in , , ,

Usajili EPL wafikia £500m

 

 

Zikiwa zimebaki karibu wiki nne kukamilika kwa usajili kwa Ligi Kuu ya England (EPL), klabu zimetumia pauni milioni 500 hadi sasa, zikiwa ni pauni milioni 335 pungufu ya zile za msimu uliopita.

 

Hii inatokana na baadhi ya klabu kutofanya biashara hiyo hadi sasa, kutoa ofa ndogo au klabu zenye wachezaji wanaotakiwa kuwang’ang’ania.

 

Hadi sasa dili la Raheem Sterling kwenda Manchester City kutoka Liverpool kwa pauni milioni 49 ndilo kubwa zaidi.

 

Hata hivyo, kocha wa Manchester United, Louis van Gaal amedokeza kwamba atafanya usajili wa kushangaza muda wowote, licha ya kuwa moja ya klabu zilizotumia fedha nyingi zaidi, pauni milioni 83, hadi sasa kwenye usajili.

 

Mtaalamu wa masuala ya fedha, Rob Wilson amekaririwa akisema kwamba madhali muda badoupo kuna uwezekano mkubwa wa klabu kusajili zaidi, kwa sababu pia zitafaidika na mkataba mnono zilioingia na vituo vya televisheni.

 

Kuanzia msimu wa 2016/17 dili za haki za televisheni kwa klabu litaongezeka kutoka pauni bilioni 3.01 hadi pauni bilioni 5.136. Dirisha hili kubwa la usajili linatarajiwa kufungwa Septemba mosi saa 12 jioni kwa saa za Uingereza.

 

Klabu ya chini zaidi itapata pauni milioni 99 kwa msimu wakati mabingwa watazoa pauni milioni 150 zikiwa ni zawadi hata kabla ya fedha za ziada kutolewa kwa mechi kutokea kwenye televisheni.

 

Kampuni ya uchambuzi ya masuala ya Deloitte inasema kwamba kiwango cha pauni milioni 500 kilifikiwa Ijumaa iliyopita.

 

Wakati United wanasubiriwa kutangaza mchezaji watakayemsajili hivi karibuni, Chelsea wanamtaka John Stones wa Everton kwa pauni milioni 30 huku Manchester City wakisubiriwa kumwaga karibu pauni milioni 60 kumpata mchezaji wa Wolfsburg, Kevin De Bruyne, dili zitakazoongeza kwa kiasi kikubwa matumizi ya klabu kwenye usajili.

 

Kwa ujumla, msimu wa 2014/15 ulishuhudia pauni milioni 965 zikitumiwa katika dirisha la msimu wa kiangazi na lile dogo la Januari  na Wilson ambaye ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sheffield Hallam anaamini kiwango hicho kitavukwa kadiri msimu utakavyokuwa unavyoendelea.

 

Anasema kwamba kuingia pia kwa BT kwenye udhamini wa Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) kumezichochea klabu kufanya usajili wa nguvu zaidi ili zivuke kwenda kushindana na nyingine za Ulaya. BT imepanga kutumia pauni milioni 897 katika udhamini wake.

 

Kuna taarifa kwamba klabu itakayofika hatua ya makundi UCL itajipatia mgawo wa pauni milioni tisa wakati mabingwa watalipwa pauni milioni 70. Hata hivyo, klabu zinajizuia kusajli kwa pupa ili kulandana na matakwa ya uungwana katika matumizi ya fedha.

 

Mamchester United wametumia pauni milioni 83 tu kiangazi hili wakati kwa mchezaji mmoja tu, Angel Di Maria kiangazi kilichopita walimwaga pauni milioni 59.7 na kuvunja rekodi ya Uingereza.

 

Mchezaji huyo anaelekea Paris Saint-Germain (PSG) kwa kima kinachokadiriwa kutofika pauni milioni 45.

 

Liverpool wametumia pauni milioni 73 hadi sasa, kati ya hizo pauni milioni 32.5 kumsajili Christian Benteke kutoka Aston Villa, pauni milioni 29 kwa ajili ya Roberto Firmino kutoka Hoffeinheim, pauni milioni 3.5 kwa Joe Gomez kutoka Charlton na pauni milioni 12.5 kwa Nathaniel Clyne aliyekuwa Southampton.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Di Maria aelekea PSG

Messi amkwida mchezaji