in

Ubovu wa viwanja vya michezo unajirudia nchini..

Tangu kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzanua Bara 2020/2021 jumla ya viwanja  vitano vya soka vimefungiwa kutumika kwenye mashindano ya Ligi hiyo kutokana na  kasoor mbalimbali. Inafahamika kuwa mchezo wa soka ni biashara na burudani. Katika  biashara kuna faida na hasara, na burudani pia inazo faida na hasara zake.  

Viwanja vingi vya mchezo wa soka vimekuwa na hali ya inayofanana kwa miaka mingi  sasa. Hali ya viwanja hivyo imechangia kuwa sababu za kufungiwa mara kwa mara. Hata  hivyo matatizo yanaelekea kujirudia rudia na kusababisha adhabu kutolewa kwa  viwanja vile vile ambavyo vinalalamikiwa na wadau wa soka. Je kwanini hali hiyo  imekuwa ikijirudia? 

Mara kadhaa tumearifiwa juu ya ubovu wa viwanja wa mpra wa Kikapu au mpira wa  pete. Hata hivyo uchunguzi unaonesha suala hilo limekuwa sugu sasa. Je, ni kwanini  hali iwe hivyo? Hayo ndilo swali la kupatiwa majibu kwa maslahi ya maendeleo ya  michezo. 

Kwa mfano, hivi karibuni Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara imefungia viwanja  mbalimbali vya soka. Bodi hiyo ilieleza kuwa uchakavu katika maeneo ya  kuchezea,ulinzi na vigezo vyote muhimu kulingana na shirikisho la Soka nchini TFF,  Afrika na FIFA.  

Viwanja hivyo vimefungiwa kutumika katika mashindano kutokana na kukosa baadhi  ya sifa za kikanuni kama zilivyoainishwa kwenye Kanuni ya 7 inayozungumzia Uwanja  na sheria namba moja ya mpira wa miguu inayozungumzia hadhi ya uwanja wa  kucheza katika mashindano ya mpira wa miguu.  

Kutokana na uamuzi huo Bodi ya Ligi iliamuru timu ya Polisi Tanzania kutumia uwanja  wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini Arusha kwa ajili ya mechi zake za nyumbani katika  mashindano ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Uamuzi huo unaenda sambamba na Kamati ya  Leseni kufanya ukaguzi wa viwanja vyote vinavyotakiwa kutumika kwenye mashindano  ya Ligi. 

Baadhi ya viwanja vilivyokumbana na rungu la Bodi; Septemba 11, mwaka huu wa 2020  Bodi ya Ligi Kuu ilifungia uwanja wa Gwambina mkoani Geita kuchezwa mechi zozote  za mashindano kutokana na eneo lake la kuchezea kutokidhi viwango vinavyoainishwa.  Kutokana na uamuzi huo, Gwambina walishauriwa kutumia uwanja wa Nyamagana au  CCM Kirumba vya jijini Mwanza kwa ajili ya mechi zake za nyumbani. 

Septemba 13 mwaka huu wa 2020 uwanja wa Karume uliopo mkoani Mara na ambao  umekuwa ukitumiwa na timu ya Biashara United kama uwanja wake wa nyumbani 

ulifungiwa kutokana na eneo lake la kuchezea na vyumba vya kubadilishia nguo  kutokidhi viwango vilivyoainishwa kikanuni. Kutokana na uamuzi huo Biashara United  ilielekezwa kutumia uwanja wa Nyamagana au CCM Kirumba. 

Bodi ya Ligi wakati inafungia uwanja wa Karume ilitoa siku 21 kwa wahusika kufanya  marekebisho yaliyosababisha kufungiwa kwa uwanja huo. 

Aidha, Septemba 27, mwaka huu wa 2020 Bodi ya Ligi ilifungia uwanja wa Jamhuri  mkoani Morogoro kuchezewa mechi za mashindano ya Ligi hadi marekebisho  yatakapofanyika. Sababu za kufungiwa uwanja huo zilitajwa kuwa; ubovu wa eneo la  kuchezea (pitch), vyumba vya kubadilishia nguo na sehemu ya kukaa wachezaji wakati  mchezo ukiendelea. 

