in , , ,

Arsenal watwaa Kombe la Emirates

*Man United wasajili kipa Romero

Arsenal wamekamilisha maandalizi ya msimu mpya kwa kutwaa taji la pili katika michezo ya kirafiki, Jumapili hii wakitwaa Emirates Cup kwa kuwafunga Wolfsburg kutoka Ujerumani 1-0.

Kwenye mechi ya nyumbani iliyohudhuriwa na watazamaji 59,815 huku kipa wao mpya, Petr Cech akilakiwa na washabiki kwa mara ya kwanza, Arsenal walipata bao lao kupitia kwa Theo Walcott anayekaribia kusaini mkataba mpya wa ‘muda mrefu’.

Vijana wa Arsene Wenger wamekuwa na maandalizi mazuri na mwelekeo chanya kabla ya mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Chelsea wikiendi ijayo, ambapo awali walitwaa Barclays Asia Trophy.

Walcott alifunga baada ya pasi maridadi ya kijana mwenye umri wa miaka 17, Jeff Reine-Adelaide huku Josuha Guilavogui wa Wolfsburg nusura awapatie bao kwa shuti kali la yadi 25 ambapo hata hivyo, Cech, aliyesajiliwa kwa pauni milioni 10 kutoka Arsenal alilipangua.

Hii ni mara ya kwanza kwa Arsenal kutwaa Kombe la Emirates tangu 2010, ambapo wamekuwa wakitolewa na washindani wao. Wenger alibadilisha wachezaji 10 ya wale walioanza dhidi ya Lyon na kuwafunga 6-0 majuzi, ambapo mchezaji pekee aliyeanza ni Mesut Ozil.

Winga Reine-Adelaide alivuta hisia za watu kwa jinsi alivyokuwa akicheza na Wenger alieleza kwamba ana kipaji cha pekee. Wolfsburg walioshika nafasi ya pili kwenye Bundesliga msimu uliopita walimtumia mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Nicklas Bendtner.

Kiungo wa zamani wa Chelsea, Kevin De Bruyne alionekana kutofanya vyema uwanjani na iwapo Manchester City wanaotaka kumsajili walimfuatilia, wanaweza kuachana na mpango wao wa kutoa pauni milioni 60 kumnasa.

Arsenal waliwachezesha Cech, Calum Chambers, Hector Bellerin, Nacho Monreal, Gabriel Paulista, Ozil (Chuba Akpom, 46), Santi Cazorla, Wilshere (Hayden, 76), Reine-Adelaide (Alex Oxlade-Chamberlain, 64), Mikel Arteta (Aaron Ramsey, 63), Walcott (Olivier Giroud, 75).

MANCHESTER UNITED WAMSAJILI KIPA ROMERO

Romero ndani ya Man Utd
Romero ndani ya Man Utd

Katika kile kinachoonekana kujiandaa na lolote iwapo kipa David De Gea ataondoka Old Trafford, Manchester United wamemsajili kipa wa Argentina, Sergio Romero.

De Gea amekuwa akihusishwa na mipango ya kurejea nchini mwake, Hispania, kwa ajili ya kuchezea Real Madrid. Romero alikuwa mchezaji huru baada ya kuondoka Sampdoria na atachukua nafasi ya Victor Valdes, aliyekorofishana na bosi Louis van Gaal.

Kocha huyo amemwambia Valdes aliyekuwa mchezaji huru baada ya kuachana na Barcelona, kwamba anaweza kuondoka wakati wowote. Romero, 28, amesaini mkataba wa miaka mitatu na alichezea Argentina katika fainali za Kombe la Dunia mwaka jana. Amepata kutwaa ubingwa wa Uholanzi akiwa na Van Gaal klabuni AZ Alkmaar.

De Gea anaingia mwaka wake wa mwisho United na hajakubali kusaini mkataba mpya, huku Van Gaal akisema hajui kwa nini anasuasua kusaini. Kocha huyo ameeleza wazi kwamba lazima wajiandae vyema msimu huu kwa sababu kuna tishio la kipa huyo kuondoka.

Hili ni ingizo la tano kwa United baada ya Matteo Darmian, Bastian Schweinsteiger, Morgan Schneiderlin na Memphis Depay.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

MAN UNITED WAWAFUNGA BARCA

ROBO FAINALI KAGAME KUANZA KESHO