in

TBF yapiga hatua katika kukuza mpira wa kikapu Tanzania…

Shirikisho la mpira wa kikpu Tanzania (TBF) tunayo furaha kuwatangazia kuwa tutaendesha mafunzo maalumu (Basketball Clinic) ya vijana chini ya miaka 17 itakayofanyika Arusha tarehe 9-10 Juni, 2012.

Mafunzo haya yataendeshwa mmoja wa makocha bora sana wa kikapu duniani anayetokea Marekani anaitwa Greg Brittenham, ambaye ni alikuwa kocha msaidizi kwa miaka 20 wa timu ya NBA inayoitwa New York Knicks ya Marekani, kocha huyo tayari yuko nchini.

Mafunzo haya yamewezekana kupitia Mtanzania anayeishi Uingereza Israel Saria mmliki wa
www.tanzaniasports.com/new .ambaye ndie aliyetusaidia kumpata Kocha huyo. Habari zaidi za kocha huyo soma hapa: http://www.nba.com/coachfile/greg_brittenham/index.html au http://www.wakeforestsports.com/sports/m-baskbl/spec-rel/082611aaa.html
Kuwezesha mafunzo haya tumesaidiwa na watu wa Marekani kupitia ubalozi wa Tanzania ambao wametoa mipira na fedha za uwezeshaji na Kampuni ya Cocacola ambao nao wametoa mipira na vinywaji kwa vijana watakaoshiriki mafunzo hayo na kocha Greg ametoa fulana kwa vijana wote 100 na pia amejitolea kufanya mafunzo haya bila malipo, tunawashukuru sana.
Vijana watakaoshiriki mafunzo haya ni 100, kati ya hao wasichana ni 30 na wavulana ni 70 na wote ni wanafunzi wa shule mbali mbali kutoka jiji la Arusha na niji jirani.
Tunawashukuru walimu, wazazi na wadau wote wanaoshirikiana nasi kufanikisha mafunzo haya
Tunaomba wakazi wa Arusha na maeneo jirani wafike kwa wingi katika viwanja vya Soweto amboko ndiko mafunzo haya yatafanyika kwa siku 2 kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 9 alasiri.
TBF kwa kushirikana na wadau wetu tuliowataja hapo juu na wengine tutendelea kuendesha mafunzo kwa vijana wetu wadogo nchi nzima ili tuwajengee msingi mzuri nan i matumaini yetu kati ya hawa baadhi yao watakuwa ni wachezaji mashuhuri siku za baadae.
[email protected]

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Mambo matatu yanayoihangaisha timu ya ย Yanga

Wachezaji wa kigeni katika ligi kuu ya EPL