in

LoveLove SurprisedSurprised

Utata wa sheria namba 11 ya soka Duniani

mchezo wa soka, mahasimu wakiwa uwanjani

Sheria namba 11 ya mchezo wa mpira wa miguu  inahusu maeneo ya kuotea, ligi ya Tanzania Bara imekuwa na tuhuma nyingi juu ya utekelezaji wa kanuni hii ndani ya mchezo wa soka.

Makosa ya waamuzi yapo tena ligi kuu ya England nayo waamuzi wake waliwahi kufanya kituko pale timu ya Wolverhampton Wanderers FC ilipofunga goli dhidi ya Manchester United na kuamuliwa kuwa kona, hii pia ilitokea bongo mchezo baina ya Yanga na Polisi Tanzania tukio likawa hivyo.

Utata huu inawezekana wanaopewa jukumu la kuzisimamia sheria 17 za mchezo wa soka yaani waamuzi wakawa wanafanya kusudi au hawana uelewa vizuri juu ya wanalolifanya.

Baada ya mechi mijadala mizito katika vituo mbalimbali hapa Tanzania inahusu mpira wa kuotea, hata hizo Yanga na Simba zimenufaika sana na mipira ya kuotea, wewe unadhani tatizo nini ?

Kwa utafati ambao nimeufanya waamuzi wasaidizi kwa hapa Tanzania ndio wamefanya vibaya zaidi kuliko wengine wote. Makosa waliyoyafanya makubwa sna na yamezigharimu timu nyingi, zikiwemo Namungo FC na Polisi Tanzania.

Kwa Tanzania waamuzi ambao wanasifika kuwa walifanya vizuri na wamestaafu kwa heshima kubwa ni pamoja na Omary Abdulkadir  na Athuman Kazi wa Kipyenga.

Licha ya hao wote kule England kwa nyakati za hivi karibuni alikuwepo Howard Webb japo alikuwa na udhaifu pindi Manchester United inapocheza anaonesha mapenzi pamoja na Mark  Clattenburg, lakini baba yao kwa ubora duniani kote ni Muitali Pierluigi Collina.

Baada ya kuona namna ambavyo wanayumba juu ya kusisimamia sheria 17 za mchezo wa soka basi nimeamua kuwakumbusha leo kuanzia sheria namba moja hadi mwisho.

1. Eneo la kuchezea, hii inasimama sheria namba moja katika zile 17 kwani huwezi kucheza bila ya kuwa na kiwanja kizuri kilichopimwa sawa sawa, nyasi zinaweza kuwa za asilia ‘Natural’ au zile za kutengenezwa ‘Artificial’ wengi hupenda kuita nyasi bandia ziwe za rangi ya kijani. Uwanja huo lazima uwe na umbo la mstatili, upana angalau ianzie  60 kwa 100 urefu.

2. Sheria namba mbili inahusu mpira wenyewe gonzi la ng’ombe, lazima uwe wa duara usiozidi inchi 28, ikiwa kwa watu wazima ila kwa watoto inatakiwa wapate saizi ndogo.

3. Namba ya wachezaji uwanjani, kila upande wanatakiwa wawe 11 akijumuishwa na goli kipa, endapo timu ikiwa na wachezaji saba uwanjani inaruhusiwa kucheza huku wachezaji wakubadilishwa wanatakiwa 3 japo kwa sasa wameongezwa watano kutokana na Corona japo haijawa sheria rasmi. Uzuri wa kanuni hii kipa anaweza kuabadilishwa na yoyote, yaani anaweza kutolewa kipa akaingia mchezaji kisha yule aliyekuwa ndani akaambiwa akadake na ikawa freshi.

4. Vifaa vya mchezaji, timu inatakiwa kuwa na aina yao ya jezi na mchezaji yoyote lazima avae jezi,soksi ambazo zinafika hadi magotini ziifiche ile ‘shin guard’ muamuzi anaouwezo wa kumtoa nje kama hajatimiza vigezo na masharti katika vifaa vyake.

5. Sheria namba tano inamuhusu muamuzi, huyu ndiye msimamizi mkuu uwanjani, maneno yake yanakuwa sheria, kama ukimsemesha sana anaweza akakuwajibisha kama mtovu wa nidhamu na akifanya hivyo basi anakuzawadia kadi  ya njano au nyekundu.

6. Muamuzi msaidizi inasimama namba sita kazi yake kubwa kumsaidia majukumu muamuzi wa kati, kazi yake kubwa kuangalia mpira kama umetoka nje ya uwanja,faulo, na kama mchezaji kaotea.

