in , , ,

Ushindani mkubwa EPL

Ligi Kuu ya England (EPL) imemaliza mzunguko wa saba kukiwa na matokeo
ya kushangaza, huku timu zikizidi kujipanga kwenye nafasi ‘zao’.
Manchester City wa Pep Guardiola ambao walikuwa wakisonga kwa kasi kwa
kushinda mechi zao zote sita zilizotangulia, walikalishwa na Tottenham
Hotspur kwa kupigwa 2-0 White Hart Lane.

Wamebaki katika nafasi ya kwanza, lakini kushindwa huko ni kicheko kwa
timu nyingine zinazowania ubingwa, kwani walionekana kuwa na
mwendokasi mkubwa mno.

Wakiwa na pointi 18 sasa kuna tofauti ya pointi tano tu kati yao na
walio nafasi ya saba, ikionesha afya kiushindani.

Nafasi ya saba ni Chelsea wanaofundishwa na Antonio Conte, ambapo
msimu uliopita walimaliza katika nafasi ya 10 chini ya Jose Mourinho.
Wakati City wanazo pointi 18 wanapoenda kwenye mapumziko kupisha mechi
za kimataifa, Mauricio Pochettino wa Spurs anazo mbili pungufu,
akiweka hai matumaini ya kupigania ubingwa baada ya mwaka jana
kuanguka dakika za mwisho.

Arsenal ambao wameshinda mechi tano za EPL mfulizo sasa wana pointi 16
sawa na Liverpool, lakini wamewapita The Reds waliowatibulia vumbi
nyumbani kwao Emirates kwa kibano cha 4-3 siku ya kwanza ya msimu.
Everton walioanza ligi vyema wakifundishwa na kocha wa zamani wa
Southampton, Ronald Koeman wapo nafasi ya tano wakishuka kutokana na
matokeo ya jumla wikiendi hii.

Kama ilivyozoeleka, mkiani wamo Sunderland katika nafasi ya 20 nao
wakishuka na sasa wanazo pointi mbili tu. Stoke waliokuwa wakishika
mkia isivyo kawaida, sasa ni wa 19 wakiwa na pointi tat utu.

Imekuwa kawaida kwa misimu mingi Stoke kuwa katika nafasi za kati,
ambapo ni nadra kuhangaikia kutwaa ubingwa wala kujinasua kushuka
daraja lakini msimu huu mambo ni mazito kwa kocha Tony Pulis aliyeapa
hataachia ngazi.

Wengine walio katika eneo tete ni West Ham, ambao msimu jana walifanya
vyema sana chini ya kocha Bilic. Aidha ukiacha hao watatu walio chini
ya mstari mwekundu, kua Swansea, Middlesbrough na Hull juu yao kidogo,
mwenye pointi nyingi zaidi akiwa nazo saba sawa na Burnley.

Ligi hiyo inaendelea Oktoba 15 kwa Chelsea kuwakaribisha mabingwa
watetezi Leicester ambao hawapo vyema msimu huu. Vijana hao wa Claudio
Ranieri wanashika nafasi ya 12 na pointi zao nane.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Arsene Wenger atimiza miaka 20 Arsenal

Tanzania Sports

Man U wamekaa vibaya