in

Maajabu ya refa kupigana na mchezaji uwanjani

Darren Drysdale

Nini kitatokea kama siku moja itatokea refa wa mechi akachukizwa na jambo aliloambiwa na mchezaji? Je ataamua kumjibu au kumwadhibu? Itakuwaje siku refa akiamua kupogana na mchezaji uwanjani kila atakapopishana kauli nao? Mchezo wa soka utakuwaje siku refa akiamua kukunjana mashati na mchezaji? Hayo ni maswali machache yanayozunguka katika tukio la refa Darren Drydale wa huko Uingereza.

Refa Darren Drysdale ameingia matatizoni baada ya kuvaana na mchezaji wa Ipswich Town, Alan Judge mwishoni mwa wiki iliyopita. Drysdale ameingia kwenye mjadala wa mchezo uliopita pamoja na refa Keith Hackett akihusishwa kwenye tukio hilo.

Wakati Kylian Mbappe akiinyanyasa Barcelona katikati ya wiki iliyopita kwa mabao yake matatu kwenye dimba la Camp Nou wengi walitupia macho huko Hispania lakini hakuna aliyekuwa anafuatilia kilichotokea katika barabara ya Portman

Matokeo ya mchezo yalikuwa 0-0 katiya Ipswich Tonw na Northampton Town jumanne hiyo hiyo, refa Darren Drysdale alizusha vurugu uwanjani.

NINI KILICHOTOKEA?

Undava undava
Undava undava

Dakika ya 90 za mchezo huo zikielekea ukingoni, kiungo wa klabu ya Ipswich Town, Alan Judge aliingia katika eneo la hatari na kufanyiwa madhambi na beki wa Northampton, Peter Kioso.

Refa Drysdale hakuona madhambi hayo, hivyo hakuwapa faulo Northampton akiamini kiungo wao Alan Judge amejiangusha. Judge alichukizwa na uamuzi huo hivyo akaamua kwenda kumlalamikia refa Drysdale.

Wakati akilalamika kwa refa huyo akaanza kumnyoshea kidole usoni, jambo ambalo lilimchukiza Drysdale. Badala ya kuondoka eneo hilo au kusimama kuendelea kumsikiliza mchezaji huyo, akaamua kumsogelea zaidi kwa kugonganisha vichwa vyao kama madume ya ng’ombe yakipambana.

Kuparurana huko kulisababisha wachezaji wa Ipswich kuingilia kati ili kutenganisha refa na mchezaji wasipigane zaidi. wachezaji kadhaa walichukua ili kuepusha vurugu ambazo zingeibuka kama wangeachwa waendelee kutunishiana misuli uwanjani hapo.

Licha ya kusukumana kwa vichwa vyao, Drysdale aliamua kumpa adhabu ya kadi ya njano Judge kwa kosa la kujiangusha katika eneo la hatari ili apatiwe penalti.

Kiungo mwingine wa Ipswich, Flynn Downes alishangazwa na hatua ya mwamuzi wa mchezo kutunishiana misuli na kuwa tayari kupigana na mchezaji mwenzake, na aliamua kukaa mbali na Drysdale huku akionekana wazi kupigwa butwaa imekuwaje refa anakuwa tayari kus]rushiana ngumi na mchezaji.

Hakika lilikuwa tukio la ajabu katika mchezo wa soka. baadaye alifikiri kuwa huenda naye atakuwa mcehzaji atakayepigwa kichwa cha refa huyo

Je, alishindwa kudhibiti hasira zake? Kuzawadiwa kadi nyekundu dakika mbili baadaye baada kuvunja sheria.

Drysdale amekuwa mwamuzi wa soka kwa kipindi cha miaka 30, akichezesha mechi za Northern Premier League mwaka 1988. Alikuwa msaidizi wa Graham Poll kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la FA mwaka 2000 na amekuwa mwamuzi wa mchezo wa soka mwaka 2004. Pia anatambuliwa kama mwamuzi msaidizi na Shirikishola Soka Duniani, FIFA na UEFA.

Mwaka 2004 alishinda tuzo ya Combined Services kutokana na umahiri wa kazi katika michezo ndani ya jeshi la nchi hiyo akiwa amefoikia ngazi ya Sajini na amechezesha mechi kadhaa za EFL.

Lakini hilo si tukio la kwanza kwa mwamuzi huyo maarufu kugombana na mchezaji uwanjani. Mwaka 2017 Drysdale alisifiwa kuokoa maisha ya mchezaji mmoja wakati wa mchezo kati ya Chesterfield na Morcambe.

