in , ,

Zidane kocha mpya Madrid

“Zizou”

Real Madrid wamemfukuza kazi kocha Rafa Benitez na kumkabidhi mikoba
hiyo Zinedine Zidane.

Benitez (55), raia wa Hispania, ametimuliwa baada ya kuhudumu kwenye
nafasi hiyo kwa miezi saba tu, uamuzi uliochukuliwa na bodi ya klabu
hiyo katika kikao cha dharura kilichoitishwa na Rais Florentino Perez.

Zidane (43) alikuwa kocha wa kikosi cha pili cha klabu hiyo na ni
mchezaji wa zamani aliyechezea Real na Timu ya Taifa ya Ufaransa kwa
mafanikio makubwa, na baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo alikuwa
na haya ya kusema:

“Nakwenda kuweka moyo na roho yangu katika kazi hii ili kila kitu
kiende vyema,” akasema Zidane ambaye kikosi anachokiacha kilikuwa
katika nafasi yapili kwenye ligi daraja la tatu na amekuwa nao tangu
2014.

Kabla ya hapo, Zidane alikuwa mtu muhimu kwenye benchi la ufundi la
bosi wa Real Madrid, Carlo Ancelotti aliyeongoza timu hiyo kutwaa
ubingwa wa Ulaya kwa mara ya 10 – La Decima.

Rafael Benitez, amekuwa na wakati mgumu pale Real Madrid.
Rafael Benitez, amekuwa na wakati mgumu pale Real Madrid.

Enzi akisakata soka, Zidane alikuwa mmoja wa wale wachezaji muhimu
wanaoitwa ‘Galacticos’ – lebo waliyopewa wachezaji aghali
waliosajiliwa na na Rais Perez katika awamu yake ya kwanza ya urais
hapo Santiago Bernabeu.

Mwaka 2001, Real walitoa ada kubwa ya pauni milioni 45.8 kwa Juventus,
ikivunja rekodi ya dunia na kumnasa kiungo huyo matata ambaye tayari
alikuwa amelisaidia taifa lake kutwaa Kombe la Dunia na la Ulaya.

Akiwa Bernabeu, alicheza na wachezaji aina ya Luis Figo, Raul, Ronaldo
lakini pia na aliyekuwa nahodha wa England, David Beckham. Miaka
mitano kabla ya kustaafu kwake, Zidane aliwasaidia Real kutwaa ubingwa
wa La Liga 2003 na kuchaguliwa kuwa mwanasoka bora wa dunia na Fifa
kwa mara ya tatu.

Msimamo wa La Liga, ukionyesha Real Madrid hawapo wanapotakiwa
Msimamo wa La Liga, ukionyesha Real Madrid hawapo wanapotakiwa

Inaelekea kilichokomelea msumari wa mwisho kwenye jeneza la Benitez ni
kushindwa kuwafunga Valencia wanaofundishwa na kocha chipukizi Garry
Neville, ambapo walikwenda sare ya 2-2 na baada ya hapo washabiki wa
Valencia wakaonesha bango wakimwambia Benitez wanamshukuru kwa kuwapa
zawadi muhimu. Alitoa raia asifukuzwe, bali apewe muda arekebishe
mambo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Chelsea wawafyatua Palace

Tanzania Sports

TETESI ZA USAJILI JANUARI 2016