in ,

UKISHANGAA YA DITRAM NCHIMBI UTAYAONA YA FREDDY ADDU

DITRAM NCHIMBI

Hivi karibuni kuliibuka mjadala ndani ya mitandao ya kijamii katika nchi ya Tanzania juu ya kiwango cha mchezaji wa timu ya Yanga Ditram Nchimbi kwamba kiwango chake ni kibovu. Baadhi ya wadau wakafikia hatua ya kusema kwamba katika usajili mbovu ambao timu hiyo imewahi kufanya katika miaka ya hivi karibuni basi huyo ni mfano hai kabisa. 

Ditram Nchimbi aliibukia katika kikosi cha timu ya Polisi Tanzania na baada ya mda akasajiliwa katika kikosi cha wababe hao wa mitaa ya jangwani Kariakoo. Mashabiki na wadau wa kilabu hicho cha jangwani walikuwa wana matumaini makubwa sana kwa mchezaji huyo na kwamba angeleta mageuzi makubwa sana katika kilabu hicho na angekuwa ni mwarobaini wa mabao kwani wengi wao walitegemea kwamba angekuwa ni mchezaji wa kuwaletea magoli 20 na zaidi kwa msimu mmoja.

Wanaomshangaa Nchimbi kukaa mda mrefu bila ya kufunga bao basi wasimshangae sana. Kuna mtu mmoja anacheza mpira nchini Sweden anaitwa Freddy Adu huyu mtu hakuna ambaye angetegemea kwamba kwa sasa angekuwa anacheza timu tena ya madaraja ya chini huko Sweden. Huyu ana historia yake ambayo mpaka kwa sasa haijavunjwa. Huyu alipofikisha umri wa miaka 14 alisajiliwa na timu ya DC UNITED inayoshiriki katika ligi kuu nchini Marekani. Aliushangaza ulimwengu kwa soka lake safi na kipaji cha hali ya juu alichokuwa nacho. Alipewa mkataba ambao akaaanza kulipwa kwa kiwango sawa na mastaa wa mpira katika ligi hiyo.

Tanzania Sports
freddy adu

Kijana huyo alipachikwa jina la pele mpya akifananishwa na mcheza gwiji wa soka nchini Brazil Edson Nascimento maarufu kama Pele. Adu alipata heshima na hadhi kubwa sana ya kufananishwa na gwiji huyo. Ilifika nyakati mpaka gwiji huyo alikuwa anakutanishwa na motto huyo katika miaka hiyo.

Adu alianza kupewa mikataba ya matangazo makubwa na bodi ya ligi ya nchi hiyo ikaanza kumtangaza kwamba yeye ndiye nembo ya soka katika nchi hiyo. Ghafla vyombo vya habari navyo vikawa havikauki kwake na kuanza kumwomba mahojiano(interview) naye. Kwa kifupi kijana huyo akawa hakauki kwenye runinga nchini marekani. Hakukaa sana timu za ulaya zikaanza kummezea mate na kuanza kutuma maombi ya kuomba huduma zake. Hakukaa sana akapata mkataba mnono na kilabu cha Real Salt Lake ambacho nacho hakukaa sana. Mwenyezi mungu si athumani akasajiliwa na mabingwa wa kihistoria wa nchi ya ureno yaani nawazungumzia timu ya Benfica. Katika timu ya Benfica ambayo ni kama chuo cha soka kwani imekuwa inasifika kwa kulea wachezaji wengi ambao baadaye huwa wanakuja kuwa wachezaji mahiri duniani basi ndugu Adu allikaa pale na kufundishwa soka pale. Katika umri mdogo alikaa pale kwa jumla ya miaka 4 yaani hiyo ni kuanzia mwaka 2007 mpaka 2011. Huwezi kuamini katika miaka yote minne aliyocheza hapo benfica alicheza jumla ya mechi ya 11.

Akiwa Benfica  kuna wakati aliuzwa kwa mkopo kwenda timu ya wababe wa ufaransa Monaco. Ndani ya Monaco hakuna la maana alilofanya katika kipindi alichokuwa kwenye mkopo ndani ya timu hiyo. Monaco wakaona hawana namna zaidi ya kuachana naye. Katika mahojiano ambayo aliyafanya hivi karibuni anasema kwamba katika makosa aliyowahi kuyafanya ni kutokujituma wakati anachezea timu ya benfica kwani katika nyakati yeye anachukuliwa kwenye kikosi hicho ndio nyakati hizo hizo alisajiliwa winga mtaalamu wa soka toka nchini Argentina yaani hapa namzungumzia Angel Di Maria. Di Maria alijituma kwa kiwango kikubwa na hatimaye kufanikiwa kushawishi klabu kubwa ya nchini Hispania yaani Real Madrid kumsajili kwenye kikosi chao. Adu amejikuta ndani ya miaka ambayo amecheza mpira anahama toka timu mmoja kwenda nyingine na hatimaye kujikuta yuko Sweden. Katika mda aliocheza mpira amejikuta amechezea jumla ya vilabu 15 vya soka la kulipwa. Mwenyewe anaamini kwamba vyombo vya habari ndivyo vilivyomharibu kwani vilimpa jina kubwa sana na hatimaye kumfanya ashindwe kupata utulivu katika kucheza soka kwani vilimpa “kiki” kubwa sana katika umri mdogo.

Binafsi naamini huo sio mwisho wa Nchimbi anachotakiwa akae ajitathmini na kujaribu kutambua tatizo alilonalo na kisha baada ya kulitambua basi atafute namna ya kulitatua ili asiharibu kipaji chake alichokuwa nacho.

Report

Written by Kahema Fimbo

Mwandishi wa habari wa kujitegemea mwenye uzoefu wa kuandika kuhusu habari za michezo anayeishi Dar es salaam Tanzania. Ana uzoefu wa miaka 2 wa kufanya kuandika na kasha kuchapisha Makala zake katika mitandao kadhaa nchini Tanzania. Ni mpenzi na pia ni mdau wa michezo. Amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi kwenye vyama vya michezo nchini Tanzania ikiwemo katibu mkuu taifa chama cha mchezo wa kabaddi Tanzania (Tanzania kabaddi sport association), mwenyekiti kamati ya habari chama cha shule za michezo Tanzania (Tanzania sport centres and academies association- TASCA) na pia makamu mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya mkuranga( Mkuranga district football association- MDFA).
Nje ya michezo ni mwanajamii na amewahi kujitolea na pia kuwa kiongozi katika taasisi mbalimbali nchini Tanzania za vijana kam vile YOA, TYVA, YUNA, na kadhalika.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
JPM

Magufuli ameng’arisha sekta ya michezo

Nuno Espírito Santo

TUTENGENEZE AKINA MOURINHO NA NUNO SANTO WETU!