Beki wa Chesterfield Brad Barry alimeza ulimi wake baada ya kugongana na mwamuzi huyo. Drysdale akijua wazi anavunja itifaki ya chama cha soka FA ambayo inaeleza waamuzi hawatakiwi kugusana na wachezaji, lakini Drysdale alimua kumsaidia Barry kumgeuza kutoka alipoangukia ili apate nafasi ya kuendelea kupumua vizuri. Drysdale alivunja sheria lakini aliokoa maisha ya mchezaji.

Kwa kipindi hicho, Drysdale asliema: “Hata kama huruhusiwi kumgusa mchezaji aliyeumia, nilipomwaona akiwa ameanguka vibaya na kushindwa kupumua nikaamua kuingilia kati na kumgeuza ili kumweka vizuri ili kuzuia asiumeze ulimi wake,”

NINI KITATOKEA?

Alhamisi iliyopita ilithibitishwa kuwa mwamuzi Drysdale kuondolewa kuchezesha pambano la Ligi daraja la Pili kati ya Southend na Bolton mwishoni mwa wiki iliyopita.

Bodi yenye mamlaka ya kuajiri waamuzi ilitoa taarifa ya kuomba radhi ya Drysdale, lakini haikueleza zaidi hatua inayofuata. “Ninafahamu ni muhimu kwetu waamuzi kuthibiti hulka zetu wakati wote wa mchezo na kuzungumza na wachezaji kwenye masuala ya kitaalamu tu. Ninaomba radhi kwa kutozingatia hilo na ninaomba radhi kwake Alan Judge na timu nzima ya Ipswich Town.”

Licha ya kuomba radhi jumatano iliyopita, FA imemwadhibu Drysdale kwa kukiuka sheria hivyo huenda akasimamishwa. Drysdale amepewa muda hadi tarehe 4 Machi mwaka huu kujibu tuhuma zinazomkabili za kuvunja sheria za soka.

Tanzania Sports
Arsenal

Ikiwa atatiwa hatiani anaweza kukata rufaa kupitia Tume Huru ya Nidhamu kupitia upya adhabu atakayopewa. Kwamba kesi hiyo inabidi ithibitishwe kwa ushahidi, pia Tume imepewa mamlaka ya kuongeza adhabu kwa kuzingatia uzito wa tukio lenyewe.

Kanuni za nidhamu zinaeleza kuwa ugomvi wa waamuzi,wachezaji na makocha ni wahusika ambao adhabu inayopaswa kutolewa ni kufungiwa. Kwahiyo Drysdale anakabiliwa adhabu mbili za kufungiwa na kutozwa faini.

Kocha wa Ipswich Town, Paul Lambert amelezea kitendo cha kuomba ni chepesi mno na mchezaji wake Judge alikuwa anabiliwa na adhabu ya kufungiwa miezi sita au mwaka mmoja kabla ya kubatilishwa, lakini kama mwanamichezo anamuunga mkono Drysdale.

“Hakukuwa na sababu ya kuomba radhi,” alisema kiungo wa Uingereza, Jack Grealish, huku mchezaji mwenzake wa Aston Villa Trrone Mings alisema “waamuzi wanasababisha presha kubwa. Kila mmoja hufanya makosa, hakuna cha mno katika tukio hilo. Judge alikuwa na bahati wachezaji wenzake waliingilia na kumtuliza.

Tanzania Sports
Paul Lambert

Aidha, hakuna kumbukumbu kama imewahi kutokea mwamuzi kugombana na mchezaji kama alivyofanya kwa Darren Drysdale kwa Ipswich Town.

Kuna wakati mwamuzi maarufu duniani Pierluigi Collina aliwahi kumsukuma Tomas Repka  katika mchezo wa kimataifa kati ya Jamhuri ya Czech na Uholanzi.

Nakumbuka mwamuzi Phil Down alikuwa mtulivu sana alipokabiliana na wachezaji wakorofi ama presha yoyote kutoka kwao. Aliwadhibiti kwa kuzungumza nao kwa maneno bila kushikana mashati.

Tukio la Darren Drysdale limeshangaza mno, ikizingatiwa amefundishwa namna ya kukabiliana na mazingira au matukio yenye kumweka hatarini akiwa huko jeshini. Kwahiyo inapotokea anashindwa kujidhibiti ni jambo linalosikitisha, na linasababisha tafakari hivi waamuzi maarufu wakiamua kuparurana na wachezaji uwanjani mchezo wa soka utakuwaje?

Mwamuzi anatakiwa kuepuka kujiingiza kwenye matukio kama hayo. Kila mtu anayehusika na uamuzi wa mchezo wa soka anatakiwa kuzingatia sheria na tararibu zinazoongoza, hivyo kukabiliana na mazingira ni jambo muhimu kwake na wasaidizi wake.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Wazir Wazir Jr

Yuko wapi Wazir Jr ?

Benjamin Mkapa Stadium Dar

‘Uenyeji’ wa mashindano ya CAF ni heshima Tanzania