Michezo yote 10 ya wiki ya tatu ya EPL imeshachezwa. Kwenye makala hii mwandishi wetu amechagua kikosi cha wachezaji 11 waliofanya vizuri kwenye michezo ya EPL wiki hii.

 

Golikipa: JACK BUTLAND (Stoke City)

 

Golikipa huyu alifanya maajabu alipookoa mashuti manne ya hatari kwenye kipindi cha pili cha mchezo dhidi ya Norwich na kuihakikishia timu yake sare iliyoipatia alama moja muhimu.

 

Mlinzi wa kulia: RITCHIE DE LAET (Leicester City)

 

Alikuwa akipanda na kushuka kwenye mchezo dhidi ya Tottenham hapo juzi. Alikuwa na morali ya hali ya juu na hili likamfanya atekeleze pia majukumu yake ya ulinzi kwa umakini.

 

Mlinzi wa kati: FABRICIO COLOCCINI (Newcastle United)

 

Coloccini aliwapa changamoto imara washambuliaji wa Manchester United na kuisaidia timu yake kumaliza dakika 90 bila kuruhusu bao kwa mara ya kwanza msimu huu.

 

Mlinzi wa kati: VINCENT KOMPANY (Manchester City)

 

Nahodha huyu wa City aliwadhibiti vizuri washambuliaji wa Everton na kuhakikisha timu yake imeendeleza makali yake kwenye ulinzi ikiwa haijaruhusu bao lolote kwenye mechi zote 3 msimu huu.

 

Mlinzi wa kusoto: ALEKSANDAR KOLAROV (Manchester City)

 

Alikuwa imara sana kwenye mchezo dhidi ya Everton hasa kwenye mashambulizi. Alipokea pasi ya Raheem Sterling akiwa kwenye nafasi finyu ya kufunga lakini akafunga bao na kutushangaza.

 

Kiungo wa kati: MATT RITCHIE (Bournemouth)

 

Ritchie alifanya vizuri kwenye nafasi ya kiungo hasa kwenye kuanzisha mashambulizi ya Bournemouth ambao waliwatandika West Ham 4-3 na kuweka rekodi ya ushindi wao wa kwanza wa EPL kwenye historia yao.

 

Kiungo wa kati: JAMES MORISSON (West Bromwich)

James Morrison (kulia)
James Morrison (kulia)

 

Wengi tulifikiri kukosa penati kwenye dakika za mwanzoni kungemuathiri kiungo huyu kwenye mchezo mkali dhidi ya Chelsea. Lakini haikuwa hivyo, akatulia na kuifungia timu yake mabao mawili.

 

Kiungo wa kulia: DAVID SILVA (Manchester City)

 

Achana na lile shuti lake zuri lililogonga mwamba. Kinachomuweka Silva kwenye kikosi hiki ni makali aliyoyaonyesha kwa kuwanyanyasa walinzi wa Everton dakika zote za mchezo.

 

Kiungo wa kushoto: RYAD MAHREZ (Leicester City)

 

Alionyesha kiwango kikubwa mno dhidi ya Tottenham. Aliwahadaa alivyotaka walinzi wa timu hiyo kwa kutumia kasi yake na chenga. Zaidi ya hapo aliifungia timu yake bao la kusawazisha ambalo ni la nne kwake msimu huu.

Mshambuliaji: PEDRO RODRIGUEZ (Chelsea)

 

Makali aliyoyaonyesha kwenye mchezo wake wa kwanza akiwa na Chelsea hapo juzi yanatosha kabisa kumuweka kwenye kikosi hiki. Alifunga bao moja na kutengeneza lingine hivyo akaipa Chelsea ushindi wa kwanza msimu huu.

 

Mshambuliaji: CALLUM WILSON (Bournemouth)

 

Aliifungia Bournemouth mabao matatu na kuipa timu hiyo ushindi wake wa kwanza wa EPL kwenye historia yao. Pia amekuwa mchezaji wa kwanza kuifungia bao timu hiyo kwenye EPL na mchezaji wa kwanza kufunga (hat-trick) msimu huu.

advertisement
Advertisement

Report

Written by Kassim

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Cech awapa Arsenal pointi

Balotelli aenda AC Milan