in

Tambo za Yanga, Simba katika soka la Tanzania zinakaribia mwisho

Kwa miaka zaidi ya 70  Soka la Tanzania lilikuwa likitawaliwa na timu mbili maarufu ambazo ni Simba Sports Club na Yanga Africans Sports Club.
Timu hizi zimekuwa zikitamba karibu miaka yote ingawa ipo miaka  ambayo  zilienguliwa kwenye ubingwa, lakini zikaambulia kwenye nafasi ya pili na ya tatu.
Kwa mfano moja ya timu iliyozifedhehesha timu hizo kwa mwaka mmoja ni Tukuyu Stars  ya Mbeya ambayo ilishiriki ligi kuu kwa mara ya kwanza na kutwaa ubingwa wa bara na Muungano.
Pamoja na kuibuka kwa timu kama hiyo, lakini ukweli  ni kwamba Simba na Yanga ni timu ambazo zimekuwa zikipata umaarufu kutokana na kuwa mabingwa mara nyingi.

 
Hata hivyo, umaarufu wa timu hizo sasa uko shakani kutokana na sababu kadhaa ambazo zingine zipo ndani ya Klabu zenyewe, ndani ya nchi na zingine nje ya nchi.
Moja ya sababu ambazo zimo ndani ya klabu hizo ni suala la kukosa mmliki  na badala yake kuitwa timu za wanachama jambo ambalo ni gumu sana kulielewa katika soka la sasa.
Timu za Simba na Yanga kwa sasa hazina wamiliki, bali zina wanachama ambao ndio wanawachagua viongozi  wa timu.
Kwa mbali unaweza kusema timu hizo ni sawa na vyama vya ushirika, lakini tofauti ni kwamba wanachama wa vyama vya ushirika wanachangia kwa malengo ya kupata  faida, wakati suala la timu wengi wanachangia ili kupata malengo ya siri pamoja na kuwasaidia wachezaji.
Hali hiyo inawafanya wachangiaji wa fedha mara nyingi wabaki wachache huku wengine wakibaki kupiga domo la ushabiki.
Timu ambazo zimo kwenye matatizo ya kukosa wamiliki ni Villa, Coastal, na Toto African, wakati timu zenye wamiliki wa uhakika ni Azam.  Lakini pia  timu za Mtibwa, JKT Ruvu, Ruvu Shooting, JKT Oljoro, Polisi, Kagera, Moro United na Lyon zina wamiliki ambao wakiamua wanaweza kuwekeza na kuzikuza zaidi kiasi cha kuzifunika Yanga na Simba..


Kinachotakiwa kwa timu zenye wamiliki kujipanga kwa kuunganisha nguvu kujenga viwanja na kumiliki. Wachezaji wa timu zenye wamiliki mara nyingi wana uhakika wa kufanya kazi kwa kufuata maelekezo ya bosi ambaye anaweza kuwaacha kama wanazembea.
Klabu zisizo na wamiliki wa uhakika , uamuzi wake unakuwa wa utata na kuzusha migogoro isiyo ya lazima.
Lakini pia upo uwezakano kwamba wachezaji wengi wa Yanga na Simba wanakuwa na usongo wa mawazo kutokana na migogoro iyaowakumba viongozi waklabu hizo.
Kufuatia hali hiyo, timu zisizo na wamiliki kamili zipo shakani kutokana na ukweli kwamba  utandawazi, Watanzania ama mashabaki wengi wa soka wamepoteza  hamu na timu za Yanga na simba kutokana na migogoro hiyo.
Lakini pia wachezaji wengi wa timu hizo wanacheza bila kufikiria ubora wa viwango katika Afrika na kulinganisha na vile vya nchi za Ulaya.
Lakini sababu zingine ambazo zitaziua klabu za Simba na Yanga ni kwa viongozi waliochaguliwa kwenye timu hizo kukosa mipango ya maendeleo kutokana na hofu ya kutimuliwa wakati wowote iwapo tu klabu zitaboronga.
Kuwa kiongozi kwenye klabu hizo ni tofauti na kuwa kiongozi wa ushirika kwa sababu kipimo cha uongozi Yanga ni kuishinda Simba ama kupata ubungwa jambo ambalo ndilo pia kwa Simba.
Viongozi wa klabu hizo hawana nafasi ya kufikiria zaidi maendeleo ya soka kwa kuanda viwanja vya kisasa na hata kuendeleaza watoto kisoka.
Tofauti na klabu hizo timu changa ya Azam inayomilikiwa na mfanyabiashara maarufu wa Dar es Salaam  imeonyesha njia kwa kuamua kutengeneza uwanja na hata vyumba mbalimbali vya mazoezi.
Pigo lingine ambalo litachangia kuziua timu hizo ni kwa watoto wengi wa Kitanzania kupenda timu za Uingereza.
Kutokana na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano ,Watoto wengi wa Tanzania wamekuwa mashabiki wa timu mbalimbali za Ulaya zikiwamo za Liverpool, Man United, Chealse na Arsenal.
Brighton Bansy mwenye umri wa miaka 13 anayeishi Tabata Dar es Salaam ni miongoni mwa watoto wasiofahamu majina ya wachezaji wa Yanga na Simba badala yake anawafahamu wachezaji wote wa Man U , Liverpool na hata wale wa Barcelona.
”Wachezaji wa Yanga na Simba siwajui kwa sababu wanacheza vibaya na wanafungwafungwa” anasema.
Mtoto huyo bila shaka alisema hayo kutokana na ukweli kwamba Yanga kwenye ligi kuu inayoendelea Tanzania sasa, hadi Septemba 25 ilikuwa imecheza mechi saba  na ilifungwa mechi mbili na kutoka sare tatu huku ikiambulia kushinda mechi mbili na ikiwa kwenye nafasi ya nane kati ya timu 14.  Nayo Simba pamoja na kuongoza, lakini bado inapata ushindi wa goli moj amoja. Simba ilicheza mechi saba na kutoa sare mechi tatu na kushinda nne.

[email protected]

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Tanzania in durable decline in track, field sports

Afrika Kusini kuandaa Kombe Afrika 2013