in , ,

Ngao ya Hisani imewapa nguvu  Simba

MABINGWA wa Ngao ya Hisani Simba hawakufunga bao katika dakika  90 za kawaida za mchezo dhidi ya Yanga. Hawakufua dafu kupiga mashuti mengi langoni mwa Yanga lakini walikuwa na wakati mzuri kuonesha kuwa wao wana uzoefu wa mechi kubwa. Katika mchezo wa unazokutanisha Simba na watani wake wa jadi, Yanga wanakuwa wakicheza kwa  kuwapa uhuru mwingi Simba. Lakini katika mchezo wa Ngao ya Hisani Yanga waliupiga mpira mwingi na kuwapa mazoezi makali watani wao. 

TANZANIASPORTS Katika tathimini yake imeonesha kuwa Simba wanatakiwa kushukuru kwa mechi mbili kali na kusisimua ambayo imepwa nafasi kujiandaa kwa mashindano ya African Super League. Simba ambao ndiyo wawakilishi pekee kutoka ukanda wa Afrika mashariki wanastahili kwa kunyakua ubingwa wa Ngaop ya Hisani kutokana na mchezo  wao wenye uzoefu na kudhibiti presha yoyote kutoka kwa wapinzani wao. Simba walianza safari ya kufukizia ubingwa huo kwa Singida Fountaine Gate ambako waliibuka kwa ushindi wa penati kama ilivyo kuwa kwa watani wao wa jadi Yanga ambao waliwatupa nje mabwanyenye wa Chamanzi, Azam Fc. 

UMAHIRI WA ALI SALIM

Kabla ya mchezo dhidi ya Yanga, Ali Salim alikuwa narekodi mbaya ya kuokoa penalti. Mashabiki wa Simba walikuwa wamesikitishwa na namna wlaivyotolewa na Wydad Casablanca ya Morocco kwa njia ya matuta, ambako Ali Salim alishindwa kuwabeba wekundu wa Msimbazi. Hata hivyo Salim amewafuta machozi washabiki wa Simba baada ya kupangua penalti 3 za mastaa wa Yanga. Tofauti ya makipa wengine wa Simba waliopo sasa Aishi Manula,Ayoub Lakde na Hussein Abel hakuna mwenye rekodi ya kupangua penalty tatu katika mchezo mmoja. Kwa maana hiyo Ali Salim amekuwa shujaa wa Simba wakati ambao lango lao limekuwa kwenye misikusuko tangu kuumia kwa Aishi Manula. Kwa mchezo uliochezwa dhidi ya Yanga, bado klabu ya Simba inahitaji huduma ya Aishi Manula wakati wanaelekea kwenye mashindano ya African Super League.

SAFU YA USHAMBULIAJI

Kocha Robertinho Oliviera bado anacho kibarua kigumu kuhakikisha safu yake inakuwa moto wa kuote mbali kwenye mashindano ya yajayo. Katika mechi mbili ambazo ni sawa na dakika 180 washambuliaji wa Simba hawajafunga bao hata moja. Si John Bocco, Jean Baleke, Moses Phiri  na wengineo. Hii ni nafasi ya benchi la ufundi kufanyia kazi upungufu uliojitokeza na kuwaimarisha zaidi washambuliaji wao. Kutokana na ubutu wa kupachika mabao, ndiyo maana kocha alilazimika kuanza na safu tofauti ya ushambuliaji, ambapo Jean balake aliwekwa benchi katika mchezo wa fainali na nafasi yake ikachukuliwa na John Bocco. Hali kadhalika benchi la ufundi lina kibarua kigumu cha kumwimarisha Luis Miquissone ambaye akikaa sawa anaweza kurejesha makali yake. Kwahiyo mechi ya ngao ya hisani imeongeza tija kwa Simba kuona namna ya kuiweka timu yao vizuri kabla ya kuanza kw amashindano ya African Super League. 

SAFU YA ULINZI

Hii imeonesha kuwa ipo imara na inaweza kukabiliana na presha yoyote. Kukosekana kwa Hennock Inonga katika mchezo wa fainali halikuwa tatizo kwao, kwani waliopangwa Kennedy Juma na Chemalone walifanya kazi yao vizuri na kuhakikisha nyavu za Simba haziguswi kwa chochote.  Uhakika ni kwmaba safu ya ulinzi ya Simba imekuwa imara na imeonesha namna ambavyo benchi la ufundi linatakiwa kuimaraisha viwnago vya mabeki wake wote ili wawe tayari pale inapotokea dharura. Kwamba Kennedy Juma anakuwa tayari kubeba majukumu ya Inonga au Chemalone endapo litatokea tatizo la majeruhi. 

BENCHI LA UFUNDI

Je kocha Robertinho yupo tayari kwa mashindano ya African Super League? Hili ni swali muhimu na gumu kwa benchi la ufundi la Simba. Hadi sasa benchi hili haliwezi kuwaomba viongozi wao  waandae mechi za kirafiki kwani kucheza mashindano ya Ngao ya Hisani ni sehemu nzuri iliyokisaidia kikosi hicho kujijenga. Lakini Simba wanaelekea kwenye ratiba ngumu za mashindano ya kimataifa na ligi ya ndani, pamoja na kombe la shirikisho ASFC. Hii ina maana benchi la ufundi linatakiwa kunoa makali ya wachezaji kw akutumia mbinu sahihi na zenhye kuipa ushindi pamoja na kuam,ua matokeo ya mchezo mapema. 

Miongoni mwa maeneo wanayotakiwa kutolea uamuzi ni nani aanze kwenye kikosi cha kwanza katika eneo la kiungo mkabajai kati ya Siado Knaoute, Mzamiru Yassin Selemba na Fabrice Ngoma. Eneo la kiungo ndilo injini ya timu, si la kubahatisha au kutegemea linabadilisha matokeo ya haraka kwa timu. Ni eneo ambalo linabadilishw akwa nia ya kuimarisha ulinzi, lakini ikitokea timu haijafunga na inatakiwa kusaka ushindi basi maeneo yanayolengwa ni kiungo wa ushambuliaji, mawinga na washambuliaji. Ni wakati wa benchi la ufundi kutilia mkazo juu ya nani aingie kikosi cha kwanza na yupi akae benchi ilia je kuongeza nguvu ya ulinzi pale timu inapokuwa inaongoza mabao na kuhitaji kuyalinda. 

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

70 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Simba kuna vita kali, msimu utawaka moto

Tanzania Sports

Jurgen Klopp ataumaliza msimu huu salama?