in , , ,

TUMSAIDIENI KUJIBU SANCHEZ, AENDE KWA PEP AU MOURINHO ?

Jana kumetoka habari za kocha wa Manchester United, Jose Mourinho
kuonekana kumtaka Alexie Sanchez.

Hii ni baada ya taarifa za awali kuonekana Manchester City kumwihitaji
Alexie Sanchez tangu dirisha la usajili la majira ya joto na dirisha
hili la majira ya baridi.

Ipi sehemu itakuwa na faida kwa Alexie Sanchez ?

Mpaka sasa Manchester City wana washambuliaji kama Sane, Raheem
Sterling, Sergio Aguero, Gabriel Jesus.

Ongezeko la Alexie Sanchez linaweza kuonekana kama kuongeza upana wa
kikosi cha Manchester City lakini kiuhalisia linaweza likaleta hali
isiyo nzuri katika vyumba vya kubadirishia nguo kwa sababu Alexie
Sanchez atakuja kuchukua nafasi ya mtu ambaye alionekana ana nafasi
pia ndani ya kikosi.

Hali hii inaweza kuleta hali mbaya kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

Manchester City wanatumia mifumo kama 3-5-2 na 4-3-3. Mifumo hii yote
Alexie Sanchez anaweza akacheza vizuri.

Mfano kwenye mfumo wa 3-5-2 , Alexie Sanchez anaweza akacheza nyuma ya
mshambuliaji.

Pia katika mfumo wa 4-3-3, anaweza ƙacheza kama false 9, na wakati
mwingine kama mshambuliaji wa kati halisi. Hivo atatakiwa kupigana
kumwondoa Aguero na Jesus.

Kwenye mfumo huu pia anaweza akacheza kama Winger , hali ambayo
itamlazimu apambane kumweka benchi Raheem au Sane.

Hivo kwenda kwake Manchester City kutamfanya agombanie namba kwa kiasi
kikubwa na siyo kuingia kwenye kikosi moja kwa moja kwa sababu
wachezaji waliopo wamezoea mfumo wa Pep Guardiola kwa muda mrefu na
wanafanya vizuri.

Vipi kuhusu Manchester United ?

Manchester United wana matatizo katika eneo la ushambuliaji, wamekuwa
wakitengeneza nafasi nyingi lakini wanatumia chache.

Alexie Sanchez anauwezo wa kufunga kuanzia goli 20 ndani ya msimu mmoja.

Hii itakuwa moja ya tiba ya Manchester United ya kutotumia nafasi
nyingi wanazotengeneza.

Hii ni faida ya kwanza ya Alexie Sanchez kupewa nafasi ya moja kwa
moja kuingia kwenye kikosi cha Manchester United.

Kwenye dirisha kubwa la usajili , Manchester United walihusishwa na
kumsajili Ivan Perisic lakini hawakufanikiwa kumpata.

Katika dirisha hili dogo ni ngumu kumpata Ivan Perisic kwa sababu
upatikanaji wake ni mdogo ukilinganisha na Alexie Sanchez.

Alexie Sanchez anapatikana kwa urahisi sokoni, na anacheza kama Winger halisi.

Mpaka sasa Manchester United wamekuwa wakiwatumia washambuliaji wa
kati kama kina Antony Martial na Marcus Rashford kama washambuliaji wa
pembeni.

Hivyo ujio wa Alexie Sanchez kutakidhi mahitaji ya Manchester United ya
kumpata mshambuliaji halisi wa pembeni.

Hii pia itamsaidia Alexie Sanchez kuwa mtu ambaye ni chaguo la kwanza
katika kikosi cha Manchester United kwa sababu mtu kama yeye
anahitajika ndani ya kikosi.

Manchester United wameandaa kiasi kikubwa cha mshahara kwa Sanchez
kuzidi Manchester City. Hii itakuwa na faida kwa Alexie Sanchez kama
akiamua kwenda Manchester United.

Vipi kwa upande wa Arsenal itanufaika zaidi wapi? Itanufaika zaidi
Sanchez akienda Manchester United au Manchester City?

Jose Mourinho anataka kumpa Arsene Wenger pesa na Henrikh Mkhitaryan
ambaye anaonekana hana nafasi katika kikosi cha Manchester United.

Hii itakuwa na msaada kwa Arsene Wenger ambaye ameandaa zaidi ya Euro
90 M kwa ajili ya kumsajili Thomas Lemar kama mtu wa kuja kuziba pengo
la Alexie Sanchez.

Kumpata Henrikh Mkhitaryan kutampa nafasi ya kumpata mtu wa kuziba
nafasi ya Alexie Sanchez.

Kwa hiyo, Alexie Sanchez kwenda Manchester United utakuwa uhamisho
wenye faida zaidi kwa Alexis Sanchez, Manchester United na Arsenal.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

ROSS BARKLEY ATACHEZAJE KWENYE MFUMO WA CHELSEA?

Tanzania Sports

Man U wamwendea Sanchez