in , ,

UKOMAVU WA MANCHESTER UNITED ULIWAPA USHINDI.

Mauricio Roberto Pochettino ameonesha dhahiri anaweza kutumia mabeki wanne na
watatu katika msimu mmoja na timu ikacheza vizuri.

Pamoja na kwamba Tottenham Hotspurs ilifanikiwa kumiliki mpira kwa
asilimia kubwa kuliko Manchester United, kuna kitu ambacho ilikosa na
Manchester United walikuwa nacho.

Kitu hicho ni ukomavu.

Manchester United walionesha ukomavu ambao uliwasaidia kuwapa ushindi
dhidi ya Tottenham Hotspurs.

Katika mechi hii Tottenham Hotspurs walifanikiwa kushinda mpira (
kumiliki mpira) lakini wakashindwa kushinda mchezo.

Hiki ndicho ambacho kiliwatofautisha kwa kiasi kikubwa na Manchester
United, ambao wao kwa kiasi kikubwa walifanikiwa kushinda mechi, kwao
kuanzia mwanzo wa mchezo walikuwa wanawaza namna bora ya kushinda
mchezo kuliko kushinda mpira.

Kuanza kwa Sissoko kulikuwa na msaada kwa Tottenham hotspurs?

Kuna kitu ambacho alikosa Sissoko ( match sharpness) , kitu ambacho
kilikuwa kinamfanya wakati mwingine kutotimiza baadhi ya majukumu.

Mfano, Sissoko alipangwa acheze kama box to box Midfielder, ambapo
alikuwa na jukumu la kukaba na kushambulia akitokea katikati ya
uwanja, jukumu ambalo alilifanya kwa kiasi kikubwa ni la yeye kuwa ana
shambulia, lakini kwa kiasi kikubwa alikuwa anachelewa kurudi nyuma
kumsaidia Winks.

Hali ambayo ilikuwa inamlazimu Erricksen kuwa anarudi katikati kuziba
nafasi ambazo Sissoko alizokuwa anaacha.

Hii iliwagharimu Tottenham Hotspurs kwa sababu kwa Erricksen kutumia
muda mwingi eneo la katikati lilimfanya awe na ufinyu wa kutengeneza
nafasi nyingi, ikizingatia hata Sissoko wakati anapanda mbele hakuwa
anatengeneza sana nafasi.

Hivo Tottenham Hotspurs ilionekana kuwa inamiliki mpira tu bila
kutengeneza nafasi nyingi za wazi. Ndiyo maana kipindi kile cha kwanza
ambapo walifanikiwa kuwamiliki Manchester United, pamoja na kuwamiliki
lakini hawakuwa na uwezo wa kutengeneza nafasi nyingi za wazi zaidi ya
kupiga pasi nyingi.

Pengo la Harry Kane lilionekana?

Hapana shaka ni mchezaji muhimu na alihitajika katika mechi hii.

Mfungaji bora wa timu mpaka sasa. Uwepo wake ulikuwa na umuhimu mkubwa sana.

Kasi ya Son ilikuwa inawafanya mabeki wa Manchester United kukabia
katika eneo lao, na kasi hii ya Son ilikuwa inaleta uwazi katika eneo
la nyuma la Manchester United.

Alihitahitajika mtu ambaye angeweza kutumia uwazi ambao ƴulikuwa
unaachwa , na mtu huyo ni Harry Kane.

Son, hafungi sana kama Harry Kane na hatoi pasi za mwisho nyingi kama
Erricksen lakini kasi yake ni muhimu sana kuifanya safu ya ulinzi ya
timu yoyote kulazimika kukaba katika eneo lao na wakati mwingine
kuacha uwazi kati ya safu ya ulinzi, kasi ya Son haiwezi kuwa na
msaada wowote ule kama hakuna mshambuliaji atakayetumia
kinachozalishwa na Son.

Dier alistahili kuanza mechi ya leo?

Kosa lake la kutokuwa makini kumzuia Antony Martial aliyetoka nyuma
yake kwa kasi na kufanikiwa kufunga goli la ushindi, haliwezi
kusababisha mazuri yake yasionekane kwa kiasi kikubwa.

Dier alikuwa mtulivu kwenye mechi hii, na amri ya timu kusogea mbele
na mpira ilikuwa inaanza kwake, yeye ndiye aliyekuwa anapiga pasi za
kuanzisha mashambulizi. Pili alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwa
mtulivu kuwazuia Rashford na Lukaku , lakini kapungukiwa kasi tu
ambayo ndiyo iliyosababisha Manchester United kupata ushindi.

Ni wakati sahihi wa Jose Mourinho kumwamini Antony Martial?
Amekuwa akionesha mchango wa moja kwa moja kila anapotokea benchi.

Mara nyingi anapokuwa anaanza, mchango wake wa moja kwa moja ( kufunga
goli na kutoa pasi za mwisho za goli) unakuwa hauonekani.

Ili kuikamata imani ya Jose Mourinho anatakiwa amuoneshe yeye ni
mchezaji ambaye anaweza kuisaidia timu katika vipindi vyote.

Ni ukweli uliowazi kuwa Pogba ameenda na magoli ya Lukaku pamoja na
pasi za mwisho za magoli za Henrik Mkhitaryan.

Henrik Mkhitaryan na Lukaku wanakosa huduma ya Pogba ambayo wao
ilikuwa inawafanya kuwa huru zaidi.

Mfano, Henrik Mkhitaryan akiwa anacheza na Pogba kwa kiasi kikubwa
huwa anakuwa karibu sana na box la mpinzani (nyuma ya Lukaku) ambapo
ndipo hutoa huduma nzuri kwa Lukaku , lakini kutokuwepo kwa Pogba
kunamlazimu Henrik Mkhitaryan kuwa anasogea chini zaidi kuchukua
mpira kitu ambacho kinapunguza ufanisi wake wa kazi.

Mourinho anatakiwa aamini katika kutumia mabeki watatu kuliko mabeki
wanne, Smalling alicheza vyema sana na kuonekana kuwa kiongozi mzuri
sana mbele ya wenzake.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

AJIB, KIFUNUE NA UKISOME KITABU CHA RONALDO

Tanzania Sports

MANULA ALIWAWEKA HAI SIMBA, HUKU YANGA WAKIKOSA UMAKINI