in , , ,

Usajili na tetesi zake kutoka England:

*Falcao wa Chelsea
*Man City watoa £40 kumnasa Sterling
*Arsenal waingia kwenye mbio kumpata

Pazia la usajili limeanza kutumiwa vyema na wenye uwezo, ambapo Chelsea wanaelekea kumsajili mshambuliaji wa kati, Radamel Falcao aliyeshindwa kazi Manchester United.

Mchezaji huyo wa Monaco na Timu ya taifa ya Colombia anatarajiwa kupewa nafsi Stamford Bridge, ambako kocha Jose Mourinho ameahidi kumrejesha kwenye kiwango cha juu.

Raia mwenza wa Colombia, Juan Cuadrado anayekipiga Chelsea kwa msimu wa kwanza ‘amethibitisha’ kwamba rafiki yake, Falcao, anaenda Chelsea.

Wachezaji hao wawili wanatumikia taifa lao nchini Chile katika michuano ya Copa America. Falcao alikuwa kwa mkopo wa msimu mzima United, na tetesi ni kwamba hata Chelsea atakuwa kwa mkopo.
Cuadrado aliwaacha vinywa wazi wanahabari kwenye mkutano nao, ambapo alizungumza waziwazi habari za Falcao kujiunga na mabingwa hao wa England.

“Amejiunga nasi Chelsea. Ni muhimu kuwa na mwana timu kama yeye (Falcao) klabuni pale lakini kwa sasa najihusisha zaidi na Copa America,” akasema mchezaji huyo wa zamani wa Fiorentina huku akiahidi kuzungumzia suala hilo zaidi baadaye, kana kwamba yeye ni kocha, kiongozi au mmiliki wa Chelsea.

Kocha wa Timu ya taifa ya Colombia, Jose Pekerman aliyekuwa kando ya Cuadrado alimwambia: “Sema umefurahi … naamini kwa pamoja watasaidiana na kwa kweli watafanya mambo mazuri huko.”

Falcao anatarajiwa kuwagharimu Chelsea pauni milioni tatu kama ada ya usajili kwa mkopo na ikiwa watapendezwa naye watalipa pauni milioni 35 kumsajili moja kwa moja kiangazi cha mwaka kesho.

Falcao, 29, amekubali kupunguzwa mshahara kwa kiasi kutoka £260,000 kwa wiki alizokuwa akipata Monaco na Old Trafford hadi kwenye £200,000.

ARSENAL KUBAKI NA OXLADE, WAMUWANIA STERLING

Sterling : anaumiza vichwa vya Arsenal na Man City....
Sterling : anaumiza vichwa vya Arsenal na Man City….

Wakati Manchester City wakitoa dau jingine kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji wa Liverpool, Raheem Sterling, Arsenal wanajiandaa kuwapiga kumbo.

Sterling aliyeuza nyumba yake Liverpool na kutafuta nyingine London hataki kubaki Anfield na City wanadaiwa kutoa ofa ya pauni zaidi ya milioni 40.

City pia wanaendelea na mipango ya kumsajili kiungo wa Juventus, Paul Pogba, 22, anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 60.
Nako wanapata ushindani, kwani Barcelona tayari wameanza mazungumzo na Juve juu ya mchezaji huyo, na mgombea urais wa huko ameahidi wapiga kura kwamba atamsajili Mfaransa huyo.

Man City wakimkosa Pogba, basi kocha wao, Manuel Pellegrini atamgeukia kiungo wa Aston Villa, Fabian Delph, 25.

Arsenal wamekataa mpango wa Chelsea wa kutaka wamtoe kiungo wao, Alex Oxlade-Chamberlain, 21, ili nao wawaachie kipa wao mkongwe, Petr Cech, 33.

The Gunners wanaona kwamba hakuna haja ya kufanya mabadilishano hayo, na wapo tayari kuzungumza biashara ya kwenye pauni milioni 10 ili kumchukua kipa huyo.