Desemba 25, 2019 viwanja vinne vilifungiwa; Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani,  Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Hivyo basi kufungiwa tena mwaka huu tena viwanja  vilevile ni jambo linashangaza. Adhabu ya mwaka jana hadi mwaka huu bado ni za aina  ileile. Hata hivyo hakuna mabadiliko. 

WAMILIKI WAFANYE NINI? 

Tanzania Sports
Baadhi ya Viwanja vinavyohitaji matengenezo (C) Bingwa Tz

Taarifa zinasema asilimia kubwa ya umiliki wa viwanja vya michezo nchini ni Chama  cha Mapinduzi. Kimsingi wamiliki wanataka mapato ili kuendesha uwanja. Wamiliki wa  viwanja vingi ni nchini wanalaizmika kukodisha kwenye sherehe mbalimbali nje ya  michezo. 

Mara kadhaa tumesikia Chama cha Mapinduzi wakikiri kuelemewa gharama za  uendeshaji kwani mapato yatokanayo na mechi mbalimbali hayakidhi mahitaji. Kwamba licha ya vilabu vya soka kukodi viwanja lakini mapato madogo ni chanzo cha  hali mbaya ya viwanja hivyo. Ikumbukwe mwaka 2013 jumla ya viwanja 7 vilifungiwa  kutokana na sababu zinazofanana na sasa. 

Hatua ya kwanza ya kuchukua kwa wamiliki wa viwanja hivyo ni kuendesha kwa ubia na  wawekezaji wengine ambao watakubali kuvitengeneza. Au wamiliki wa viwanja kuamua  kuachana navyo hivyo kuviuza kwa wamiliki wapya ambao watakuwa na uwezo wa  kuvikarabati na kuvifanya kuwa vya kisasa. 

Njia nyingine ni kwa Halmashauri za Wilaya na Manispaa kukabidhiwa viwanja hivyo  kama mnunuzi atakayemiliki kuendesha shughuli ambazo zitakuwa chanzo cha mapato  ya ndani ya maeneo husika. Kwamba serikali inaweza kuchukua kwa maana ya kununua  viwnaja hivyo kutoka Chama cha Mapinduzi na kuvimiliki. Inawezekana sina uthibitisho  kisayansi lakini kwa maoni yangu viwanja hivi vinatakiwa kuuzwa kwa wamiliki  wengine ama Chama cha Mapinduzi kiongeze uwekezaji kwa kuhakikisha vinakuwa na  ubora.

ADHABU YA WAKAGUZI NI IPI? 

Kabla ya Ligi kuanza Kamati ya Leseni ya Bodi ya Ligi Kuu inakagua viwanja vyote  vinavyopaswa kutumika msimu mzima na kuidhinisha vile ambavyo vinakidhi matakwa  ya kikanuni. Mathalani suala la vyumba vya kubadilisha nguo au maeneo ya kukaa  wachezaji ni mambo ya msingi ambayo Kamati inatakiwa kuyazingatia. Ni kwanini  wanaidhinisha viwanja ambavyo havina sifa? Je, nini adhabu ya wajumbe wa Kamati ya  Leseni katika hali hii? Kama hatutachukua kwa pande zote, tatizo la ubovu wa viwanja  litaendelea kututafuna.

Report

Written by Mark Mpangala

*Markus Mpangala ni Mhariri, Mwandishi wa Makala Maalumu, Mwanahabari,Mwanablogu,Mwanafasihi na Mwanasafu, ambapo kwa kipindi cha miaka 12 amefanya kazi katika vyombo vya habari mbalimbali vikubwa na vidogo nchini Tanzania katika Michezo, Siasa, Elimu na utalii. Pia ni mchambuzi mchangiaji wa masuala ya siasa na utawala bora katika idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC SWAHILI). Ni mhariri na mhamasishaji wa usomaji wa vitabu*

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Namungo fc

Namungo ni Singida United iloyochangamka

cedric kaze

Kocha Wa Yanga Kutua Siku Ya Azam FC