*Liverpool na  Middleborough wapigiana 30
*Chekechea Arsenal watupwa nje na Saints

Raundi ya nne ya michuano ya Kombe la Ligi ilikuwa na matukio ya aina yake, ambapo Liverpool waliokabiliana na Middlesbrough waliishia sare ya 2-2 kabla ya kupigiana penati 30 kupata mshindi.

Liverpool walishinda kupitia tundu la sindano, ambapo makipa wa timu mbili hizo nao walipiga penati, katika kile kilichoonekana kwamba ni uhondo wa kuzipiga, nyingi kati ya hizo zikiingia nyavuni pasipo makipa kuonesha ufundi wa kuzizuia.

Ilifika mahali penati 20 zikatumbukia kimiani mfululizo, na kuwa kana kwamba ni mchezo ambao haungekuwa na mwisho, lakini hatimaye Liverpool walifanikiwa kuvuka kwa ushindi wa penati 14-13 kwenye michuano hiyo inayojulikana zaidi kama Capital One Cup.

Mechi hiyo iliyochezwa kwa dakika 120 iliishia 2-2, baada ya dakika 90 za kawaida kumalizika kwa sare ya 1-1 na kulazimisha mikwaju mitano mitano ambayo haikutoa mshindi, wala 10 mingine, ndipo rekodi mpya ikawekwa.

Rekodi ya penati nyingi kupigwa katika michuano hii ni ile ya ya 9-8 iliyotokea mara tatu, baina ya Arsenal na Rotherham in 2004 na Manchester City dhidi ya Stoke na pia ya Aston kuwafunga Colchester zote zikiwa ni za 1982.

Katika michuano ya Kombe la FA, iliyokuwa ndefu zaidi ni ya mwaka 2001, pale Macclesfield walipowafunga Forest Green 11-10 katika raundi ya kwanza.

WATOTO WA ARSENAL WATOLEWA
pichaaaaaaaaaa

Arsenal wametolewa kwenye michuano ya Kombe la Ligi, baada ya kufungwa na Southampton kwa mabao 2-1 katika muda wa kawaida.

Arsene Wenger amerudia mtindo wake wa zamani wa kuchezesha chipukizi, hasa katika eneo la ulinzi, na kwa kiasi kikubwa matokeo hayo yametokana na ukosefu wa uzoefu miongoni mwao.

Alimwanzisha pia kwa mara ya kwanza kipa David Ospina, ambapo mchezaji mwingine mpya, Alexis Sanchez alifunga bao zuri la kuongoza kwa mpira wa adhabu ndogo aliouchonga kifundi, lakini saints walilirusisha na kuongeza jingine.

Wachezaji wa usiku wa Jumanne walikuwa wapya 10 ikilinganishwa na wale walioanza katika mechi dhidi ya Villa. Huko Arsenal walivuna ushindi wa mabao 3-0.

Saints walisawazisha bao kupitia kwa Dusan Tadic kwa penati baada ya Sadio Mane kuchezewa vibaya na kisha Nathaniel Clyne alifunga bao zuri, walilolilinda hadi mwisho, Arsenal wakikosa mbinu za kupenya kusawazisha.

Wenger ameeleza kusikitishwa kutolewa kwao, ikizingatiwa walicheza vizuri, wachezaji walijituma na kutawala mchezo kuliko adui zao, lakini akatetea uamuzi wake wa kuwachezesha chipukizi.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

‘Kombe la Dunia halitafanyika Qatar’

Ukiacha joto, vipi kitisho cha ugaidi Qatar?