in

TAVA Yawanoa Makocha wa Wavu Mikoani

CHAMA cha Mpira wa Wavu Tanzania (TAVA), kimeanza kuwapatia mafunzo ya wiki moja makocha wa mchezo huo wa Zanzibar kwa ngazi ya kwanza.

Mafunzo hayo yaliyoanza juzi jioni, yanashirikisha makocha 42, ambao wanafundishwa mbinu mbalimbali zitakazowawezesha kuwafundisha wachezaji wanaoanzia ngazi za chini.

Mkufunzi wa mafunzo hayo Alfred Selengia kutoka kamati ya Maendeleo ya mchezo huo, amesema mafunzo hayo yanafanyika chini ya ufadhili wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Wavu (FIBV) kupitia mfuko wake wa maendeleo.

Alisema, FIVB kupitia mfuko wake huo, imetoa vifaa vya kuendesha mchezo huo ikiwemo mipira 80 na nyavu kumi vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 21.8.

Alifahamisha kuwa, mafunzo hayo ni mpango wa TAVA wa kuendeleza mchezo huo Tanzania ambapo kwa kuanzia wameanza na Zanzibar na baadae wataendelea katika mikoa ya Tanga, Mwanza, Morogoro, Manyara,

Kilimanjaro, Arusha na Dar es Salaam, na kila mkoa utapatiwa vifaa hivyo.

Aliongeza kuwa, lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwanyanyua wachezaji wachanga pamoja na kupata wachezaji wengi wenye ujuzi sahihi katika mchezo huo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply
  1. HUU NI MPANGO MZURI NA INSHALLAH NI MATARAJIO YETU SASA VOLLEYBALL TANZANIA ITAANZA KUPANDA NA KUSONGA MBELE.

    TUUNGANISHE NGUVU KWA PAMOJA ILI KUURUDISHA MCHEZO WETU KWENYE CHATI YA KIMATAIFA KAMA ILIVYOKUWA MIAKA YA 80 NA 90 HUKO.

    LETS KEEP THE BALL FLYING!!!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Man City imekaribia kuwa bingwa…

Milima na Mabonde Soka ya Uingereza