in , , ,

Van Gaal awekwa mtu kati


*Wachezaji wamwambia mbinu zake mbovu

*Rooney, Carrick na Mata wampasulia ukweli

Ni mtafutano Old Trafford. Kocha Louis van Gaal amewekwa kati na
wachezaji waandamizi katika kikao kazi, wakamshambulia waziwazi,
wakimweleza kwamba mfumo wake ni mbovu ndiyo maana hawajashinda mechi
sita mfululizo.

Wachezaji waandamizi, wakiongozwa na nahodha Wayne Rooney, Michael
Carrick, Chris Smalling na Juan Mata walionekana kuzungumza zaidi,
wakimtaa bosi abadili njia zake, vinginevyo wanalo msimu huu.

Kikao hicho kimefanyika baada ya motto mwenye umri chini ya miaka 10
kuonekana akizungumza kwa ufasaha kwamba United wasifikiri kwamba soka
ya kumiliki mpira ni mali kitu, huku akisimulia walivyofundishwa soka
na Norwich wakalala 2-1 Old Trafford wikiendi hii.

Taarifa za ndani zinasema kwamba Mata na Ander Herrera wanaongoza uasi
wa Kihispania dhidi ya Mdachi huyo. Viungo hao wanapenda na washabiki,
lakini wanahisi wanakwazwa kwa mbinu za Van Gaal. Tangu Novemba 21
mwaka huu Man U hawajashinda mechi yoyote.

Mata amekuwa akichezeshwa mara kwa mara, lakini nje ya nafasi
anayoipenda na kumudu, wakati Herrera msimu huu amecheza mechi sita
tu. Van Gaal hajaeleza sababu japokuwa Herrera anaamini alitakiwa awe
kwenye kilele cha mafanikio na kupangwa mara kwa mara. Amechezea timu
za vijana za ngazi mbalimbali Hispania na sasa angetarajia apate namba
ya kudumu kwenye timu ya wakubwa, lakini Van Gaal anaelekea kuwa
kikwazo.

Baadhi ya nyota wa kimataifa wa Ulaya wana hofu kwamba hali mbaya ya
timu inaweza kuchangia wao kutupwa nje ya vikosi vya mataifa yao kwa
ajili ya Euro 2016. United ni wa kwanza katika Ligi Kuu ya England
(EPL) kwa kutoa pasi za nyuma โ€“ 1,553 wakati vinara wa ligi, Leicester
wamepiga 811 na West Bromwich Albion wana chache zaidi โ€“ 735.

Wachezaji wa United pia walieleza kutofurahishwa na mbinu za mazoezi,
aina a utawala wake wa kiimla na mbinu zake siku ya mechi. Van Gaal,
baada ya mechi hiyo na Norwich, amekiri kwamba anahofia hatima yake
klabuni hapo.

Tukirudi klabuni, wachezaji waliochangia mada kikaoni walionesha
wasiwasi wao kwamba hata orodha kubwa ya majeruhi tangu kuingia Van
Gaal inasababishwa na mazoezi kupita kiasi na kumtaka kuyapunguza.

Wachezaji na menejimenti walikubaliana kwamba washirikiane katika
jitihada mpya za kuirudisha timu kwenye โ€˜reliโ€™. Imebainika kwamba
baada ya Van Gaal kuona wachezaji wakitaka kumgeuka, alishauri pawepo
mazungumzo kati yao na menejimenti ili kurejesha ari ya timu
iliyopotea chini ya ukocha wake.

Van Gaal pia amezungumza na Makamu Mwenyekiti Mtendaji, Ed Woodward
wiki hii akitafuta kutatua baadhi ya matatizo klabuni hapo.

Pamekuwapo tetesi kwamba United wanaweza kumwajiri Jose Mourinho
aliyefukuzwa kazi Chelsea majuzi, ikidaiwa Mreno huyo ana hamu ya
kuingia Old Trafford ambako aliwania kutua 2013 baada ya kungโ€™atuka
kwa Sir Alex Ferguson.

Hata hivyo, inadaiwa kwamba palikuwapo mvutano miongoni mwa wakuu wa
klabu hiyo, juu ya kumchukua Mourinho aliyepata kuingia matatani
kutokana na matendo na kauli tata. Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger
amesema ni kumkosea heshima Van Gaal kuanza kujadili hatima yake
klabuni hapo, akisema anasikitishwa kila mtu anapopoteza kibarua
chake.

Inaelezwa kwamba United wanajiona ni klabu yenye msimamo na asili
fulani, hivyo wasingependa kucheza ngoma za Mreno huyo aliyepoteza
mechi tisa msimu huu na kufutwa kazi.

Woodward anaelezwa kuwa na imani bado na Van Gaal akiangalia mafanikio
ya alikotoa, japokuwa alikuwa nafasi ya tatu katika mpangilio wao wa
kutafuta mrithi wa David Moyes, akiwa nyuma ya machaguo yao, Pep
Guardiola na Diego Simeone wa Atletico Madrid ambao hawakupatikana.
Van Gaal amebakisha miezi 18 kwenye mkataba wake na sasa yumo katika
shinikizo, timu yake ikiwa imetupwa nje ya nne zilizo juu kwenye
msimamo wa ligi.

Van Gaal ameshakosa moja ya malengo yake msimu huu โ€“ kusonga hadi
hatua ya 16 bora kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) baada ya kupigwa
3-2 na Wolfsburg on Desemba 8 na kutupwa nje hadi katika Ligi ya
Europa.

Hata hivyo, lengo lake jingine la kumaliza ndani ya tatu bora ili
kufuzu moja kwa moja kuingia UCL bado linawezekana kufikiwa. United
wanashika nafasi ya tano nyuma ya Tottenham waliolingana pointi.
Watasafiri kucheza na Stoke Desemba 26 kabla ya kuwakaribisha vijana
wa Guus Hiddink โ€“ Chelsea siku mbili baadaye.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Sepp Blatter: Yametimia

Tanzania Sports

โ€˜Chelsea jitazameni kwenye kiooโ€™