Ufaransa wawacharukia Uswisi

*Wawachabanga 5-2

Timu ya Taifa ya Ufaransa imeonesha dhamiri ya kufanya vyema kwenye michuano hii kwa kuwachakaza Uswisi 5-2.

Ufaransa ambao mwaka 2010 hawakushinda hata mechi moja na kutolewa kwenye hatua ya mwanzo, walionesha mchezo mzuri, wakiutawala hasa kipindi cha kwanza na mwanzoni mwa kipindi cha pili.

Ufaransa walipata mabao yao kupitia wa Olivier Giroud, Blaise Matuidi, Mousa Sissoko, Karim Benzema na Mathieu Valbuena.

Uswisi walikumbuka shuka kukiwa kumekucha, ambapo walipata mabao yao mawili dakika ya 81 kupitia kwa blerim Dzemaili na dakika ya 87 kwa bao la Granit Xhaka. Benzema alikosa penati baada ya kuchezewa rafu, mkwaju ambao uliokolewa na kipa.

Comments