7. Namba saba inahusu muda wa mchezo, dakika 90 ndizo zinatumika kwa muda wa kawaida na ndani yake zimegawanywa katika vipindi viwili yaani dakika 45 za kipindi cha kwanza na zile za cha pili. Ila kama mchezo wa fainali unaweza kuamuliwa uchezwe kwa dakika 120 kama magoli hayajapatikana na kama huko pia hakuna mshindi basi matuta yatafuata.

8. Kuanza  kwa mechi,muamuzi anashika shilingi ili kuchagua timu ipi ianze, iliyoshinda kuanza inaweza kuchagua ianzie goli lipi na kipindi cha pili itaanza ile nyingine ambayo haijaanza kipindi cha kwanza.

9. Kuingia kwa mpira ndani yagoli au kutoka nje ya uwanja, hii sheria kule England mara nyingi wanatumia ‘goal technology’ ili kusaidia kujua kama mpira umeingia golini au haujaingia, kwa nchi zisizo endelea inakuwa mtihani mkubwa kama hakuna kifaa hiko. Hii ni sheria namba tisa ambayo inasema kuwa ili mpira uhesabike kama umeingia lazima upite eneo kubwa katika ule mstari ndipo linahesabika kama goli au ikiwa umetoka pembeni basio unakuwa wakurushwa au kona.

10. Sheria namba kumi namna ya ufungaji wa goli kama tulivyoeleza huko juu kuwa mpira lazima upite kwa ile goli line katika ‘frame’ ya goli mwisho wa mchezo timu iliyokuwa na magoli mengi ndio inahesabika kama mshindi na anaondoka na alama tatu au ubingwa.

11. Namba kumi na moja ni ile ambayo tumeanza kuielezea awali kuwa ni mpira wa kuotea ‘Off side’, mara nyingi mshambuliaji akiwa peke yake nyuma ya mabeki wa timu pinzani kisha mpira ukapigwa anayefuata hapo ni kipa hapo inakuwa ameotea. Inakuwa ngumu kidogo kuelewa na ndio maana waamuzi wengi wanapuyanga.

12. Sheria namba 12 inahusu madhambi ‘Foul’ hii imeelezewa sana  na zipo nyingi ila kwa uchache ni kwamba ikiwa umeushika mpira,umemkwatua mchezaji wa upinzani, umeserereka kutokea nyuma ya mcheaji hata kama umeuchukua mpira inakuwa afaulo yaani ‘Tackle from behind’ na nyingine nyingi.

13. ‘Free kick’ hii ni kanuni namba 13 inahusu upigaji wa mipira iliyokuwa inaweza ikawa ‘Direct au ‘indirect’ kuelekea goli ambako adhabu hiyo inaelekezwa.

14. Penati  hii inapigwa kama beki au mchezaji wa timu A amefanya faulo mchezaji B katika eneo la 18 la langoni mwake,au ameshika mpira ndani ya eneo hilo muamuzi ataamuru ipigwe penati au tunavyoita tuta.

15. Hii sasa inahusu kurusha mpira ndani ya uwanja  kuna utaratibu wake mchezaji anatakiwa aurushe kwa mikono miwili asiiname huku miguu yake ikiwa imekaa vizuri, kama hajafanya haya muamuzi anaweza kukataa na kumpa mchezaji wa timu pinzani arushe.

16. Goli kiki ‘Goal kick’ hii inafanywa tu kama mpira umetoka katika mstari wa goli upande wa timu pinzani mfano mchezaji aliyekuwa timu ya kaskazini ameupiga mpira umetokea huku katika goli la timu ya kusini upande wa kushoto au kulia hapo inahesabika kama ‘goal kick’.

17. Kitinda mimba katika sheria 17 za mchezo huu ni upigaji wa kona ‘Corner kick’ huwa wanapewa timu pinzani kam mabeki wa timu A wameutoa mpira katika mipaka ya uwanja upande wa goli lao. Mpigaji kona anaweza kufunga moja kwa moja kama Shiza Kichuya , au anaupiga ndani ili wagombanie.

Unaweza kutoa maoni yako hapo chini juu ya mjadala huu unadhani tatizo liko wapi hadi kufikia waamuzi wengi kushindwa kuchezesha katika misingi ya sheria 17 za mchezo wa mpira wa miguu.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

76 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Vikwazo kurejea EPL

Lilian thuram

LILIAN THURAM: