Taifa Stars, kushuka dimbani kesho..

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kesho inashuka dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwakabili Chad katika mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2017.

Taifa Stars itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa bao 1-0 ilioupata katikati ya wiki jijini N’Djamena katika uwanja wa Idriss Mahamat Ouya, bao lililofungwa na nahodha Mbwana Samatta dakika ya 30 ya mchezo.

Kocha wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema maandalizi kwa kikosi chake yamekalimika, vijana wote wapo katika hali nzuri ya kusaka ushindi ushindi kesho, kikubwa amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Taifa kujwa kuwapa sapoti vijana watakapokuwa wakiwakilisha Tanzania.

Kuelekea katika mchezo huo, tiketi za mchezo zimeanza kuuzwa leo katika vituo vya Ubungo Oilcom, Buguruni kituo cha mafuta, Mbagala Darlive na Karume ofisi za TFF. Viingilio vya mchezo huo ni Shilingi 25,000 kwa VIP A, Shilingi 20,000 kwa VIP B na Shilingi 5,000 kwa viti vya rangi ya Blu, Kijani na rangi ya Machungwa.

Comments