in , , ,

TETESI ZA USAJILI DIRISHA DOGO

*Vikumbo Chelsea, Arsenal, Liverpool

Harakati za usajili katika dirisha dogo la msimu wa 2014/15 zimeanza, ambapo Leicester wamewapiku Chelsea kwa kumsajili mshambuliaji wa Croatia, Andrej Kramaric (23).

Leicester walio katika hatari ya kushuka daraja wakati Chelsea wapo nafasi ya kwanza wamevunja rekodi ya klabu hiyo kwa kutoa dau la pauni milioni 9.7 kwa klabu ya Rijeka.

Arsenal wanaendelea kumzengea kiungo wa Southampton, Morgan Schneiderlin (25) na wapo tayari kutoa pauni milioni 25 mwezi huu.
 
Mabingwa wa Ulaya, Real Madrid wanatarajiwa kumsajili kiungo Mnorway mwenye umri wa miaka 16, Martin Odegaard ambaye tayari ametua Madrid kukamilisha mambo.

Liverpool wamekubali kutoa pauni milioni 10 kumnasa kiungo wa Bayern Munich, Xherdan Shaqiri (23). 

Arsenal wamekwama katika jitihada zao za kutaka kumsajili kinda wa miaka 17 kutoka Legia Warsaw, Krystian Bielik.
 
Kocha mpya wa Real Sociedad, David Moyes anaendelea vyema na mpango wake wa kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Joel Campbell (22)
Borussia Dortmund wanaelekea kuwa tayari kumwachia kiungo Ilkay Gundogan (24) kuhamia Manchester United kwa pauni milioni 16, lakini bado makubaliano ya mwisho hayajafikiwa.

West Ham wameonesha nia ya kumchukua kiungo wa Atletico Madrid, Mario Suarez (27)

Liverpool bado hawajafikia makubaliano yoyote juu ya kumrejesha mshambuliaji wao, Divock Origi (19) aliye kwa mkopo Lille nchini Ufaransa.
Mshambuliaji wa Chelsea, Islam Feruz (19) ameeleza nia yake ya kusajiliwa na Cardiff City kwa mkopo hadi mwisho wa msimu ili apate muda wa kucheza.

Chicago Fire wametangaza kumsajili mshambuliaji wa zamani wa kati wa Southampton, Guly do Prado (33).
 
Kocha wa Timu ya Taifa ya England, Roy Hodgson amemwelezea mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane (21) kama mchezaji aliye katika kiwango cha hali ya juu.

Kipa wa zamani wa Liverpool, Bruce Grobbelaar ametabiri anguko la klabu hiyo wakimwacha nahodha wao na mchezaji wa muda mrefu, Steven Gerrard (34) kuondoka.

Pasted from

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Blatter apata mpinzani Fifa

Champagne kuwavaa Blatter, Prince Ali