EPL imekuja kivingine.

Bodi ya Ligi Kuu ya England (EPL) imeonesha umwamba dhidi ya wadhamini na watangazaji wa michuano hiyo mikubwa hapa – BT Sport and Sky Sports.

Wakati klabu zikinyenyekea ili kampuni hizo zisisitishe malipo kutokana na haki ya matangazo na mechi zilizosalia kwa msimu huu kwa kuwa hatima yake haijulikani, EPL imekuja kivingine.

Bodi hiyo imewazuia Bt Sport na Sky Sports kuhiji lolote juu ya lini msimu utarejea tena kwa mechi zilizosalia kuchezwa, ili bingwa kupatikana na wa kushuka au kupanda daraja kujulikana vile vile.

Wametakiwa kuwa makini na kufuata sheria, kanuni, miongozo na mikataba waliyofikia awali, na kwamba hatua kali zitachukuliwa iwapo watajaribu kuwafikia na kuzungumza na makocha au wachezaji wa ligi hiyo.

Ligi Kuu ya England imesimamishwa kwa muda usiojulikana kwa sababu ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa homa kali ya mapafu maarufu kama Covid-19. Kwa msingi wa msimamo uliotolewa na EPL, ni kwamba maswali na masuala yote yanayohusiana na athari za virusi hivyo kwa ligi yamepigwa marufuku kwa wawili hao.

Sky, wamelipa kima cha £1.19bilioni kwa haki za matangazo ya mechi msimu huu wakati BT wametoa jumla ya £325 milioni. Klabu zilikuwa zimeshakunbali kutoa makocha wao kwa ajili ya mahojiano na vituo hivyo kila baada ya wiki nne na mchezaji mmoja kila baada ya wiki mbili, wakati huu ambapo watangazaji hao wakiwa na kiu ya kuendelea na matangazo yanayohusiana na michezo msimu ukiwa umezimwa kwa muda.

Tayari Sky wamesema kwamba hawatadau kurejeshewa fedha zao kutokana na masharti na vigezo juu ya kufanyika kwa mechi na kurushwa kote duniani kutofikiwa ipasavyo. Barua pepe imetumwa kwa watangazaji hao wawili ikiwaonya kuwa makini na kwenda kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa wakati wa majadiliano wiki jana

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Harry Kane Madrid?

Tanzania Sports

Italia kupima wanasoka