in

Naikubali Simba, Ajibu fundi sana- Shahanga

Simba Sports Club

Utamaduni wa kupenda timu inayotoka katika kitongoji chako upo barani Ulaya peke yake sio Tanzania na  Afrika kwa ujumla, huku kuna utaratibu mwingine kabisa.

Gidamis Shahanga ni mwanariadha maarufu aliyeshinda medali nyingi ikiwemo zile mbili za jumuiya ya madola ‘Commonwealth games’  alizinyakua mwaka 1978 na ile ya 1982 ya mita elfu kumi (10,000).

Tovuti hii www.tanzaniasports.com ilipata nafasi ya kumuuliza yeye ameegemea upande gani kati ya timu hizi  kuu mbili  ambazo ndio pendwa zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki Simba au Yanga.

Hakupata taabu kujibu aliweka wazi kuwa Simba ndio moyo wake ulipolalia ila sio kama walivyo mashabiki wengine kuwekeana ahadi zisizo na msingi.

Shahanga akizungumza nasi

“Mimi nashabikia timu inayotegemea kuchukua ubingwa hivi karibuni ambayo ni Simba,”alisema.

Shahanga ameweka wazi kuwa yeye anashabikia ila sio kama wengine wanaweka ahadi ya majumba au hata wake zao kuwaweka rehani.

“Mimi ni shabiki wa kawaida ila sijafika huko kwa kupenda hadi kuahidi vitu vingi, siwezi kuahidi mke wala nyumba kama timu yangu ikifungwa au kushinda, kuna wengine wanavua na nguo kabisa mimi sipo huko,”alisema.

Pia amefurahishwa kwa kurejea kwa ligi kwani kutatoa bingwa halali wa michuano ya mwaka huu, akiweka wazi kuwa Korona ilitaka kuharibu taswira hii nzuri ya michezo.

“Nimefurahishwa kurejea kwa ligi, sipendi mshindi apatikane mezani, natamani washinde wakiwa kiwanjani, yaani tushindane kwa hoja za kiwanjani, nataka kombe liende kwa wanaoshinda kiwanjani,”aliongeza.

Juu ya maendeleo ya michezo pia amethibitisha kwa sasa kila kitu kinaenda vizuri tofauti na zamani, ili mambo yaende sawa katika michezo yote lazima viongozi wanaosimamia wawe weledi.

Alitanabaisha kuwa  endapo kampuni au taasisi mbalimbali zikijitokeza kudhamini wanaosimamia wanatakiwa wazifikishe mahali husika kwa ufasaha.

“Niwaombe viongozi mbalimbali wanaosimamia mashirikisho wanatakiwa wawe wawazi na wakweli, kama kampuni au taasisi zikijitokeza kudhamini inatakiwa kinachopatikana wakipeleke sehemu husika,”alisema.

Ilicha ya kuipenda timu ya Simba SC anamuona nyota wa timu hiyo Ibrahim Ajib fundi sana katika kucheza mpira.

“Ajibu ni mchezaji mzuri sana miongoni mwa wachezaji wanaojua sana mpira naamini kama watanzania tutathamini vya kwetu wachezaji wengi watatoka katika soka la kimataifa,”alisema.

Shahanga amesisitiza kuwa vijana wanatakiwa wajitume na wawe na dhamira ya kweli ya kucheza soka kimataifa huenda taifa likapata watu sahihi wa kuwatumia katika mechi za kimataifa za mataifa ya Afrika.

Inawezekana kabisa shabiki wa Aston Villa akija Tanzania akifanya uchunguzi juu ya utaratibu wa maisha ya wapenda soka wan chi hiii basi atashangaa sana kuona namna mtu yupo Shinyanga ila ana mapenzi li alia na Simba au Yanga.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

74 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
David Beckham anayechukiwa zaidi England.

Wachezaji hata uwachukie lakini utawapenda tu!

YANGA

Niyonzima mwenye sura ya “Uongozi” na “Ufundi”