenga vipaji vya wanamichezo chipukizi kilichoko Kidongo Chekundu, Dar es Salaam. Kilijengwa  na kampuni ya umeme ya Symbion Power baada ya safari ya Rais  klabu ya Sunderland mwaka juzi.

 Oktoba 17 kituo cha Kidongo Chekundu kitaanza rasmi.

Timu ya taifa ya TANZANIA
Timu ya taifa ya TANZANIA

 

Je ni kiongozi gani mwingine anayeahidi kuendeleza michezo kiasi hiki Tanzania? Na tunapozungumzia maendeleo ya michezo tuna maana gani? Kwanza kabisa tukubaliane Tanzania kama nchi nyingine zozote jirani imeshiba vipaji. Wakati Waziri wa Utamaduni, Vijana, Habari na Michezo, Dk Fenella Mukangara, akieleza makadirio ya wizara  yake kwa 2014 / 2015, alisema asilimia mia 70 ya Watanzania ni vijana- wanaotegemewa “kuchangia uchumi” wa taifa.

Humo humo ndimo mna uwekezeaji katika michezo, kimafunzo.

 

Waziri Mukangara : “Hivi sasa zaidi ya asilimia 50 ya waalimu ambao hushiriki katika uendeshaji na ufundishaji wa michezo kwa ajili ya mashindano ya shule za msingi (UMITASHUMTA) na shule za sekondari (UMISETA) ni wahitimu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya, Vituo vya Michezo na Mpango wa Michezo kwa Jamii.”

Akasisitiza kuwa Wizara yake imeendelea kutafuta maeneo mapya ya ushirikiano wa kimataifa na kufuatilia utekelezaji wa Mikataba kati ya nchi marafiki na Tanzania katika Sekta ya Michezo.  “Kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China.”

Haya ni baadhi ya mambo yaliyofanywa na serikali ya awamu ya nne inayoondoka. Lakini je yataendelezwa vipi baada ya  Oktoba 25?

Tumeona namna Rais Kikwete anavyopenda michezo. Tumemsikia Waziri mhusika wa kitengo hiki akizungumzia ari ya kuendeleza michezo na kuwashukuru asilimia 70 ya wananchi ambao ni vijana.

Advertisement
Advertisement

Mwezi Desemba mwaka jana wakati wa ufunguzi wa michuano ya michezo baina ya wabunge wa Afrika Mashariki mjini Arusha, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Nyirembe Munasa aliwataka wabunge wasiwe na imani za ushirikina katika michezo. Wamtegemee Mungu kwani michezo ni kama ajira.

Mmoja wa washindi wa michezo hii alikuwa Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mara, Esther Matiko. Alipigwa picha kavalia mavazi ya michezo.

Katika mahojiano aliyofanyiwa na  gazeti la Mwananchi mwezi Januari 2015, Bi Matiko alisifiwa kama mhamasishaji wa vijana. Aliongelea juu ya maendeleo ya kina mama na watoto. Alifafanua kwanini anapenda siasa na nini maana yake. Lakini hakugusia michezo.

Suala la michezo bado liko hewani na halieleweki.

Pamoja na sisi kutofanya vizuri kimataifa, ikitokea siku Tanzania ikateuliwa kuwa sehemu ya michuano mathalan ya Kombe la Afrika (CAF), je tunavyo viwanja vya kufaa?

Uwanja wa Uhuru wa Dar es Salaam unafaa maana umekamilishwa karibuni. Uwanja wa Maji Maji , Songea ni wa wastani lakini hauna majani tosha. Viwanja  vya Nangwana (Mtwara) na Kirumba (Mwanza)  haviko katika hali inayolingana na viwanja vya wenzetu nchi nyingine.

Kifupi,  hatuna mwelekeo wa kuwa na matumaini kwamba serikali ijayo na wahusika wake watatuoa katika giza  la kutofanya vizuri kimichezo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

LIGI YA MABINGWA ULAYA:

Tanzania Sports

LIGI YA EUROPA: