in

  Tanzania yajaa matumaini kupata medali olimpiki

KIJANA Mtanzania mwenye ulemavu wa miguu,  Zaharan Mwenemti  ni mmoja wa Watanzania watano watakoiwakilisha nchi katika michuano ya Olimpiki itakayofanyika nchini Uingereza mwishoni mwa Julai , mwaka huu.

Mwenemti ambaye kwa sasa anajifua kwa udi atacheza michezo mitatu ambayo ni kurusha tufe, kurusha kisahani na kutupa mkuki.

Mbali ya mchezaji huyo mahiri, pia wapo vijana wapya wane wanaotegemewa kupata medali kwa masuala ya riadha na kuogelea.

Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi ameviambia vyombo vya habari kwamba ana uhakika vijana wa riadha watatwaa medali  kwenye michuano hiyo itakayotimua vumbi nchini Uingereza.

Matumaini ni makubwa, vijana wanaendelea kujifua vizuri hususan wa riadha’’ alisema alipowazungumzia wanariadha waliopiga kambi katika Mji wa Kibaha kilometa karibu 50 kutoka  Jiji la Dar es Salaam.

Wanariadha tegemeo ni  Samson Ramadhani ambaye anajifua kwa kufukuza upepo katika umbali wa mita 5,000 pamoja na Fustine Mussa na Musendeki Mohamed anayetarajiwa kupata medali ya kuongelea.

Bayi ambaye aling’ara katika riadha mwaka 1980 kwa mbio za mita 3,000 aliwahakikishia waandishi kwamba anayo imani kubwa na wanamichezo wake wanaokwenda kwenye olimpiki.

Kwa upande wa ngumi kijana pekee ni Seleman Kindunda ambaye anajifua usiku na mchana kujiandaa na michuano hiyo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Basketball Clinic kwa Msaada wa tanzaniasports.com Arusha.

Hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya vijana wa chini ya miaka 17 Arusha tarehe 9, Juni 2012.