in

Wachezaji 5 waliobeba Simba SC

Jana Simba SC walianza vyema kampeni yao ya mechi za ligi ya mabingwa barani Afrika katika hatua ya makundi kwa kuifunga As Vita kwenye uwanja wa nyumbani wa As Vita.

Matokeo haya yanaipa nafasi nzuri Simba SC kwenye kundi lao. Tuachane na matokeo ya jana tutazame wachezaji wanne ambao waliibeba kwenye mechi hiyo ya jana ambayo Simba Sc alishinda goli moja (1) kwa sufuri dhidi ya As Vita.

1: AISHI MANULA

Aishi Manula aliiweka Simba Sc ndani ya mchezo kwa kuokoa michomo mbalimbali ambayo ilikuwa ya hatari. Aishi Manula alisimama imara pia katika kuipanga safu yake ya ulinzi pamoja na yeye kuonekana kuchomoa michomo mbalimbali.

TADEO LWANGA

Kazi yake kubwa ni kutibua mipango yote ya As Vita katika eneo la kati. Alipokonya mipira iliyokuwa karibu na eneo la ulinzi. Alihakikisha pia anatoa ulinzi mzuri kwenye mabeki wa kati wa Simba Sc kwa kiwango kikubwa.

3: MZAMIRU YASSIN

Moja ya faida kubwa ambayo Simba SC walipata kupitia Mzamiru Yassin kwenye mechi ya jana ni uwiano katika eneo la katikati. Mzamiru Yassin alikuwa anakaba na kuchukua mipira iliyokuwa inapokonywa na Tadeo Lwanga na kupiga pasi kwenda mbele.

Faida nyingine ambayo Mzamiru Yassin aliitoa kwa Simba SC ni yeye kuwapa nafasi kina Luis Miqussione, Claoutus Chama na Lary Bwalya kuwa katika eneo la mbele wakati Simba ilipokuwa inashambulia.

4: CHRIS MUGALU

Achana na goli alilofunga jana. Lakini Chris Mugalu ni moja ya wachezaji ambao waliweka hai mpango mkakati wa Simba SC kwenye mechi ya jana.

Chris Mugalu hakuwapa uhuru mkubwa mabeki wa kati wa As Vita. Hawakupata uhuru wa kusogea mbele kwa ajili ya mashambulizi. Pia Chris Mugalu  alikuwa anakaba kuanzia juu na alikuwa anashuka chini kukaba.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Ndayiragije

Tumlaumu kocha wa taifa stars au TFF?

Scott McTominay

Manchester United wanaugua ugonjwa wa Liverpool?