in , , ,

UCHAMBUZI WA MECHI MBALIMBALI WEEKEND HII

José Mourinho, centre, looks on as Manchester United threw away a 2-1 lead to 10-man Leicester in injury-time.

ARSENAL vs LIVERPOOL.

Arsenal katika mechi hii walitumia mfumo wa 4-3-2-1 wakati Liverpool
walianza na mfumo wa 4-3-3, ila walikuwa wanabadirika kulingana na
wakati, kuna kipindi walicheza 4-3-2-1 na kuna wakati wakacheza 5-3-2.

Mohamed Salah, akifurahia bao lake dhidi ya Arsenal

Liverpool walianza vizuri katika kipindi cha kwanza kwa kumiliki
mpira, na kukaba kwa nguvu hali ambayo iliwafanya Arsenal wafanye
makosa binafsi ambayo yaliwafanya wasipate nafasi ya kushambulia kama
Liverpool.

Wakati Liverpool walipokuwa wanacheza mfumo wa 4-3-3, Roberto Firmino
alikuwa anashuka chini katikati.

Hali ambayo ilisababisha Nacho Monreal kushuka naye chini katikati,
alikuwa anafanya man to man marking.

Nacho Monreal alipokuwa anashuka chini, nyuma alikuwa anaacha nafasi,
nafasi ambazo zilikuwa zinawafanya kina Countinho, Mane na Salah
kuzitumia, hata goli la kwanza lilitokana na Countinho kuwa peke yake
akitumia nafasi iliyoachwa wazi na Nacho Monreal aliyekuwa ameshuka
chini kumkaba Roberto Firmino.

Goli la pili lilitokana na Firmino pia kushuka chini katikati na
mabeki wa Arsenal kumfuata na kuacha nafasi wazi ambayo ilitumiwa na
Mohamed Salah kufunga goli.

Mabadiriko ya kutoka Hernderson na kuingia James Milner kulikuwa na
faida kubwa kwa Liverpool kwenye suala la kujizuia na kushambulia.

Liverpool walijua beki wake wa kulia Hector Bellerin anapanda sana
kushambulia , hivo James Milner alikuwa anakuja upande wa kushoto mwa
Liverpool kumsaidia Robertson , hali ambayo ilipunguza nguvu kwa
Hector Bellerin.

Liverpool mabeki wake hawakuwa na marking nzuri kwa sababu walikuwa
wanawaacha peke yao washambuliaji wa Arsenal. Mfano goli la kwanza la
Arsenal ambapo Sanchez alikuwa peke yake kabla na baada ya kupokea
mpira.

Arsenal walifanikiwa kurudi kwenye mchezo na kufanikiwa kufunga goli tatu.

Liverpool walirudi katika mfumo wa 4-3-2-1 ambapo Firmino alibaki peke
yake mbele na kunyimwa uhuru wa yeye kushuka chini katikati.

Baada ya kuona Arsenal anaongoza goli tatu , Klopp alibadirika haraka
na kurudi katika mfumo wa 4-3-3 ambapo Firmino alirudi katika majukumu
yake ya awali, na timu ikasawazisha. Baada ya kusawazisha Liverpool
walibali mfumo na kwenda katika mfumo wa 5-3-2 ambapo waliongeza watu
katika eneo la kujilinda na mbele wakabaki Salah na Firmino.

EVERTON vs CHELSEA.

moja kati ya hatari langoni kwa Everton

Sam Allardyce amefikisha michezo 6 bila kufungwa na akiwa na clean
sheets nne, huku akishinda michezo minne na kutoka sare michezo miwili

Phil Jagielka na Micheal Keane walifanikiwa kutengeneza ukuta imara wa ulinzi.

Pamoja na kwamba Phil Jagielka ilikuwa mechi yake ya kwanza hakuonesha
kukosa sharp nzuri kwenye timu.

Antonio Conte aliamua kumtumia Hazard kama false 9, lakini akawa
ameangushwa na kutokuwepo na kiungo ambaye anatengeneza nafasi nyingi
za magoli.

Hivo hata wakati Hazard anashuka chini katikati, na kina Pedro na
Willian wakitokea pembeni kuja eneo la box la Everton hawakuwa na
nafasi ya kupata mipira mizuri kutoka katikati kwa viungo

Sam Allardayce alihakikisha timu yake iwe na ugumu katika ukabaji.

Alitumia mfumo wa 4-1-4-1 ambapi ulimfanya Dominic Calvert-Lewin kuwa
mshambuliaji peke yake kule mbele, ambapo Rooney hakuwepo.

Sam Allardayce alifanya mabarikio ya kiufundi ambapo alimwingiza
Williams kuchukua nafasi ya Tom Davies na kutengeneza idadi ya mabeki
watatu nyuma, na Aaron Lenon nafasi yake kuchukulia na Sandro Ramirez

LEICESTER CITY vs MANCHESTER UNITED.

Harry Maguire

Timu zote katika makaratasi zilikuwa zimeingia na mfumo wa 4-5-1 ,
lakini hii ilikuwa tofauti kwa Manchester United walipokuwa
wanashambulia ambapo walikuwa wanabadirika kwenda 4-3-3 .

Leicester City walitumia muda mwingi kukaa nyuma na kushambulia kwa kushtukiza.

Goli la kwanza la Leicester City , wachezaji wa Manchester United
walikuwa mbele , upande wa kushoto Ashley Young alikuwa amepanda
kusaidia mashambulizi.

Kitu ambacho kilimpa nafasi Mahrez kuwa peke yake na kuanzisha
shambulizi ambalo lilizaa goli la kwanza.

Wachezaji wengi wa Manchester United walionekana kukosa umakini pale
walipokuwa wanapata nafasi.

Lingard, Rashford na Martial walipata nafasi za wazi lakini
wakashindwa kuzitumia ipasavyo.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

ARSENE WENGER ATAENDELEA KUWA MNYONGE KWA JURGEN KLOPP?

Tanzania Sports

HIKI NDICHO KINACHOISIBU MANCHESTER UNITED.