in , , ,

PSG NI MBOGO WAKIWA NYUMBANI

Santiago Bernabeu, uwanja ambao ulikuwa na nyasi ambazo zilichagua
ng’ombe wa nyumbani kupata malisho.

Kutoka na ubabe wa ng’ombe ngeni tulitegemea kwa kiasi kikubwa
ungemfanya amzidi ng’ombe mwenyeji

Magoli matatu yalitosha kumpa pumzi ndefu mwenyeji, pumzi ambayo
anaenda nayo ƙkatika uwanja wa Parc des Princes.

Uwanja ambao umekuwa siyo salama kwa kila timu inayokanyaga kucheza na PSG.

Uwanja ambao msimu huu PSG wamefungwa goli moja katika michuano ya
klabu bingwa barani ulaya.

3-0, 5-0 na 7-1 ndiyo matokeo ya kikatili ambayo yaliwahi kufanywa na
PSG dhidi ya timu ambazo zilikanyaga nyasi za Parc des Princes msimu
huu.

Magoli 15 katika uwanja wao wa nyumbani na wanahitaji ushindi wa magoli 2-0.

Kitu ambacho kinaonekana chepesi kwao kwa sababu na historia kuonekana
kuwabeba wao.

Msimu huu wamefanikiwa kufunga magoli kuanzia mawili katika michuano
ya klabu bingwa ulaya wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani.

Mwaka 2014 walifanikiwa kuifunga Chelsea magoli 3-1 katika uwanja huo
huo, na msimu wa mwaka jana walifanikiwa kuifunga Barcelona magoli 4-0
katika uwanja wao wa nyumbani.

Kitu hiki ni kielelezo tosha kuwa PSG huwa wanakuwa mbogo kipindi
wanapokuwa wamekanyaga nyasi za uwanja wao.

Viingilio vya mashabiki wao huwa wanavionea huruma, ni mara chache
sana huwauzunisha mashabiki wao katika uwanja wao wa nyumbani.

Katika mechi 19 za msimu huu ambazo PSG kacheza katika uwanja wa
nyumbani kafanikiwa kufunga magoli 76, ikiwa ni wastani wa kufunga
magoli 4 kila mechi.

Safu yao ya ushambuliaji huwa haishibi haraka inapokuwa nyumbani.

Udhaifu wa beki ya Real Madrid inaweza ikawa faida kwa PSG?

Varane na Ramos wamekuwa na kiwango kisichokuwa kizuri sana
ukilinganisha na msimu jana, safu yao ya ulinzi imekuwa ikiruhusu
kufungwa magoli magoli mengi msimu huu.

Mfano katika ligi kuu ya Hispania pekee , wameruhusu kufungwa magoli
29 msimu huu. Na katika michezo 15 iliyopita wamefanikiwa kutofungwa
goli katika michezo miwili pekee.

Michezo mitano iliyopita hawajafanikiwa kupata clean sheet (kutoruhusu
kufungwa goli)

Hii ni kutokana na kiwango cha safu ya ulinzi ya PSG imekuwa siyo
imara sana. Ramos na Varane wamepungukiwa kasi na umakini , Marcelo
amekuwa anaisaidia sana timu inapokuwa inashambulia lakini inapokuwa
inashambuliwa imekuwa ngumu kwake.

Hivo safu ya ulinzi ya ƊReal Madrid isipojirekebisha mbele ya PSG
ambayo ina takwimu nzuri za magoli katika uwanja wao wa nyumbani,
tunaweza kushuhudia PSG akipindua matokeo.

Pengo la Neymar linaweza kuwateteresha PSG?

Anaikosa mechi ya leo, mchezaji ambaye amehusika katika magoli mengi
ya PSG msimu huu.

Leo hii hayupo, ni namna gani PSG wanaweza kucheza bila yeye na
kufanikiwa kupata ushindi siku ya leo?

Kwanza kuna faida kwa kutokuwepo kwa Neymar kwenye mechi hii, moja ya
faida ni PSG kuwa na njia nyingi za wao kupatia magoli.

Asilimia kubwa ya mashambulizi ya PSG hupitia upande ambao Neymar huwa
anakuwepo, sasa leo hayupo kitu ambacho kitamsaidia PSG ni yeye kupata
njia nyingi za kupitishia mashambulizi yao.

Ni mchezaji yupi anafaa kucheza sehemu ya Neymar?

Angel Di Maria, ni mmoja ya wachezaji ambao wanaweza wakawa hawana
sanaa kubwa kama ya Neymar lakini wakawa na madhara ya moja kwa moja.

Ana magoli 17 mpaka sasa katika mashindano haya ya ligi ya mabingwa
barani ulaya.

Hii inatosha kuonesha ana uzoefu ambao unaweza kuwasaidia PSG katika mechi hii

Kipi kitakuwa msaada kwa Real Madrid ili waweze kufanikiwa kuvuka hatua hii?

Moja ya matatizo makubwa ambayo PSG imekuwa ikikumbana nayo hasa hasa
inapokutana na timu kubwa ni eneo lao la kiungo cha kuzuia kutokuwa
imara.

Thiago Motta amekuwa ni mtu muhimu eneo hili lakini anapokosekana
kwenye mechi kubwa PSG huonekana inayumba, leo hii wanamkosa tena
Thiago Motta, kwa hiyo hii inaweza ikawa faida kwa kiasi kikubwa kwa
Real Madrid.

Kiungo cha kuzuia kinapokuwa hakiko imara kina nafasi kubwa sana ya
kuifanya safu ya ulinzi kupokea mashambulizi mengi, hivo kama Toni
Kroos na Luka Modric wakiweka presha eneo la kiungo kutakuwa na nafasi
kubwa kwa Real Madrid kupita hatua hii na kwenda hatua nyingine.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Arsène Wenger: AKILI, MWILI WAKE UMECHOKA

Tanzania Sports

GATTUSO NA ATHARI YA UTU WAKE AC MILAN