Hata hivyo kuna msiri aliyesema kwamba si ajabu Cech akawasili Emirates wiki ijayo, kwa sabau ndiko anakotaka kwenda, lakini Mourinho hangependa, maana ni washindani wao.

Chelsea wameanza kujiandaa kwa maisha bila Cech, na wamemgeukia kipa wa Stoke, Asmir Begovic, 27 ili awe chaguo la pili baada ya Thibaut Courtois klabuni hapo.

Kipa wa Manchester United, David De Gea, 24, anaelekea kuwa na uhakika wa kuondoka na kujiunga na Real Madrid, lakini Iker Casillas, 34, amesema kwamba bado hajakubali kuachia nafasi yake langoni kama chaguo la kwanza.

Tottenham Hotspur wamedhamiria kuhakikisha kipa wao, Hugo Lloris, 28, anabaki White Hart Lane, lakini watakuwa na wakati mgumu iwapo Man United watatoa pauni milioni 25 kwa ajili ya kumchukua.

Kadhalika, United wanakabiliana na upinzani kutoka Real Madrid juu ya kumsajili mlinzi Nicolas Otamendi, 27, wa Valencia anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 35.

Bosi mpya wa Madrid, Rafael Benitez angependa sana kumwona raia huyo wa Argentina akivaa uzi mweupe hapo Santiago Bernabeu.
Kwingineko, West Ham na West Bromwich Albion wanashindana kumsajili mshambuliaji wa kati wa Senegal, Demba Ba, 30.

Ba anataka kuondoka Besiktas ya Uturuki kwa sababu kuna kutokukubaliana katika masuala ya fedha.

Queen Park Rangers (QPR) wamewaonya Chelsea, Liverpool na Newcastle kamba itawabidi watoe pauni milioni 15 ili kumpata mpachika mabao wao, Charlie Austin, 25.

West Ham pia wanazitaka huduma za mfungaji huyo bora wa QPR msimu uliopita.

Inter Milan wamekataa ofay a Liverpool ya kutaka kumsajili kiungo Mateo Kovacic, 21, katika dili ambalo Liver wangewapatia Milan mshambuliaji wa kati, Mario Balotelli, 24, kama daraja.

Southampton na Sunderland wanalenga kumsajili kwa mkopo beki wa pembeni wa Arsenal, Carl Jenkinson, 23, ambaye msimu uliopita alikuwa West Ham.

Wakati Southampton wanamhitaji ili kuziba pengo linalonukia la beki wake wa kulia, Nathaniel Clyne, 24 anayehusishwa na Liverpool na Manchester United.

Hata hivyo, West Ham nao wana nia ya kuhuisha usajili kwa mkopo wa Mwingereza huyo. Zipo taarifa kwamba Sunderland wanaelekea kukubaliana dili la pauni milioni mbili na Arsenal.

Bosi wa Aston Villa, Tim Sherwood anataka kumsajili kiungo wa Hull walioshuka daraja, Tom Huddlestone, 28, na winga Robbie Brady, 23.
Everton bado wanataka kumsajili winga wa Spurs, Aaron Lennon, licha ya kukaribia makubaliano na Barcelona kwa ajili ya kumchukua tena Gerard Deulofeu, 21.

Swansea wanataka kumsajili winga wa zamani wa Liverpool, Ryan Babel, 28, katika dili la pauni milioni mbili kutoka klabu ya Uturuki ya Kasimpasa. Babel alikaa Anfield kwa miaka minne kati ya 2007 na 2011.

West Brom wamekubaliana ada ya pauni milioni 1.5 na Wigan kwa ajili ya kumsajili winga wao, James McClean, 26.
Newcastle wanadai pauni milioni 10 kwa ajili ya kumwachia mshambuliaji wake mwenye umri wa miaka 30, Papiss Cisse.
Kipaumbele chao katika usajili ni mshambuliaji wa West Brom, Saido Berahino, 21.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Ratiba Ligi Kuu England yatolewa 2015/16

Stars wanahitaji upasuaji