in , ,

VAN PERSIE AMCHANA KOCHA

Van Gaal hakunitendea haki

Mchezaji wa Manchester United aliyeuzwa nchini Uturuki majuzi, Robin van Persie, amefungua yaliyo moyoni mwake, akisema kocha Louis van Gaal hakumtendea haki kwani hakumpa fursa kuonesha vitu uwanjani.

RVP aliyejiunga United akitoka Arsenal ambako alikuwa nahodha na mfungaji bora kwa England anasema kwamba Mdachi mwenzake huyo hana huruma na ndiye amesababisha akapoteza kiwango na kazi yake Old Trafford.

Van Persie anasema alishangaa kuona uhusiano baina yake na LVG ukiporomoka ghafla na kwa haraka na kufuatiwa na kuuzwa katika klabu ya Fenerbahce badala ya kumpa nafasi ya haki na uaminifu kubaki Manchester United wafanye kazi.

Van Persie anasema kwamba licha ya kukubalia uamuzi wa kuuzwa kwake, hakupewa hata fursa ya kuongezewa mkataba walau kwa muda mfupi wala LVG hakuzingatia kwamba baada ya kuwa majeruhi alitakiwa kuanzia sasa kupewa muda arudi kwenye kiwango chake.

“Niliomba kucheza walau na kikosi cha pili ili nipate dakika za kutosha kwa ajili ya kukuza kiwango changu, lakini ajabu ni kwamba baada ya hapo nilitupwa benchi tena. Hali ilibadilika kati ya uhusiano wangu na Louis na watu klabuni pale waliona – lakini mie nilishikilia maadili ya mchezaji wa kulipwa.

“Nilidhani kwamba baada ya kutoka likizo tungeanza vizuri kujijenga lakini niliporudi tu hapakuwapo tena mazingira sawa na sikupewa fursa ya kupigania namba kikosi cha kwanza. Hilo halikuwa wazo lake.

“Sikukasirika wala kuonesha hisia mbaya. Haya mambo yamo kwenye soka na ni sehemu ya maisha na mtu anatakiwa kutumia vizuri kadiri anavyoweza hali yoyote anayokuwamo nami nimefanya hivyo kwa kuondoka na kusonga mbele,” anasema Van Persie.

Amekaa United kwa misimu mitatu, ambapo alisajiliwa na Sir Alex Ferguson lakini baada ya msimu huo kocha aliyemuamini wangekaa muda mrefu akaondoka. Aliingia David Moyes aliyeboronga, timu ikaishia nafasi ya saba msimamo wa ligi, akafukuzwa akawapo kwa muda Ryan Giggs.

Kuingia Old Trafford kwa Mholanzi mwenzake kulimpa moyo na ilifika mahali ikadhaniwa ndiye angekuwa nahodha. Licha ya kuumia hapa na pale, alipochezeshwa hakuonekana kuwa na kiwango kikubwa na mara LVG akaanza kulalamika hana washambuliaji. Msimu uliopita RVP alifunga mabao tisa tu katika mechi 29.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Rais wa Fifa Februari 26

Man City: £60m kwa De Bruyne