*Rodriguez aikataa Man U, aenda Real Madrid

*Arsenal, Man U wamgombea Alexis Sanchez

*Wenger anamtaka  Arturo Vidal, Mandzukic

 

Dirisha la Usajili wa Ligi Kuu England linafunguliwa rasmi Julai Mosi, ambapo klabu zimeshaanza kujipanga, baadhi zikiwa zimenasa wachezaji, japo mmoja au wachache.

Chelsea wanajaribu kuwapiga kumbo Liverpool katika kumuwania Lazar Markovic huku pia wakijiandaa kuwapita Manchester United katika kumnasa William Carvalho wa Sporting Lisbon.

Kadhalika, Arsenal na Chelsea wana hadi Jumatano hii kujua iwapo wapo katika nafasi ya kumsajili mshambuliaji anayeondoka Bayern Munich, Mario Mandzukic.

Manchester United wapo katika mazungumzo na kiungo wa Benfica, Nicolas Gaitan na huenda wakamjumuisha Bebe katika dili lolote la raia huyo wa Argentina.

Mshambuliaji kinda aliyeng’ara katika fainali za Kombe la Dunia na Timu ya Taifa ya Colombia, James Rodrgiuez amesema hataweza kujiunga na Man United kwa sababu ndoto yake ni kucheza Real Madrid, na ndiko anaelekea.

Kocha wa Uruguay, Oscar Tabarez aliyepoteza mechi dhidi ya Colombia kutokana na mabao ya Rodriguez (22) amesema kwamba kijana huyo ni mzuri kama Lionel Messi.

Liverpool wamesema hawana nia ya kutumia kifungu cha mkataba kinachowaruhusu kumsajili Iker Muniain mwenye thamani ya pauni milioni 36 kutoka Athletic Bilbao, hivyo kumpa fursa ya kumfuata Ander Herrera Man United.

Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal anafikiria kupunguza gharama kwa kumsajili Mdachi Nigel de Jong huku klabu ya Eintracht Frankfurt wakijipanga kumsajili Marko Marin wa Chelsea na garasa la Arsenal, Nicklas Bendtner.

Liverpool wanaweza kumkosa winga wa Hellas Verona, Juan Manuel Iturbe (21) baada ya Juventus kuweka mezani dili la euro milioni 21 pamoja na mchezaji wao, Fabio Quagliarella.

Arsenal wamedhamiria kumsajili winga wa Barcelona na Chile asiyetaka kubaki Camp Nou, Alexis Sanches lakini watapata ushindani kutoka kwa Man United. Arsenal pia wamejiandaa kupeleka ‘posa; Southampton kwa ajili ya kiungo mkabaji, Morgan Schneiderlin. Inadaiwa wametenga pauni milioni 42 kwa ajili ya wawili hao.

Kocha Arsene Wenger pia amedokeza kwamba watajaribu kuwapandia mgongoni Man United ili kupata saini ya kiungo mwingine wa Chile, Arturo Vidal.

Old Trafford pia wanaonena wanataka kuhakikisha beki wa Kidachi, Stefan De Vrij anakuwa mchezaji wao wa tatu kusajiliwa msimu huu wa kiangazi baada ya kuelezwa wamewazidi kete Lazio kwa ajili ya mchezai huyo wa Feyenoord.

Habari nyingine ni kwamba Liverpool wanataka kuwaomba Fifa wamruhusu mshambuliaji wao, Luis Suare, raia wa Uruguay, aendelee kufanya mazoezi nao katika kipindi cha miezi mine aliyofungiwa.

Bado Arsena wapo njia panda juu ya iwapo wamrejeshe kundini mshambuliaji wao raia wa Costa Rica, Joel Campbell anayetamba Brazil au wamuendeleze katika timu nyingine kwa mkopo kama alivyo Olympiakos sasa.

Robin van Persie amesema anafuata nyayo za kocha wake kwa kutokwenda likizo ya msimu huu wa kiangazi ili aandamane na timu kwenye ziara nchini Marekani baadaye Julai hii. Kwa uraia wa Uholanzi wa Van Gaal, kuna dalili ya wachezaji wengi wapya kutoka nchi hiyo kusajiliwa Old Trafford.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Aveva rais mpya Simba

Nigeria wafungishwa virago