in , , , ,

TETESI ZA USAJILI LEO…

*Chelsea wamtaka Walcott
*Man City wanamvizia Kevin De Bruyne
*Mourinho bado amtaka Douglas Costa
*Cazorla: Siendi popote, nipo Arsenal tu
Adui yako mwombee njaa, ndivyo unavyoweza kusema sasa kwa kinachoendelea miongoni kwa klabu kubwa zinavyotaka kupoka wachezaji kwa kutumia udhaifu.
Chelsea wanafuatilia kwa makini mpango wa mazungumzo ya kuongezwa mkataba Arsenal kwa kiungo wa kimataifa wa England, Theo Walcott ili yakikwama wamchukue.
Bado Walcott ana mkataba Arsenal hadi 2016 lakini bado mazungumzo ya kuuhuisha hayajaanza, na kulikuwapo tetesi kwamba alikorofishana na Kocha Arsene Wenger, japokuwa alikana.
Chelsea walitaka kumshawishi Walcott (26) ajiunge nao alipoingia miezi 12 ya mwisho ya mkataba uliopita na kukwama kwa mazungumzo ya sasa kunatoa hisia za uwezekano wa mchezaji huyo kuondoka Emirates.
Mlinzi wa Ujerumani na Borussia Dortmund, Mats Hummels amesema iwapo angekuwa na nia ya kuondoka kwenye Ligi Kuu ya Ujerumani, lazima angetua Manchester United.
Hummels (26) anayewaniwa na Kocha Lous van Gaal bado ana mkataba Dortmund hadi 2017 na amekana kwamba alitoa ahadi ya kutua Old Trafford, akisema kwamba bado yupo Bundesliga.
Mshambuliaji aliye kwa mkopo Manchester United, Radamel Falcao (29) amesema kwamba atafanya kila analoweza kubaki Manchester United baada ya msimu huu kumalizika.
Baada ya kuwafungia Colombia mabao matatu katika mechi mbili za kimataifa za kirafiki, Falcao anawaza kwamba akirudi Old Trafford ataonesha cheche uwanjani akipewa nafasi.
Katika tukio jingine, Manchester City wanawania kumsajili mchezaji wa zamani wa Chelsea, Kevin De Bruyne (23) anayechezea Wolfsburg nchini Ujerumani.
Chelsea walimuuza De Bruyne kwa pauni milioni 18 mwaka jana.
Kipa wa Tottenham Hotspur, Hugo Lloris (28) anaweza kuondoka White Hart Lane msimu huu wa kiangazi kwa kuuzwa kwa pauni milioni 15 ikiwa Spurs hawatafuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Klabu ya Ligi Kuu ya Ufaransa, Paris St-Germain wanataka kumsajili Lloris kuchukua nafasi ya kipa Mtaliano, Salvatore Sirigu.
Beki wa Cologne, Kevin Wimmer (22) anasema yupo tayari kutimiza ndoto yake ya kutua Spurs kutoka Bundesliga.
Kiungo wa Arsenal, Santi Cazorla (30) amebeza taarifa kwamba anatarajia kurudi nchini mwake Hispania kuchezea Atletico Madrid.
Mshambuliaji matata wa Palermo, Paulo Dybala (21) anadaiwa kusema kwamba chaguo lake la kwanza ni kujiunga Arsenal iwapo ataondoka Italia.
Kwa upande mwingine, Arsenal wanasubiri ufafanuzi juu ya hatima ya kipa mkongwe wa Chelsea, Petr Cech (32) wanayetaka kumchukua baada ya kutupwa nafasi ya pili nyuma ya chipukizi Thibaut Courtois.
Mmiliki wa Southampton, Katharina Liebherr amesema hana tatizo la fedha hivyo haoni sababu ya kumuuza beki wao wa kulia, Nathaniel Clyne (23) wala kiungo Morgan Schneiderlin (25). Ameikopesha klabu hiyo pauni milioni 20.
Beki wa kushoto wa Real Madrid, Fabio Coentrao (27) amesema ingekuwa heshima kubwa iwapo angepewa nafasi kuchezea Manchester United.
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho ameanza tena jitihada zake kumsajili kiungo wa Shakhtar Donetsk, Douglas Costa (24) na yu tayari kulipa pauni milioni 20.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

England, Italia hakuna mbabe

Morocco waibwaga CAF kortini