in , ,

MWAMUZI ALITUNYIMA USHINDI TANZANIA

Jana kulikuwa na mechi ya timu ya taifa ya Tanzania pamoja na timu ya
taifa ya Benin.

Mechi ambayo timu yetu ya Taifa ilikuwa na idadi kubwa ya wachezaji
wenye majeraha kwenye kikosi chao.

Kiliwakosa watu muhimu kama nahodha wa timu ya taifa Mbwana Samatta.

Je kulikuwepo pengo la Mbwana Samatta?

Kukosekana kwa Samatta kulikuwa na hasara na faida yake pia kwenye
mechi ya jana.

Hasara ilikuwa wapi?

Kukosekana kwa Samatta kulimlazimu kocha Mayanga kutumia mshambuliaji
mmoja ambaye ni Maguli.

Huku nyuma yake akiwepo Raphael Daudi.Raphael Daudi hakuwa na uwezo
mkubwa sana wa kumlisha mipira Maguli kipindi cha kwanza, nafasi hii
ndiyo ilionesha pengo la Mbwana Samatta.

Samatta angeweza kucheza kama mshambuliaji wa pili ili atoe huduma
stahiki kwa Maguli.

Kuingia kwa Mbaraka Yusuph na kumwacha nje Ajib nje haukuwa uamuzi
wenye tija kwenye timu.

Kuingia kwa Ajib kucheza kama mshambuliaji wa pili kungeongeza tija
kubwa kwa sababu Ajib ana uwezo mkubwa kutengeneza nafasi za magoli na
kufunga.

Kumwingiza Ajib kama mbadala wa Kichuya kiliondoa uwiano kwenye timu.

Kwa sababu kipindi cha pili Kichuya alianza kuingia katikati uwanja
akitokea pembeni.

Hii ilikuwa inaleta idadi kubwa ya wachezaji katikati ya uwanja. Hivo
kuleta uwiano mkubwa mzuri eneo la katikati ,ambapo ongezeko la watu
wa eneo hilo la katikati lilileta nguvu kubwa sana eneo lile.

Mchezo wa kirafiki kati ya Tanzania na Benin

Baada ya Ajib kuingia hakuwa na uwezo wa kuingia katikati ya uwanja
kuongeza idadi ya watu katika eneo hilo.

Mabadiliko yenye tija kubwa yangeonekana kama Ajib angekuwa mbadala wa
Raphae l Daudi na Kichuya kuendelea kuwepo ndani ya uwanja.

Faida ya kutokuwepo kwa Samatta ilikuwa ipi?

Timu ilicheza kitimu bila kuwa na mawazo ya kumtegemea mchezaji mkubwa.

Ilikuwa sahihi kwa Himid Mao kucheza kama beki wa kulia?

Mechi ilimwihitaji Himid Mao kama kiongozi na mchezaji mwenye kiwango
kikubwa, lakini haikimwihitaji katika sehemu ya beki wa kulia.

Mwalimu Mayanga alikuwa na Maganga Boniface kama beki namba mbili.

Ambaye alitakiwa kumwamini kuliko kumpeleka Himid Mao upande wa beki
wa kulia, hali iliyomfanya aonekane katika kiwango kikubwa.

Himid Mao, alifaa kuanza kama kiungo wa kati kwa kuchukua sehemu ya
Hamis Abdalah,ambaye alionekana kutokuwa na hali ya kuiamrisha team
kwenda mbele.

Kumweka Maganga Boniface pamoja kama beki wa kulia na kumwanzisha
Himid Mao na Mudhathir Yahaya katika eneo la katikati ya uwanja
kungekuwa na tija kubwa sana.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

MOHAMMED IBRAHIM, KIVULI CHA HARUNA KINAKUZIBA, TOKEA MLANGO WALIOTUMIA KINA TAMBWE NA AJIB

Tanzania Sports

YUPI NI MWAKILISHI BORA WA AFRICA KOMBE LA DUNIA?