in , , ,

Tembo wa Afrika…

Ivory Coast, England wapoteza
*Colombia, Uruguay wapeta

Hatua za makundi za fainali za Kombe la Dunia zimeendelea kufunguka, ambapo Ivory Coast wamepoteza mechi kama walivyofanya England.

Wakati Tembo wa Afrika wakipoteza mechi yao kwa Colombia baada ya kushinda ile ya awali, England wamepoteza mechi ya pili, safari hii wakipigwa na Uruguay.

Lakini wote walikuwa na ufanano katika kifungo, kwani walichapwa 2-1 na palikuwa na jitihada tosha za kutafuta ushindi lakini siku hazikuwa zao.

Colombia wanakaribia kutinga kwenye hatua ya mtoano ya timu 16, ambapo Alhamisi hii walipata mabao yao kupitia kwa James Rodriguez na Juan Quintero na timu kuwa juu kwa 2-0.

Hata hivyo, Gerviho, mshambuliaji wa zamani wa Arsenal alichomoa moja baada ya kuwatoka mabeki watatu wa Colombia na kurejesha matumaini kwa Tembo hao. Waafrika walitia shinikizo kubwa mwishoni lakini Colombia wakahimili.

Waafrika hao sasa watawakabili Ugiriki katika mechi ijayo na wanaweza bado kufuzu kwa hatua za mtoano kwa sababu Ugiriki walikwenda sare na Japan katika mechi nyingine Alhamisi hii.

ENGLAND NAO WAKUBAI KICHAPO
20140620-074510-27910254.jpg

England wapo katika limbo la kutolewa kwenye fainali za Kombe la Dunia mapema baada ya kupoteza mechi ya pili.

Kama kuna mtu watakayemkumbuka kwa ubaya huo ni mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez wa Uruguay aliyewafunga mabao mawili katika mechi yao ya pili ya kundi lao.

Hatimaye Wayne Rooney alifanikiwa kufunga bao lake la kwanza katika fainali za Kombe la Dunia akisawazisha moja la Suarez. lakini mchezaji huyo wa Uruguay aliongeza la pili dakika za mwisho.

England sasa wamebakisha mechi moja dhidi ya Costa Rica na Uruguay na pia England wawafunge Costa Rica.

Hata hivyo, hayo ni matumaini makubwa sana kwa timu na watu kujipa, kwa sababu kufungwa mechi mbili za awali ni moja ya tiketi za kutolewa kwenye michuano kwa kuwa imebaki mechi moja. Hakuna timu iliyopata kusonga mbele baada ya kupoteza mechi mbili za awali.

Ilikuwa Suarez asicheze, na kocha wake alisema hivyo kwa sababu hakuwa fiti baada ya upasuaji wa goti mwezi mmoja uliopita, lakini uwanjani alikuwa tishio kubwa.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Kimenuka Hispania

Arsenal wamwita Ivanovic